Bora wewe upo urusi.
Eti kwanini urusi hataki Ukraine ajiunge nato?
Kwasababu NATO iliundwa kujihami dhidi ya USSR ileee ilikuwa inatisha siyo Urusi kibogoyo,
Ndoto za USSR kuitawala Dunia zilizikwa mwaka 1991 baada ya kusambaratishwa!!
Pamoja na wao kudhoofika Lakin NATO ameendelea kuwa imara na kuongeza wanachama!!
Hili Suala linamkera sana Kiongozi wa Urusi ambaye ana ndoto za kudhani siku moja anaweza kurejesha UMOJA huo!!
Mbaya zaidi wanachama wanaoongezeka NATO ni wale waliokuwa USSR,
UKRAINE katika historia ya Urusi ni zaidi ya Estonia Au Lithuania Au Moldova, UKRAINE ndo hata mji mkuu ulitumika Kiev haikuwa MOSCOW!!
Wana intellijensia wengi wa Urusi wana mshikamano na Ukraine na pia siri nyingi za Ukraine wanazijua Urusi na Urusi Kama kuna Taifa linalojua sana mambo yake ya ndani basi ni UKRAINE
Ndo maana hata Ki UKRAINE ni sawa na Kirussia Kwa asilimia zaidi ya 60 ila ki Estonia Au Lativia Au Macedonia language hazifikii hata asilimia 5 ya ufananano na mrusi
Lingine Urusi anaona Ukraine akijiunga na NATO position ya UKRAINE Kwa Urusi ni hatari zaidi kuliko zingine, maana wana Mauripol, Odessa na ile Donbass ni eneo ambalo ni angle nzuri ya kuishambulia Urusi Kama ikitokea ulazima,
Lingine Russia naye anataka atengeneze empire yake kwamba naye ana vinchi vinamtegemea .
Kwenye masuala ya biashara na uwekezaji hata kuwauzia baadhi ya vitu, in case Ukraine akajoin NATO hizo privileges zimeisha sasa,,,,,
UKRAINE INA NATURE YAKE YA MAZINGIRA NI NZURI KUZALISHA URANIUM SANA SANA SANA YAAN SANA hata ZILE Silaha za Nuclear alizo nazo Russia ni Ukraine alimpa Miaka ya 90 ili apewe uhuru wa kujitegemea Kwa mambo yake, na hiyo ilikuwa ni makubaliano
Akachukua silaha zoote za Nuclear akampa Urusi,,
Sasa Russia akiona Hii ni hatari kuwaruhusu NATO KUWEKA MKONO PALE
Kimsingi makubaliano ya UKRAINE Kubaki Neutral hayana mashiko tena kwakuwa sasa Miaka imesharuhusu na Ukraine ni Taifa HURU hapangiwi awe na urafiki na nani na awe na uadui na nani,
Juzi nilikuwa Albania nimekutana na familia ya Kirusi ambayo wameenda huko baada ya Kutishwa kusapot upinzani Yaan walikuwa wanafanya kazi kwenye platform ya Telegram na wakawa wanaendekeza mijadala ya siasa na kutoa taarifa zaidi za Upinzani.
Jambo ambalo lilimkera Putin wakaamua kukimbia, hiyo familia ya Yuria Kononenko wameshare na mimi mambo mengi sana na kwenye kitabu ntakacho andika kuna mengi ntayaweka,
Ila Urusi Kwa sasa wanaona kuna haja ya kuacha uongozi wa ubabe na udikteta ndo inapelekea kufanya maamuzi ya hovyo na kuvamia nchi nyingine bila kushauriana na walio wazunguka
ILA KWA SASA URUSI MAMBO MENGI YAMEMSHINDA NA HII INAWEZA KUWA TERM YA MWISHO YA PUTIN
BRITANICCA ENCYCLOPEDIA