Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA


Umetoa mfano mzuri unaoimarisha hoja yangu.

Ni hivi:

Kwenye kituo ulichosimamia Tundu Antipas Lissu alipata kura 79 na Magufuli akapata kura 31.

Lakini Lissu alindikiwa kura 6 na Magufuli kura 379.

Kisha unauliza, "sasa hapo unakubali vipi?"

Majibu yangu:

Kama ni kweli, kura 6 alizoandikiwa Lissu ni sehemu ya kura zake halali 79 ulizozishuhudia.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa maelezo yako, Lissu aliibiwa kura 73.

Hivyo basi, tunapaswa kukubali kwamba kura 6 ni kura halali, na kuendelea kudai kura 73 kwa kuweka vielelezo mezani.

Hizo kura 6 ambazo tunajua kwamba ni halali ni sehemu ya kura ambazo zimetangazwa na NEC na kuzaa wabunge wa viti maalum 19.

Kwa hiyo, viti maalum 19 vya Chadema ni halali.

Katika kituo chako ulichosimamia, ambacho sio halali, kama kikitibitika, ni kutotangazwa kwa kura 73.

Hizi kura 73 ziendelee kudaiwa bila kuharamisha kura 6 ambazo ni halali.

Wanasheria wote wa Chadema wanaujua ukweli huu.

Tafuta yeyote umwulize na atakwambia ninachokwambia.
 
Jamani, wewe umeona hadithi za X na Y pekee?

Umeruka ruka mistari kwenye hoja zangu mbona?

Labda ninyooshe mstari wa hoja yangu.

1. To defeat your enemies you must outpeprform them.
2. To outperform your enemies you must out-think them
3. To out-think your enemies you must infiltrate them (Ndio maana tuna maafisa vipenyo kila sehemu nyeti).

Kwa sababu hizi tatu, tunahitaji wabunge wa viti maalum ili wawe maafisa vipenyo wetu bungeni, hata kama hotuba zao hazitasomwa.

Hapa nimeongea kisumbawanga kigumu, naomna unisamehe

Tehe tehe tehe....
 
Wenye akili ndogo hawawezi kuelewa
 

Huu udadavuzi unatambua kuwa jiwe alipata kura A lakini ikatangazwa B ambapo:

B >> A

Hako ka symbol:

">>" Husomeka kama "much greater."

Hapo napo ushauri wako bado unasimama? Labda kama gunia tupu!

Kwanini isiwe haki bin haki tu?

Unaona kwanini msimamo wa CDM bni muafaka zaidi? Maalim na akaone ya CDM na kuyafanyia kazi.

Hapendwi mtu!
 
🚮🚮🚮🚮



Kwa tabia za namna hii, kama hayati Samwel Sitta akifufuka leo na kurudia kauli yake kwamba Chadema hawana sifa ya kupewa nchi kwa sababu bado hawaonyeshi ukomavu wa kifikra, utapinga vipi tuhuma hiyo? Shit!
 
Mama amon TULIA umwandalie mumeo maji ya kuoga.

Habar za siasa waachie wanaume
 
With all due respects, I beg to differ with your conclusion.
Mtu akifuatilia kwa makini uchambuzi wako atagundua kuwa umeupiga chenga uchambuzi wako ili ufikie conclusion uliyoitaka.
Jinsi ulivyoanza na ulivyihitimisha ni moja ya miujiza.
 
Mama Amon, ktk hili naomba niazime maneno ya Jakaya; "za kuambiwa changanya na zako."

Kama kuna usanii umefanywa na NEC dhidi ya Chadema (na kuna uwezekano wamefanya hivyo) wametufanyia sisi wapiga kura, hivyo Chadema kugomea kuteua wabunge wa viti maalumu hawafanyi hivyo dhidi ya CCM wala Bunge/Ndugai bali dhidi ya hao NEC. Kama NEC wanao uwezo wa kuwagawia kura wasistahilli, basi wateue na Wabunge wa viti maalumu.

Vv
 
Embu acheni vyokovyoko buana si mlitaka muwe peke yenu na mmefanikiwa !!? Sasa tatizo nini ?

CHADEMA WAMESEMA HAWAYATAMBUI MATOKEO NA MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI KITU AMBACHO NAWASAPOTI SANA.

CCM TULIENI PIGENI KAZI ....HAPA KAZI TUU.
 
Lakini kama Chadema imeamua haitaki viti maalum na kiti kimmoja cha jimbo,labda uongozi wa Chadema ina mpango kazi.
 
Kwa heshima, sikubaliani na kauli yako hii hapa.
Kwani mwajiriwa aliyelipwa milioni tatu hapo juu, akazipokea, na kisha akaendelea kudai ziada, alikuwa ameunga mkono ufedhuli wa mwajiri mkorofi?
CHADEMA HAWATAMBUI MCHAKATO MZIMA SASA HIVYO VITI MAALUM NAVYO CHUKUENI NINYI MABIGWA YAANI.

ZAMANI MAMA AKIKUCHAPA TULIKUWA TUNAGOMA KULA...KUMBE UNAJIUMIZA MWENYEWE JAPO MAMA NAE HUUMIA NDIO CCM SA HIVI.
 

Narudia tena mama Aron, sina shaka na uwezo wako wa kujenga hoja, ama ubora wa hii hoja yako. Hivyo sujibu mstari kwa mstari wa hoja zako zene wingi wa busara, ila tulichokiona kwenye uchaguzi, na maumivu watu waliyopatiwa, kushiriki hilo bunge ni kuhalaliisha uharamia, na dakika za mwisho itaonekana wapinzani wanawapeleka watu wakaumizwe ili wao waingie bungeni? Sikutarajia kama mama Aron unaweza kuhalalisha uharamia hata kama una nia njema.
 
Mbona ubabe wa mwenyekiti wenu huusemi? Tulieni mnyolewe.

Endeleeni kujenga nchi wapinzani walikwamisha sana maendeleo.
 

Nianzie kwenye signature yako...

"We define things as we are, and not as they are.." by Anais.

Huyu Ananias anakupotosha, achana naye.

Katika mtazamo wa realism, tunaongozwa na correspondence theory of truth.

Truth is out there to be discovered.

Sasa turudi kwenye hoja.

Wewe na mimi tunajua fika kwamba pale NEC HQ kuna dawati la TISS.

Ulishawahi kufuatilia dawati hili kazi zake?

Huenda hapana, na sio lazima.

Lakini, kubwa ni kwamba, kuna lawama zinaelekezwa kwa NEC kimakosa.

Natamani kusikia na sijasikia:

Chadema wanasema walipata kura ngapi? (X)
NEC wametangaza kura ngapi? (Y)
Nani ameshikilia tofauti ya kura kati ya X na Y, yaani Z=X-Y?
Aliwezaje kuzishikilia?
Tunaweza kumnyang'anya kura hizo ili ziende kwa Chadema?

Maswali ni mengi...

Tuzidi kutafakari pamoja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…