Tatizo la CCM na Samia ni kiburi tu. Familia 99% nchi 1%

Tatizo la CCM na Samia ni kiburi tu. Familia 99% nchi 1%

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Tatizo la CCM na Samia ni kiburi tu. Familia 99% nchi 1%. Je hii ina maana gani kama nchi

1. Mzunguko wa Pesa umepungua na utapungua kwasababu uwekezaji umepungua, watalii wamepungua na uwekezaji utapungua. Kwa mfanya biashara sasa atapata riba ya juu sana kama anakopa bank za nje kuja kuwekeza Tanzania kutokana na hali na mazingira ya sasa. Hivyo wafanyabiashara watahakikisha wanalipa wafanyakazi kidogo, wanaajiri kidogo na wanaongeza bei ya vitu ili kufidia gharama za mikopo.

2. Kwasababu ya hali mbaya na siasa za kibabe wafanyabiashara wataficha zaidi nje ya nchi mfano kama wewe ni mfanyabiashara wa utalii utaona ni bora pesa za watalii zibaki kwenye bank zao huko nje kuliko kuleta Tanzania nchi ambayo haieleweki kwa sasa

3. Uwekezaji sasa mwingi kwa kanda yenu unaenda Kenya kwasababu pamoja na ukabila wao Kenya wana katiba nzuri inayolinda wawekezaji, mahakama ambayo ni muhula unajitegemea na hautumiki kisiasa kama Tanzania na bado wamaweza kuchukuwa rasilimali kwa kutumia mgongo wa EA community kwenye mambo ya kodoi yaani wanaweza kuja kama wakenya na kuchukuwa Gold, makaa ya mawe bila kuja Tanzania moja kwa moja.

Yote haya yanatokea kwasababu serikali yetu kwasasa inapigana na wananchi wake ambao hawaitaki na wanataka haki badala ya kujenga hali nzuri za uwekezaji. Hali nzuri hatuwezi tena kupata kwa katiba hii na uongo na utamaduni wa wizi na udanganyifu tulionao.

Hivi Kenya kwa mfano blog gani imefungiwa, mwanaharakati gani kafungiwa, chama gani pinzani kimefungiwa, mwanasiasa gani ana kesi ya uhaini?

Ukijiuliza yote haya ndiyo sababu tunamuona Rutto yuko na Trump na wanapewa pesa za uwekezaji na Mama Samia yuko anakimbizana na watoto mtaani. Mama Samia ni lazima aelewe watoto wapo na watakuwepo wakati Mama Samia hayupo.

Mama Samia atatuachia kitu gani cha maana zaidi ya familia zao kuiba pesa!!! na marafiki zao. Watu wa ndani ya CCM bila kubadilika Chama chenu kitakufa gafla ni bora muanze kusikiliza wananchi
 
Back
Top Bottom