Mzizi Mkavu, hii topic imenigusa sana na kwa kweli imenirudisha nyuma kwa miaka mingi sana ,namimi nilikuwa kama huyo binti anayesumbuliwa na hilo tatizo,mimi bila ya kuona haya nilisumbuka sana mpaka ilifikia nina miaka dhidi ya huyo binti lakini bado nilikuwa naendelea kukojoa kitandani mpaka ilifikia kulazwa chini ili nisiharibu magodoro pale nyumbani kwa grand wangu Dar.
Ni kweli concept ya mashetani kudhuru watoto ninaiamini kabisa,when things got so serious nilisafirishwa kwenda Ujiji kwa Wamanyema na nilipofika kule nilitambulishwa kwa bi mkubwa mmoja mtu mzima na alinipangia ratiba yangu ya matibabu na huduma. Kwanza nilifanyiwa kitu inaitwa nyungu ili kumuondoa huyo adui aliyekuwa mwilini mwangu akisababisha mimi kukojoa kitandani na halafu baada ya kufushwa nyungu nikapewa mafusho ya kujifukiza kila siku na dawa ya kunywa,amini au usiamini problem ilisimama mara moja na m[paka narudishwa Dar nilikuwa tayari tatizo limeisha ondoka,lo ilikuwa ni kasheshe moja mbaya sana na kidogo iniharibu akili yangu.
Jamaa mwenye huyo binti ni lazima apigane sana kuliondoa hilo tatizo,maana muda ukipita sana itashindikana kumtibu,ninaye cousin sister wangu mmoja yeye naye alisumbuliwa na hiyo kitu mpaka ikashindikana kuolewa,wako wengi mitaani tunasikia kuwa yule mwanamke ni kikojozi hawezi kuolewa na ikitokea kuolewa basi hakai kwa mme ataachwa na kurudishwa nyumbani kwao.
Simtishi jamaa lakini kila matatizo yana solutions zake,eventualy binti atatibika wala wasiwe na wasiwasi kabisa na anachotakiwa ni kulifikisha hilo suala ndani ya family yake na akifanya hivyo dawa itapatikana asitie shaka kabisa.Ila experience yangu kuhusu hilo tatizo ilikuwa ni mbaya sana ilifikia mpaka performance yangu shule ikawa affected vibaya sana kwa hilo tatizo,ni kweli kuhusu mashetani nakumbuka nilikuwa nikioteshwa ndoto za ajabu ajabu kila siku na baada ya hizo ndoto ndio tukio la kujikojolea kitandani lilikuwa likinitokea, hii ni kitu very serious sana na nampongeza huyu mwana forum kwa kujitokeza na kutafuta solution ya kumtibu binti yake na pia naamini hii topic itaweza saidia watu wengine pindi wakikutikana na same issue, ukweli hii topic leo imenigusa sana na kunirudisha utotoni Dar.
M/Mpamba.