Habari wanajamvi mambo vipi, no mara chache naandika nyuzi huku jf katika hili naomba tumsaidie.
Nina mdogo wetu mmoja wa kwetu huko mkoani kwa sasa yupo Kibaha hapa ana tatizo kukojoa kitandani na ni mtu mzima ana miaka 28 kwa sasa namnukuu "Kaka tatizo hili ninalo muda mrefu toka nipo mdogo mpaka sasa na nina elimu ya chuo kikuu nimeishi kwa wasi wasi sana mara.nyingi nimekorofishana na.watu nilowahi kaa mabweni ya mtaani ilinibidi.nipange chumba cha peke yangu ili niondokane na.aibu hyo.japo si mara zote lkn jambo hili ni la aibu sana sana,"" hayo ni machache waungwana dogo aliongea kwa uchungu akilia pia anasema amehangaika sana sana kutafuta tiba bado tatizo liko palepale akaongeza kuwa imebidi aishi kwa unyonge sana sana. Kama mtu.anajua mtu ama hospitali inayoweza kutibu hlo tatizo pm namba zenu nitampatia awatafute jamani. msaada wenu hata kuoa dogo anaogopa siku za usoni maana ni aibu sana. Nawasilisha asante