Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Kukojoa kitandani ni tatizo la kisaikolojia zaidi,hii ni tiba mbadala isiyo na madhara ya aina yoyote,chukua ndevu za maindi (mahindi mabichi yakikomaa yanakuwa nu uzi uzi nyekundu hivi nimeamuaz kuziitz ndevu ingawa linwezw kuwa si jina lake sahihi) chemsha kwenye maji na uwe ikinywa mpaka tatizo litakapokwisha.
 
Ukikutana na wenye majibu ya kunya umu utaambiwa na wewe mkojolee! Kuna mwanangu alkuwa na tatizo ilo tulilisort out kwa kuhakikisha kabla ya kulala anakojoa na mid night pia twamwamsha na kukojoa. With time likaisha!
 
Atakua ana infections kwenye kibofu pengine ni UTI binti yangu hakuwa anakojoa kitandani nilipoenda mcheki hospt ikagundulika na UTI kali sana. Njowepo umenchekesha hapo juu!!
 
naomba ushauli mke wangu anatatizo la kukojoa kitandani

Pole sana mwambie apunguze unywaji wa maji/juice kuanzia saa moja usiku pia mjaribu kutafuta Alarm ya kuwashtua zile saa ambazo mara nyngi huwa anakojoa. Kwa mfano kama anakojoa saa saba za usiku basi sita na nusu za usiku alarm itegeshwe ili iwaamshe kabla hatafanya vitu vyake kitandani.
 
Pole sana mkuu,kwakuwa unakabaliwa na tatizo fuata ushauri mzuri pia achana na wale watakao kukejeri.
 
Kujibu nashindwa kwani sababu nyingi, matibabu ni muda mrefu, mda sina , pole. train heR!!! uh...!!! niandikie private msg naweza pata muda ipitia na kukusaidia. Jibu hii!! ila vidonge vipo hata dar madukani. bei nafuu!!!
 
Pole sana. Mwambie apunguze unywaji wa maji/juice kuanzia saa moja usiku pia mjaribu kutafuta Alarm ya kuwashtua zile saa ambazo mara nyngi huwa anakojoa. Kwa mfano kama anakojoa saa saba za usiku basi sita na nusu za usiku alarm itegeshwe ili iwaamshe kabla hatafanya vitu vyake kitandani.

B kweli unavyosema kuset muda ule ambao anakojoa itasaidia sana hata mtoto ukishajua muda wake hakupishida kukojoa
 
Jamani hakuna jambo baya kama kukojoa kitandani.na admit,nilikuwa nakojoa kitandani mpaka kwenye miaka 14.kufika 15 ndio nikaacha for good.nikilala naota mkojo umenibana,naenda chooni kukojoa,kumbe naumwaga hapo hapo kitandani. Ilikuwa so embarrassing. Kutaniwa nilishataniwa, ila sikupelekwa hospitali wala nini,baadae nilikuja kuacha.mpaka sasa,sielewi tatizo lilikuwa nini.kama kuanika godoro nje, nilishaanika sana.mtoa mada kuhusu mke wako, I feel her pain,bora uwe unamuamsha amsha usiku.au labda hospitali wanaweza kukusaidia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kimsingi ctofautiani na wachangiaji waliopita nakusihi jaribu kumsaidia na kamwe usionyeshe kunyanyapaa kiukweli kwa mtu niliepitia wakati mgumu kama huo ninajua jinsi gani anavyokosa amani moyoni mwake bt kama anakunywa pombe mwambie aache.
 
Chukulia kama flavour za ndoa wala usitafute kidonge. Chukua ushauri wa kutokunywa maji/juice kabla ya kulala halafu mwamshe usiku apunguze mkojo kama ni tatizo la kila siku.

Ajabu kama ni la kushitukiza usihofu kawaida hadi uzeeni mtu anaweza kujikojolea kama bahati mbaya hasa unapoota uko porini unazunguka kichaka..hamadi..umelowesha kitanda, ipotezee not a big deal
 
naomba ushauli mke wangu anatatizo la kukojoa kitandani
Kukojoa kitandani (Bed wetting):

Kama mtu anakunywa maji kabla ya kwenda kitandani (ndiyo, hiyo ni sahihi, kabla ya kwenda kitandani), hatajikolea kitandani. Kile anapaswa kufanya ni kunywa maji mengi zaidi. Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha hidrojeni na ‘naitrojeni' (nitrogen) kwa pamoja na kuunda amonia. Amonia ni sumu kwa mwili wa binadamu. Wakati ubongo unapata ujumbe kutoka kwa kibofu cha mkojo kwamba amonia ipo katika kibofu cha mkojo, ubongo hukusababishia ndoto uote upo bafuni, kisha utajikojolea. Unafikirishwa upo chooni kwa ajili ya kukojoa!

Hivyo jibu kwa tatizo la kukojoa kitandani ni kujirundika kwa Amonia katika kibofu cha mkojo, Amonia hurekebishwa kirahisi kwa kunywa maji mengi zaidi.

Tembelea www.maajabuyamaji.net kujifunza namna tunavyopaswa kunywa maji kila siku, na nini hutokea mwilini inapotokea tunaipa miili yetu maji ya mgawo (tunapokunywa baada ya kusikia kiu)!.
 
mnunulie pampas tafuta cd ya mrembo kikojozi itakusaidia

My dear ushauri huo wa popansi si mzuri, ina maana akitaka kufanya mzee si atacheleweshwa? mara avue mara limbane mzee si atakosa raha?
 
Back
Top Bottom