Sina shaka hamjambo members.
Nisaidieni chanzo cha tatizo hili na utatuzi wake: Binti yangu mwenye umri wa miaka miwili anapata choo kikubwa kigumu mara zote. Kuna dawa nimewahi kumpa kwa ushauri wa pharmacist fulani,ni vidonge ambapo anameza kimoja na kupata choo laini,lakini baada ya siku mbili hivi anaanza kupata choo kigumu tena.
Katika muendelezo huo,hivi sasa anaonekana kupata maumivu ya tumbo,hali inayompelekea kulia sana hasa usiku. Si muda mrefu sana(takriban miezi miwili) alitumia dawa za minyoo na sasa anamalizia co-trimoxazole baada ya kumpima mkojo na kugundulika kuwa ni mchafu kiasi.
Ana tabia ya kula udongo anapocheza mbali na uangalizi.
Nisaidieni jamani.