Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

pole sana mkuu
jaribu kunywa maji karibu lita mbili,kutwa mara 3
 
Pole kula mapapai, fanya mazoezi au fanya vegitable fasting. Ukishindwa ntafute ntakupa njia mbadala.+255 689 417 472
 
Kwa haraka nenda phamacy wambie wakupe castor oil,hii ni dawa nzusri sana,iko kama mafuta ya kupikia,ukipata kunywa nusu yake ndani ya mda wa dk 6 utakuwa umepata choo laini wala hutachanika,baada ya hapo nenda maabara ukachukue stool.
 
...kafanyiwe oparesheni ndogo teh teh, its a joke,majibu mazuri umepata,piga papai ila hizi njia zoote sidhani kama zitasaidia mara ya kwanza maana uchafu tayari umeshajiunda na kujikusanya tayari kutoka...
 
kunywa maji glas mbili baada ya dk kumi kunywa juice ya ukwaju baada ya nusu sasa leta mrejesho hapa!
 
Nasumbuliwa siku kama ya 6 sijapata haja kubwa na leo nilihisi kupata ila ndo kigumu nimeshindwa naogopa kupasuka,.Nifanyeje jaman
Ok! Kunya hunyi, but jee unajamba?
Na kama Unajamba, unajamba vipi? Jee unajamba yusuf, unapiga bastola au ripua mabomu?
...
Kula maharage kwa wingi upate kujamba! Si unajua dalili ya mvua ni mawingu!
 
Ok! Kunya hunyi, but jee unajamba?
Na kama Unajamba, unajamba vipi? Jee unajamba yusuf, unapiga bastola au ripua mabomu?
...
Kula maharage kwa wingi upate kujamba! Si unajua dalili ya mvua ni mawingu!

duuh, can't help but smile!! majanga
 

Angalizo:Juice ya ukwaju ni nzuri lakini kama utaifakamia bila kipimo sahihi,UTAHARISHA badala ya kupata choo laini hivyo inywe kistaarabu.

Vipi lakini kiongozi,unakula kweli milo kamili? au unashindia mapera mabichi? Maana siku 6 sio kitu cha kawaida!

Anyway,Ukianza kuhisi na maumivu makali ya tumbo na kiuno wakati huu jua intestinal obstruction inakuhusu ambapo operation itakuhusu na ukichelewa utumbo unaoza,Guess what!You'll definitely die.STUKA,
 
habari. tatizo la kushindwa kupatahaja kubwa linatokana na nini? na ukipata haja kubwa unapata choo kigumu sana tena kinaweza kutoka na damu afu unapata maumivu makali sana baada ya kutoa huo uchafu. hii inasababishwa na nini na nini tiba yake.
 
hiyo hali inaitwa constipation, ni pale ambapo unakuwa hauna na enough fibre kwenye mfumo wa chakula solution ni kula matunda kama mapapai
 
Mimi ninatatizo na maji ya asubuhi nikiyanywa ninapata choo laini mno kiasi cha kutisha je na hili linaweza kuwa tatizo gani?
UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
naomba unijulishe castor oil ni mafuta ya aina gani na yanapatikana wapi....
 
Kwa uzoefu wangu kwa hili tatizo dawa hii hapa chin ni kiboko ya matatizo
Hilo tatizo litakuwa hostoria kama utafanikiwa kuipata hii product
Ukihitaji ni pm au npigie 0752720276 ntakusaidia
 

Attachments

  • 1398423360415.jpg
    1398423360415.jpg
    8.6 KB · Views: 176
  • 1398423401953.jpg
    1398423401953.jpg
    53.2 KB · Views: 176
  • 1398423426658.jpg
    1398423426658.jpg
    9.5 KB · Views: 344
Back
Top Bottom