Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

rejea maelezo hapo juu,choo kimekuwa kigumu na kinatoka kwa maumivu mno,hatua kadhaa zimechukuliwa bila mafanikio,hatua zilizochukuliwa kunywa maji mengi,kutumia mapapai,juisi ya ukwaju.........nasubiri ushauri wa kitaalamu.........................natanguliza shukrani
Binafsi nilikuwa na tatizo hili. Nilipewa aloe gel juice. Ya lita moja tatizo limeisha. Inauzwa elfu 40. Lakini itakusaidia sana. Na utapona kbsa. Uyu bro ndo alinipatia 0713297066. Namshukuru sana.
 
rejea maelezo hapo juu,choo kimekuwa kigumu na kinatoka kwa maumivu mno,hatua kadhaa zimechukuliwa bila mafanikio,hatua zilizochukuliwa kunywa maji mengi,kutumia mapapai,juisi ya ukwaju.........nasubiri ushauri wa kitaalamu.........................natanguliza shukrani

Gilo24

Kula hizo papai zako, kula parachichi(avocado), ndizi mbivu, mtindi, nyanya(tomato),pera(guava) na kunywa maji moto kikombe kimoja.
Fanya matembezi ya kilomita mbili,tatu..kama unaweza kukimbia, timua mbio kama kilomita mbili,tatu. Utoke jasho kidogo.

Ukirudi kunywa tena maji moto( uvuguvugu, sio ya kuunguza) vikombe viwili au chai halafu usikae mbali cha choo. Hata utapokwenda matembezi au kukimbia, chukua mfuko wa plastiki akiba.

Halafu uendelee kula matunda na mboga mboga, usingoje mpaka upate tatizo
 
Mkuu Gilo24 UKOSEFU WA CHOO:

Soma tiba rahisiUKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.


Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.


Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.


MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.


NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.


NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.


Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu. Chanzo:MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
article.htm
Mtu yeyote anayepata walu mlo mmoja kwa siku na kupitisha kati ya siku moja au tatu bila kupata choo, anatatizo la kukosa choo (Constipation), pia kupata choo kigumu na maumivu makali ama kufikia kutoa choo kama mbuzi wakati mwingine kikiwa na matone ya damu ni dalili za tatizo hili la kukosa choo.

"Tafiti zinaonesha kuwa mtu anaweza kupoteza maisha iwapo atakosa choo siku tano mpaka saba mfululizo"

Sababu za kukosa choo ziko nyingi ikiwa ni pamoja na:-
•Kukosa mlo kamili ama kula vyakula viingi vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta,
•Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike,
•mifumo hatarishi ya maisha (Dangeraous Lifestyles) kama vile matumizi ya pombe na sigara kwa wingi,
•Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika milo yetu,
•Maji yasiyo salama,
•Kuvuta hewa chafu,n.k

Hizi ni baadhi tu, na hadhari zake zaweza kuwa:-
•Chakula kutomeng'enywa vizuri (poor function of digestion system)
•Maumivi makali wakati wa kupata choo,
•Uchafu uliokaa muda mrefu kugeuka sumu,
•Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.

Hii yaweza sababisha magonjwa sugu kama:
•Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer)
•Presha (Arteriosclerisis)
•Kuongezeka uzito (Obesity)
•Tumbo kujaa gesi
•Magonjwa ya Ini
•Figo kushindwa kufanya kazi vizuri,
•Magonjwa ya ngozi,
•Kukakamaa kwa mishipa ya damu,
•Kisukari,
•Magonjwa ya moyo n.k

SHAKE OFF dabo 2.jpg

Sote twaweza kuwa sehemu ya utatuzi wa maradhi haya, tuwasiliane iwapo wapenda kushiriki katika kutatua tatizo hili. nitwangie 0716927070. TEMBELEA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI
 
Shake Off Phyto Fiber zinapatikana duka gani hapa Dar?
 
Kwa hapa Dar fika ofisini Karibu na soko la kisutu au piga 0716927070 kwa maelekezo, utaletewa pia waweza nunua pitia online popote duniani. HAPA
 
Wasalaam sana wakuu,
nina zaidi ya mwaka mmoja nimekuwa najisaidia asubuhi tu mara niamkapo,na mchana hata nileje siendi choo hadi asubuhi.na hiyo asubuhi nikishajisaidia tu ninaanza kujisikia kichefuchefu haswa kwakati wa kuswaki.naomba mwenyekujua kama ni tatizo anijulishe.
NB,nimeshapima choo na kukuta sina tatizo na sina vidonda vya tumbo pia.
 
Kupata haja kubwa na kukojoa ni subjective. Kuna mwingine anaweza kuwa anapitisha siku mbili bila kunya. Kwani we mwanzo ilikuwaje?
 
Mwanzo ilikuwa hata mchana au jioni naweza enda choo.hii hali huwa inanisaidia wakati wa safari njiani hata nile vipi simsumbui dreva kuchimba dawa
 
Acha woga broda upo fresh kabisa, mie huwa nakunya kila baada ya siku mbili and all it noramlly happen at the same time.
 
Labda Wataalamu waseme watu wajisaidie mara ngapi kwa wiki au kwa siku
ndio better
 
once a day ni sawa tu.
inategemea na chakula unachotumia pia. the process mpaka inabakisha chenji ya wewe kutoa, ndo maana huwa mara nyingi asubuhi payload iko tayari for delivery. Umeshajaribu kupitisha hiyo asubuhi bila "ku-download hiyo attachment" ili u-resume baadae? what happens?

Choo chako ni kigumu unapoenda haja? bornagain amekupa option nzuri ya mapapai na maji, pia waweza kutumia juisi ya ukwaju.
pungusa soda, na pia unaweza kutafuta digestive biscuits. kila la heri Marire
 
Last edited by a moderator:
Acha woga broda upo fresh kabisa, mie huwa nakunya kila baada ya siku mbili and all it noramlly happen at the same time.

Hizi Id nyingine bwana si ungejiita kabisa boro yanki
 
Acha woga broda upo fresh kabisa, mie huwa nakunya kila baada ya siku mbili and all it noramlly happen at the same time.

wewe una matatizo tena si kidogo ndugu! una ugonjwa wa constipation na usipofanya utaratibu sasa utapata madhara baadae ingawa si makubwa ila mabaya kuwa nayo! Kwenda haja kubwa inatakiwa japo mara moja kwa siku lakini siku mbili?! nemda hospitali ndugu....!
 
Hyo co ishu mkuu,ni mazoea 2 uliyojiwekea kulingana na ratiba zko za kila cku,ndo mana mwili unafatisha hivyohivyo!otherwise cdhani km unatatzo mkuu
 
Back
Top Bottom