Kwa sasa unaendeleaje mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mimi ilinianza tarehe 24-25 April niliumwa kichwa, mwili kama unachemka ila joto halipandi.
Nilitapika na kuharisha pia(hii baadae niliambiwa ni minyoo), kupima malaria, typhoid, hamna, wakasema nna UTI.
Nikawa fresh kidogo, ila tarehe 26 April nikawa nakohoa kohoa, 27 April kukohoa ikakata hapo ndio nikapotez harufu na ladha,nakumbuka pilipili kichaa niliitafuna bila kuhisi chochote.
Nilivyoperuzi nikahisi ni symptoms za Covid-19,braza wangu ni daktari yupo Turkey ndio akaniambia hii ni Covid-19 kwamba kashakuwa na cases kama hizo nyingi kule.
Hapo kabla ya mimi, wadogo zangu na jirani walishapitia hali hiyo na washkaji wengine kama watano pia.
Nikawa nameza panadol kama anti-pain( kutuliza kichwa, au kama utahisi homa), azuma kama anti-bacteria infections( kukinga kutopata pneumonia), nilipiga nyingine kwa ajili ya ile ishu ya minyoo.
Ila hapa kwenye minyoo ndio naamini kuwa hawa wajuba wakikuingia mwilini halafu wakakuta una kaugonjwa wanakupelekesha mbio, maana kuwa na minyoo nilikuwa nahisi kichefu chefu zaid, na kushindwa kula kabisa yaani na kutapika.
Hali ikaja kukaa sawa yenyewe, sikunywa tangawizi wala limao.
So kama hauna changamoto zingine hiyo hali inakata yenyewe, dogo zangu wame recover bila ya dawa.
NB:
kama ni Covid-19,bado unaweza kuwa positive hata week 3, so tukae mbali na watu wenye matatizo ya kiafya, ( vaa barakoa, beba sanitizer ili tusiambukize wengine)
Pia, kujilinda muhimu kwa kuwa unaweza kupata tena infections.
Alexander The Great