Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Asante mkuu...
 
Jamani habari zenu,

Mimi naombeni mnisaidie hivi mshawahi kukutana na watu wanaosweat mikononi na miguuni? Kwa anayejua tiba ya hii kitu msaada tafadhali, yani hii hali ni chukizo kwangu mpk najisikia vibaya mwenye anaweza nipa suluhisho ya hii kitu msaada plz.
 
Nliwah kuskia kuwa ni dalili ya ugonjwa.. fulani ila sina hakika.
 
Subiri wataalamu wanakuja.. kukupa tiba... Ila sidhani kama ni tatizo
 
Same[emoji1751]
 
Pole sana. Jaribu kwenda hospitalini na ueleze kwa daktari kwa kina juu ya tatizo lako.
Ama nenda hizi diagnostic centre na ufanye Serum TSH, free T3 na free T4 level
 
Shikamoni wakubwa, Wadogo marahaba.

Ndugu zanguni ni muda wa miaka mingi sasa nimekuwa na tatizo la kufumkwa na jasho kwa kiwango kisicho cha kawaida.

Tatizo hili limenianza tangu nikiwa na miaka 17 sasa nina 35,mwanzo watu walikuwa wakinitania eti ni afya bora.

Hali hii imedumu kwa mda mrefu sasa naona imezidi na imeanza kunitisha,kinachonishangaza nikioga kabla ya dakika 10 naanza kutokwa jasho.

Wakati wa kunywa chai au chakula huwa nalowa kabisa hadi watu hunishangaa nkiwa mgahawani au sehemu yoyote nitakapokuwa nakula.

Naweza kutokwa jasho hata wakati wa baridi mbaya zaidi nikikaa karibu na feni jasho hilo hugeuka chumvi nakuanza kuwashwa hususani napofanya kazi ngumu au kutembea umbali mrefu.

Wakuu mpaka naandika uzi huu hali hii imekuwa mbaya tena usiombe nikiwa faragha na..........inakuwa kero hadi najiskia vibaya hata mwenzangu maana kitanda hulowa kwa jasho.Nisaaidieni ndugu zanguni maana ushauri wa kwanza nautegemea jf kabla ya hatua zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…