Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Uoga, uvutaji wa sigara, unywaji wa vilevi...

Tafakari, chukua hatua..
 
Alianza lini na hilo Tatizo? Kama ni tangu alipokuwa mdogo sina la kukuambia. Ila kama limemuanza uzeeni basi ni vizuri ukampeleka akafanyiwa vipimo vya Kidney. Kama anazo symptoms nyingine unaweza kuzisema??
 
labda nikimuona ndiyo naweza kujuwa anasumbuliwa na nini hasa, anaishi wapi? ana uzito gani?
 
Nnavoelewa kutoka jasho ni moja kati ya faida za kufanya mapenzi, hapo unaua cells zote mfu, unaunguza calories, pia ngozi inajisafisha, na vinyweleo vinapata oksijeni safi. Usihofu si tatizo hata ukitoka jasho la ulimi
 
Wadau naomba kupata maelezo kuhusu tatizo hili.Kwanza ni kwamba chumba ninacholala kina nafasi ya kutosha na huwa naacha dirisha wazi lakini napata tatizo la kutokwa na jasho sana mgongoni na kifuani.

Na mbaya zaidi siwezi kulala bila kujifunika. Na wakati mwingine hutokea kama nilikunywa pombe then siku mbili zinazofuata nisinywe.

Nawakaribisha kwa ushauri.
 
Habari zenu ndugu zanguni.

Nina mtoto mwenye umri wa miaka mitatu. Mtoto huyu amekuwa akitokwa na jasho jingi iwe asubuhi, mchana, jioni hata usiku. Akila anatokwa na jasho. Akilala jasho linammwagika na akilia pia jasho linamfumuka.

Hata kama ni kipindi cha baridi yeye huwa anatokwa na jasho.

Mtoto huyu si mlaji sana ila ni mnywaji sana wa maji.

Je, hali hii ni kawaida au kuna tatizo? Nini chanzo?
 
Ni kweli, inawezekana ni maswala ya homoni hazijakaa vizuri hormonal imbalance au maambukizi (infection). Hii inaitwa Hyperhidrosis
[h=2]Key points[/h]
  • Hyperhidrosis is the term for excessive sweating (kutoka jasho kuliko kawaida).
  • There are 2 types of hyperhidrosis. One type occurs over the entire body. The other type occurs on certain parts of the body such as the underarms, soles of the feet, palms of the hands, and face.
  • Your child's doctor can diagnose hyperhidrosis with an exam, simple starch iodine tests, or a paper test.
  • There are many treatments that your child's doctor may recommend. Lakini pia kuna kumweka kwenye maji na kupitisha umeme dogo ili kuharibu mpangilio wa homoni na pia kuweka mazingira mazuri ya kupata hewa na ubaridi (kuwa karibu na mtoto mwenye tatizo hilo umfundishe namna ya kuepuka mazingira ya joto na kukosa kupunga upepo)
 
Habari wataalam wa hili jukwaa,

Kuna mtoto mchanga wa miezi mitano ana kilo 7 amekuwa na tatizo la kutokwa na jasho sana hata wakati wa baridi na hii hutokea muda wote si mchana wala usiku. Imefkia ata kuvalishwa nguo nyepesi ili kusolve tatizo lakini bado linaendelea.

Naombeni msaada wenu wataalam kama itakuwa ni tatizo la kiafya.Mkoa anaoishi ni mwanza na nyumba ina madirisha ya kutosha na ni makubwa.Asanteni
 
Kuna jamaa yangu mmoja anasumbuliwa sana na tatizo la kutoka jasho kwenye viganja vya mikono na miguu hali hii inamfanya kukosa raha hasa anapokuwa na mpenziwe kwani awezi kumshika shika pia anashidwa kusalimu kwa kupeana mkono anahofia tatizo lake.

Kasema awezi kuvaa viatu vya wazi ni ishu sana mda mwingi yeye uvaa viatu na soksi nzitonzito. Mimi nilishidwa kumsaidia sababu sijui chochote juu ya tatizo hili sasa kama kuna mtaalamu anayejua juu ya hii issue atueleze chanzo cha tatizo hili na tiba yake au ushauri tumsaidie mwenzetu.
 
Ugonjwa huo unaitwa HYPERHIDROSIS.
Kawaida tunatoka jasho ili kuupoza mwili.Mwili unapokuwa na joto nervesystem inatuma ujumbe automatic kwenye sweatglands ili kupunguza joto.Unapokuwa na hyperhydrosis hizi nervesystem zina kuwa zinafanya kazi pasipo na mpangilio na zinatuma ujumbe wakati wote kwahio jasho linatoka hata kama mwili hauna joto.
Hali hio pia inaweza kusababishwa na mtu kuwa na sukari ya chini,hyperthyroidism au side effects za dawa.
Zipo njia tofauti za kutibu kama
  1. Aluminium chloride solution ambayo unaweka kwenye viganja vya mikono na miguu.
  2. Potassium permanganate.
  3. Nimeshawahi kuona botox ikitumika pia lakini ni tiba ya muda hali hio hujirudia.
  4. Iontophoresis:Njia inayotumia kupitisha maji chini ya ngozi kwa kutumia umeme.
  5. Upasuaji kwenye nerve ambazo zinahusika na jasho.
Hizo njia nilizokutajia zinapunguza dalili za ugonjwa huo lakini haziondoi tatizo,njia kama za upasuaji na umeme sidhani kama zinatumika!
Asante Doctor wangu gorgeousmimi huu ndio ugonjwa wangu mimi hapa nilipo ninatoka maji kwenye viganja vya mikono na nyayoni pasipo na sababu yoyote ile maji kila wakati kwenye viganja na kwenye nyayo hongera bibi.
 
Last edited by a moderator:
Ugonjwa huo unaitwa HYPERHIDROSIS.

Kawaida tunatoka jasho ili kuupoza mwili.Mwili unapokuwa na joto nervesystem inatuma ujumbe automatic kwenye sweatglands ili kupunguza joto.Unapokuwa na hyperhydrosis hizi nervesystem zina kuwa zinafanya kazi
pasipo na mpangilio na zinatuma ujumbe wakati wote
kwahio jasho linatoka hata kama mwili hauna joto.
Hali hio pia inaweza kusababishwa na mtu kuwa na sukari ya chini,hyperthyroidism au side effects za dawa.
Zipo njia tofauti za kutibu kama
  1. Aluminium chloride solution ambayo unaweka kwenye viganja vya mikono na miguu.
  2. Potassium permanganate.
  3. Nimeshawahi kuona botox ikitumika pia lakini ni tiba ya
    muda hali hio hujirudia.
  4. Iontophoresis:Njia inayotumia kupitisha maji chini ya ngozi kwa kutumia umeme.
  5. Upasuaji kwenye nerve ambazo zinahusika na jasho.
Hizo njia nilizokutajia zinapunguza dalili za ugonjwa huo lakini haziondoi tatizo,njia kama za upasuaji na umeme sidhani kama zinatumika!

Mkuu asante sana kwa msaada wako ila nilitaka kufahamu zaidi kuhusu namna ya kupata hizo tiba na gharama zake ili nimueleweshe jamaa yangu vizuri..!!
 
Asante sana huo ni ugonjwa wa wengi na inakera kwelkwel mi had simu nahisi inatapigwa short make hadi nimalize kuandika sms inakuwa yote imelowa na mijasho!
Msaada sasa hizo dawa zinapatikana wapi? Kwenye Pharmacy kweli zipo?!
 
Mimi nina hii condition na huwa natokwa jasho hasa mikononi hadi naona karaha muda mwingine

Ni hali inayotuathiri psychologically zaidi; kujishtukia, kutotoa mikono wakati wa salamu n.k

Ngoja kwanza nifute jasho mikononi :A S cry:

Nimeshawahi kutumia hizo drysol (Aluminium chloride solution na Potassium permanganate) bila mafanikio yeyote

Botox ni temporary solution na ni gharama sana huku Iontophoresis inaelezwa kuwa njia bora zaidi ya kutibu na salama lakini sijui mahala wanapotoa huduma hii bongo

Cha muhimu kuwa msafi penda kuosha mikono yako mara kwa mara na kutumia hand sanitizer oftentimes na uwe na kitambaa cha walau kukausha mikono yako pindi jasho likizidi

Mwanamama wangu anapenda mikono yangu so far anadai ni laini (labda ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa sijui!!); thou kweli watu tulio na tatizo hili huwa na mikono laini

Muhimu: usiwe mtumwa wa tatizo hili fanya mambo yako na jamii itakuzoea tu.
 
Hizo dawa nyingine ulizipata hospitli gani au pharmac zinapatikana na gharama zake je..??
 
Nimeshawahi kutumia hizo drysol (Aluminium chloride solution na Potassium permanganate) bila mafanikio yeyote Botox ni temporary solution na ni gharama sana huku Iontophoresis inaelezwa kuwa njia bora zaidi ya kutibu na salama lakini sijui mahala wanapotoa huduma hii bongo

Hizo dawa nyingine ulizipata hospitli gani au pharmac zinapatikana na gharama zake je..??
 
Je ugonjwa huo unasababishwa na ni nini hasa . Au linatokea kwa mtu wa umri gani au mazingira gani. Je kuna njia ya kuzuia tatizo hilo kabla . Na je lisipotibiwa kabisa madhara yake ni nini?
 
Maswali yako yote yamejibiwa hapo kwenye post ya kwanza. Ni ugonjwa unaweza kupata mtu yoyote!hakuna madhara yoyote zaidi ya kutoka jasho na kuaibika!
 
Jamani naombeni msaada kwan hili tatizo la kutoka jasho kwapani linaninyima raha na ata uhuru wa kuvaa nguo.

Je nitumie dawa au deodrant gani..?msaada plz.
 
jamani kwapa zangu zinatoa jasho mpaka nakosa uhuru wa kuvaa nguo., navaa nguo nyeusi tu.,naombeni msaada nitumie deodorant gani au dawa gani.,msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom