Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Anzia hospital kwanza, kuhusu huyo specialist nenda hata Mwananyamala hospitak au pale namanga hospital ENT wake hua anapatikana kila jumatatu saa nane mchana nenda one day before kuweka appointment kumuona specialist ni sh.30000 kama sijakosea..... kama mfuko hauko poa nenda hospitali za serekari ... harufu mbaya mdomoni ni kero kwako na kwa wengine na inaweza hata kukukosesha kazi na mengineyo mengi
 
Kwanza kuwa na mazoea ya kuongea na wenzako kwa karibu tena unawakaribia makusudi, ukiona katika maongezi unaeongea nae anarudisha kichwa kwa nyuma ujue hali si shwari, kuna watakaokuambia na kuna ambao hawawezi kukuambia bali vitendo vyao vitakupa jibu.

Chukua uzi upalaze kwenye ulimi wako kuanzia nyuma ya ulimi wako kuja mbele mara moja tu, kisha utoe uzi unuse, ukiona uzi unanuka ujue hali si shwari.

Chukua kiganja chako cha mkono kigeuze upande ambao huwezi kupokea kitu ramba na ulimi wako kisha subiri kidogo hadi mate yatakapokauka, kisha nusa, ukiona kiganja kwa nyuma kinanuka basi ujue hali si shwari.

Chukua nyuzi zile za kusafishia meno sijui kwa kiswahili fasaha zinaitwaje!, pitisha pitisha kwenye upenyo wa meno yako, kisha nusa ukiona kamba inanuka ujue hali si shwari, domo linanuka

Hivi mtu unaweza kujijua kama unatoa harufu mbaya mdomoni? Kama kuna njia ya kuweza kujichunguza ili kujua naomba mnijuze...

We kiganja cha mkono kwenye mdomo, pumua hapo then nusa
Njia hii haiwezi kukupa jibu kama mdomo wako unanuka au haunuki
 
Wadau,

Naombeni ufafanuzi wa tatizo hili la kinywa kutoa harufu mbaya.Yaani muda ukitoka kusugua ama kuswaki tu ndiyo hakitoi harufu ila ukitulia kidogo labda masaa kadhaa harufu mbaya inarudia palepale hata kama hujala kitu!

Naombeni kujua tatizo ni nini na suluhisho lake.

Ahsanteni.

Tatizo linaweza kuwa ni kinywani au tumboni, ninakushauri tumia huu udongo wetu wa asili, unaukoroga kijiko kimoja cha chai kwenye glass moja ya maji baada ya kupiga mswaki na unakunywa asubuhi mara moja na usiku mara moja. Utaona mafanikio baada ya siku mbili tatu tu:Kwa wanaume na wanawake: Udongo (natural) Unaolainisha ngozi sasa unapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
 
Watu wengi wanatoa harufu mbaya ila hawajijui mpaka upate mtu wa karibu akwambie, Ukipiga mswaki sugua na ulimi.
 
Pia inatakiwa kuwa na mazoea ya kujisafisha kwa kidole kabla hujaanza kuswaki.

Chukua kidole cha shahada au chochote ambacho kwa upande wako utaona kitafika kirahisi chini ya ulimi wako karibu na koromelo, utakuwa unajigoa na mwanzoni mimacho itakuwa inakutoka kama mjusi aliebanwa na mlango, hiyo isikuogopeshe ni sehemu ya usafi. Jitahidi kuchokonoa uchafu kuuvuta kwa kidole kisha unaosha kidole, na unaendelea tena mpaka pale utakapoona mate mazito ya ute ute yamepungua/yamekwisha/yamemalizika kisha sukutua ukiwa unaangaalia juu huku maji ukiyachezesha mlio wake "(khrurrrrrr)" kwa japo nusu dakika (sekunde thelathini au ukipenda endelea mpaka pale utakapojisikia inatosha) kisha tema, rudia zoezi hilo mara kadhaa upendavyo.

Baada ya hapo anza kuswaki kama kawaida.

Na pia kuwa na kawaida ya kusafisha kuta zako za mashavu kwa ndani na kwenye mafizi nje na ndani, inasaidia mafizi yako kutokuwa na weupe weupe fulani mithili ya ukungu mweupe
 
Wadau,

Naombeni ufafanuzi wa tatizo hili la kinywa kutoa harufu mbaya.Yaani muda ukitoka kusugua ama kuswaki tu ndiyo hakitoi harufu ila ukitulia kidogo labda masaa kadhaa harufu mbaya inarudia palepale hata kama hujala kitu!

Naombeni kujua tatizo ni nini na suluhisho lake.

Ahsanteni.
je unaswaki mpaka ulimi?
 
Watu wengi wanatoa harufu mbaya ila hawajijui mpaka upate mtu wa karibu akwambie, Ukipiga mswaki sugua na ulimi.

Yupo mdau amesema tutumie baking powder. Nimetumia naona harufu imepungua sana ingawa bado ipo kwa mbali ila nikipigia mswaki asubuhi, ikifika jioni saa 11 tayari harufu inarudi. Swali langu, haina madhara?
 
Kwanza kuwa na mazoea ya kuongea na wenzako kwa karibu tena unawakaribia makusudi, ukiona katika maongezi unaeongea nae anarudisha kichwa kwa nyuma ujue hali si shwari, kuna watakaokuambia na kuna ambao hawawezi kukuambia bali vitendo vyao vitakupa jibu.

Chukua uzi upalaze kwenye ulimi wako kuanzia nyuma ya ulimi wako kuja mbele mara moja tu, kisha utoe uzi unuse, ukiona uzi unanuka ujue hali si shwari.

Chukua kiganja chako cha mkono kigeuze upande ambao huwezi kupokea kitu ramba na ulimi wako kisha subiri kidogo hadi mate yatakapokauka, kisha nusa, ukiona kiganja kwa nyuma kinanuka basi ujue hali si shwari.

Chukua nyuzi zile za kusafishia meno sijui kwa kiswahili fasaha zinaitwaje!, pitisha pitisha kwenye upenyo wa meno yako, kisha nusa ukiona kamba inanuka ujue hali si shwari, domo linanuka

Njia hii haiwezi kukupa jibu kama mdomo wako unanuka au haunuki
Sasa Mkuu, saidia tiba. HARUFU
 
Yupo mdau amesema tutumie baking powder. Nimetinumia naona harufu imepungua sana ingawa bado ipo kwa mbali ila nikipigia mswaki asubuhi, ikifika jioni saa 11 tayari harufu inarudi. Swali langu, haina madhara?

Ina madhara baba.Baking powder ni kemikali.Itayaharibu meno yako yawe dhaifu.Inatoboa meno.
 
Pia inatakiwa kuwa na mazoea ya kujisafisha kwa kidole kabla hujaanza kuswaki.

Chukua kidole cha shahada au chochote ambacho kwa upande wako utaona kitafika kirahisi chini ya ulimi wako karibu na koromelo, utakuwa unajigoa na mwanzoni mimacho itakuwa inakutoka kama mjusi aliebanwa na mlango, hiyo isikuogopeshe ni sehemu ya usafi. Jitahidi kuchokonoa uchafu kuuvuta kwa kidole kisha unaosha kidole, na unaendelea tena mpaka pale utakapoona mate mazito ya ute ute yamepungua/yamekwisha/yamemalizika kisha sukutua ukiwa unaangaalia juu huku maji ukiyachezesha mlio wake "(khrurrrrrr)" kwa japo nusu dakika (sekunde thelathini au ukipenda endelea mpaka pale utakapojisikia inatosha) kisha tema, rudia zoezi hilo mara kadhaa upendavyo.

Baada ya hapo anza kuswaki kama kawaida.

Na pia kuwa na kawaida ya kusafisha kuta zako za mashavu kwa ndani na kwenye mafizi nje na ndani, inasaidia mafizi yako kutokuwa na weupe weupe fulani mithili ya ukungu mweupe
Baba nimejaribu kutumbiza kidole cha shahada kohoni.Nusura nife kwa kupaliwa na kukosa hewa safi..Bahati majirani walinipa msaada wa huduma ya kwanza.
 
Last edited:
Tiba wadau wengi wameshafunguka kwenye huu uzi.

Cha kufanya wewe pitia maoni kuanzia mwanzo wa uzi mpaka mwisho.

Na pitia ingia kwenye link alioiweka bibie Zainab Tamim.

Kama huamini wengi wanaonuka midomo ni uchafu, kama una kawaida ya kujisafisha kohoni, mara moja moja kuna kipindi kunatoka kibuja au vibuja kama viwili hivi, hebu jaribu kuvibonyeza viwe kama mbatata iliochemshwa kisha ikasagwa na unuse, uone itakavyonuka.

Ukiona unabonyeza na hainuki ujue unazingatia usafi.

Tiba ni kwa wale walio na matatizo, lakini ukichunguza wengi wao wenye matatizo ya kunuka mdomo ni uchafu (kutozingatia usafi wa vinywa vyao) kitu ambacho si maradhi bali ni uchafu
Sasa Mkuu, saidia tiba. HARUFU
Baba nimejaribu kutumbika kidole cha shahada kohoni.Nusura nife kupaliwa na kukosa hewa safi..Bahati majirani walinipa msaada wa huduma ya kwanza.
Pole sana.

Mwanzo mgumu, endelea kujizoesha itafikia muda utazoea.

Kama nakuona mimacho ilivyokutoka kama mjusi aliebanwa na mlango vile
 
Last edited:
Back
Top Bottom