Shukrani sana mkuu kwa kutoa ushuhuda wa dawa hii.Mungu akubariki sana kwani umesaidia na wengine wasio amini!Baosita ubarikiwe sanaaaa mkuu nimepona kabisa fangas sina tena nimesumbuka nazo miaka 6 mpaka ilifika najichoma na maji ya moto ndo nilale. Azantesna mkuu
nashukuru mkuu. ngoja nijiandae kuitengenezaMkuu Raia Fulani tumia kama dawa sio tena unakula kila siku hakuna wasiwasi tumia hakuna matatizo.
Shukrani sana mkuu kwa kutoa ushuhuda wa dawa hii.Mungu akubariki sana kwani umesaidia na wengine wasio amini!
Hiyo minyoo itakwisha ukishatumia hii dawa mkuu.Utaona njaa haikuumi tena hovyo.Nami naenda kujaribu maana nimekuwa nikisumbuliwa na minyoo kila mara na nakunywa dawa oolaa! Asante mkubwa.
Mkuu hapa singoji kitu vitungu swaumninavyo ndani fastar natengeneza kesho ntachek fangas wangu wapoje namiaka sita nasumbuliwa na fangasi miguuni baada ya sikutano ndo ntakuja kutoa tarifa rasmi
hii dawa inatibu kila kitu??
hahaha nilikomesha amoeba kwa kutumiia njia hii. yaani kuna kipindi amoeba walikuwa wananitesha nikinywa dawa baada ya muda naumwa tena na dawa zenyewe za Amiba kama unavyoziju zinachafua. Aah nikajisemea ya nini kuhangaika nikatengeneza juisi ya vitunguu Swaumu yaani niliviponda kama punje thelathini nikachanganya na ndimu/limao mbili kisha nikailaza usiku wote. Kesho yake nikaanza kuitumia kama robo glass kutwa mara mbili kwa siku kama tatu.
Baada ya hapo sikusumbuliwa tena na amoeba labda niwe mzembe kwa kula vichafu. Ingawa mmh vitunguu vilikuwa vikali siku ya kwanza nilivyokunywa asubuhi tu nilivyoamka bila kula chochote wee huo mchemsho kama nusu saa hivi baada ya hapo kama masaa mawilii niliharisha na choo nikakisikia ni harufu ya vitunguu swaumu tu.
Ila tahadhari usiweke kwenye chombo cha chuma hasa mchanganyiko huo unapokuwa umechanganya na asali maana hufanya sumu.
Nilisumbuliwa na mimi tumbo miaka kibao.Nimejaribu leo kama siku ya tatu sisikii maumivu tena,kwa kweli ndugu uliyetoa tiba kupitia jf Mungu akubariki sana.
Tuache kudanganya watu. Fungus haziwezi kuponyeshwa na kitunguu swaumu na kwa kutumia dose ya kitunguu kimoja tu.
Je kwa mwanamke mwenye ujauzito wa miezi minne hii dawa haiwezi kuleta madhara[/QUOTE
Adm Kwa hapa labda Mzizi Mkavu atusaidie ingawa kwa mimi nahisi anaweza kutumia vitunguu swaumu kwa kupunguza makali yake yaani kama mimi nilivyo tengeneza then badala ya kuinywa robo glass tena kwenye tumbo tupu apunguze kipimo cha kunywa tena anywe baada ya kula maana nasikia kutumia kiasi kikubwa cha vimiminika vichungu kwa mwanamke mjamzito haishauriwi maana husababisha mimba kuharibika.
Ingawa hii ya vitunguu swaumu sijui kama iko kwenye kundi la vitu vichungu mi naona iko kwenye kundi la vitu vikali ila kwa kuwa ina antibiotique so matumizi yake kama dawa lazima yawe na viwango.
Kwa yeye pia kama kinga ya magonywa mengi naamini anaweza kuitumia mahali pengi mfano akitengeneza saladi ili kujiepusha na minyoo angalau achukue punje mbili au tatu akatie vipande vidogovidogo achanganye na hiyo saladi. itamsaidia ila kwa ufafanuzi zaidi ngoja tusubiri wataalamu.
kama hujasikia kichefu chefu na maumivu tumboni, itakuwa umetumia garlic ya kichina. Jaribu garlic ya mbeya uone muziki wake.Nimetumia leo, kwanza sijasikia kichefuchefu wala kujisaidia kabisa wala haina ucxhungu hebu nione mpaka kesho nione
kama hujasikia kichefu chefu na maumivu tumboni, itakuwa umetumia garlic ya kichina. Jaribu garlic ya mbeya uone muziki wake.