Tatizo la Maji na Ukame: Lawama zangu zote ni kwa Waziri Lukuvi na Waziri wa Mazingira

Kwangu mimi naona hii inaweza kuwa ni mipango ya kutuandaa kisaikolojia ili tukubaliane na tutakacholetewa nahisi si ajabu wakatokea wakina aptl wa kutosha lakini swali la msingi hapa ni je hii timu mpya iliyosajiliwa ndio tunaona haya mambo kwa nini sasa tusidhani huu usajili unajambo tusilolijua? Mbona wachezaji wa zamani hatukuona wala kusikia haya? Na je huu ukame wa miezi miwili tu gafla unatia shaka? Kwa kweli mwenda zake sikuwahi kumkubali ila kwa sasa kuna mambo nahisi alikua sahihi ngoja tusubiri dakika tisini
Kama upo kanda ya Ziwa panda basi hadi Dar

Kama upo Dar panda Basi kwenda kanda ya Zina Au Iringa au Dodoma, ukikuta mito 5 inatiririsha maji tena kwa Kiwango kizuri nitafute nikupe hela.
 
Tulisema hili mapema kabisa ile bodi mpya ya Tanesco iliundwa kwajili ya kutengeneza channel za upigaji.

Soon watatangaza umeme wa kuzalishwa kwa mitambo ya kutumia mafuta mazito ili wale wafanyabiashara walioko kwenye bodi ya Tanesco wapige hela.

Waziri Makamba ni mshenzi sana
 
Nyie kwa nini mnang'ang'ania mito tu wakati nchi hii kuna maziwa, mvua kila mwaka, bahari? Nchi hii ina sehemu nyingi ambazo maji ya kuchimba yako karibu. Kwa nini unang'anga'ania mito tu???
Kama upo kanda ya Ziwa panda basi hadi Dar

Kama upo Dar panda Basi kwenda kanda ya Zina Au Iringa au Dodoma, ukikuta mito 5 inatiririsha maji tena kwa Kiwango kizuri nitafute nikupe hela.
 
Kuna diwani mmoja kule kwetu Iringa juzi katuma mapicha kwenye account yake ya facebook eti anajisifu wanachimba kisima cha milioni 50 kwenye zahanati.!

Nikishangaa sana,

Hivi sehemu kama Iringa tena kule dabaga mito kila sehemu ni kwa kupoteza milioni 50 kuchimba kisima?

Sehemu kama kigoma unaweza kukuta nako kuna uhaba wa maji wakati ziwa lipo pale pale!

Na alafu tulivyo wapumbavu, huwa tunatafuta watu wakuwatupia zigo kama hivi.
 
Kuna muda ni lazima ukweli usemwe maana usiposemwa lazima kumbukumbu zitakuwa za upotoshaji Mkubwa

Kwenye Tatizo linaloikumba Tanzania la ukame na ukosefu wa Maji kwa sasa lawama zangu zote nazipeleka kwa watu wafuatao

1. William Lukuvi
Akiwa Waziri wa Ardhi kuanzia Awamu ya Tano, nchi yetu imeshuhudia urasimishaji mkubwa sana wa Mapori ya akiba pamoja na hifadhi kuwa makazi ya watu!

Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana uharibifu wa Mazingira hasa ukataji Miti wa kutisha kwenye mapori mengi yaliyokuwa yanategemewa kuleta mvua uliofanywa na Jamii za wafugaji na wakulima hasa kwenye mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora, Morogoro, Pwani na kusini mwa Tanzania.

Mfano wa hili nimejionea kwenye Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora inayoongoza kwa kuwa na Misitu mingi.

Kwenye mikoa hii kumekuwa na uvamizi sana wa maeneo yenye mapori na misitu ya asili unaofanywa na Jamii za watu wa mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Watu hawa wamekuwa wakikata miti kwenye mapori kwa Kiwango cha kutisha na hata sasa takwimu zimeanza kuonesha hivi karibuni mito iliyokuwa ikititirisha maji mwaka mzima kwenye mikoa ya Kigoma na Katavi bila kusahau Rukwa imeanza kukauka kutokana na shughuli hizi za binadamu.

Waziri Lukuvi akiwa waziri wa Ardhi badala ya kushauri Serikali watu hawa waondolewe kwenye maeneo haya na kurudishwa kwenye maeneo yao ya asili yeye amezidi kushauri serikali watu hawa kurasinishwa kwenye maeneo hayo. Hivyo tusilaumu mtu. Tatizo ni Lukuvi

2. Mawaziri wa Mazingira kuanzia Awamu ya 3,4,5 na huyu wa Awamu ya 6

Hii ni Kwa sababu Nchi yetu imekuwa na Mawaziri wa Mazingira kwenye Awamu zote. Ila kamwe nchi hii haijawai kuwa na kampeni kubwa ya upandaji Miti.

Kila siku watu wamekuwa wakisema juu ya ukame na ukataji mkubwa wa Miti Ila kusema kweli Mawaziri wa Mazingira hawajawai kuanzisha kampeni ya Kitaifa kubwa inayohusu upandaji miti yenye lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na misitu mingi, mapori mengi ivyo kuwa salama dhidi ya majanga ya ukame.

Kwa Waziri wa Sasa wa Mazingira Suleiman Jaffo huyu ndo naona ameshindwa kabisa kazi yake maana hata suala la mifuko ya plastiki naona linaanza kurejea kwa kasi sana. Ukitembea kwa basi kutoka Dar kuelekea mikoani hali unayoikuta barabarani inasikitisha. Kuna mifuko mingi ya plastic na materials nyingine za plastiki zimetupwa kando ya Barabara hadi unafikia kujiuliza Kama kucontrol plastiki au usafi tu inatushinda kwa nini tuwe wa Waziri wa Mazingira au Wakuu wa Mikoa na Wilaya?

Nilikuwa Mkoani Dodoma siku si nyingi nikaona hadi Kuna vibanda vya chips vimeanza kuwafungia wateja wake chips kwenye mifuko ya plastiki. Waziri Jafo lawama zangu haziwezi kukuacha kwenye hili maana unamuangusha Mama Samia. Kama huwezi kazi sema.

Hatari ninayoiona mbeleni

1. Sasa tumeanza ona baadhi ya sehemu zinapata mgao wa maji na umeme kutokana na ukame unaosababishwa na maamuzi mabovu pamoja na usimamizi mbovu ubaofanywa na watu walioaminiwa na kupewa madaraka. Hali ikienda hivi ninaona nchi ya Tanzania ikishindwa kuzalisha umeme wa kutosha na baadae chakula cha kutosha.

Tukishindwa kuzalisha umeme wa kutosha kutokana na ukame Mradi wa Bwawa la Nyerere utaonekana rasmi kuwa mradi ulioliingizia Taifa hasara kutokana na kushindwa kuzalisha umeme uliotarajiwa pamoja na kujengwa kwa gharama kubwa.

2. Naona baadae Taifa litakuwa tegemezi na gharama za maisha kuongezeka maradufu jambo linaloweza kuleta hatari kwa kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kutokana na nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye nishati na chakula!

Tuchukue hatua sasa
Idea yako ni ngumu sana kuielewa.

Mara mnatuambia maji yamefunguliwa mara sijui kimetokea nini.

Nyie watu bana mtamaliza sababu zote ila mwisho we mtasema tu ukweli . Nchi ishawashinda hii. Watu hawaendi kazini wanafanyia kazi nyumbani na offisini tu.

Hakuna hata siku moja rais ameenda ziara kuko mapolini, yeye anapiga ziara za kupangiwa tu. Mtanzania bila kusimamiwa hafanyi kazi.
 
Kwenye maji wanatumia teknolojia inaitwa desalination. Ni teknolojia ya kusafisha maji chumvi hasa ya Bahari Kwa matumizi ya kunywa. Hii inatumika Israël, Saudia, Qatar, Kuwait na Dubai.

Ni teknolojia aghali sana inayohitaji fedha nyingi sana. Swali ni Je sisi tutaiweza na hali yetu ya kiuchumi?
Sisi hatuitaji hiyo technology kutibu maji Chumv tuna mito karibu kila mkoa yenye maji ya kutosha mwaka mzima

Tuna maziwa, mvua tuna Pata karibu kila mkoa shida hapa ni mifumo mibovu tulio nayo juu ya maji na hili Lina kera Sana
 
Bibi ushungi yeye na ndege
 
Wasomi na watawala wanatuangusha, ukweli mchungu matumizi mkaa na kuni hayaepukiki, misitu mingi hifadhi imebaki vichaka,
Mzaha na utani upandaji miti siku ya mazingira Ni usanii
1. TSF ufugaji sio dhambi serikali igawe vitalu kwa shariti wafugaji walinde miti kwa ada nafuu
2. Ubunifu miti mbao na kuni muda mfupi serikali ifanye PPP na sector binafsi Ni biashara na fursa kubwa kuongeza uchumi wetu tutapata Faida endelevu nature na mahitaji badala ya vichaka.
3. 70% ya Tz Ni vijiji Wana maeneo ya kutosha iwekwe plan na sheria , Aina miti rahisi kuni ya Muda mfupi kila Kaya idadi fulani kuzunguka nyumba na mashamba, Kama wakazi Kilimanjaro, utamaduni uzio wa miti.
 
Kwenye maji wanatumia teknolojia inaitwa desalination. Ni teknolojia ya kusafisha maji chumvi hasa ya Bahari Kwa matumizi ya kunywa. Hii inatumika Israël, Saudia, Qatar, Kuwait na Dubai.

Ni teknolojia aghali sana inayohitaji fedha nyingi sana. Swali ni Je sisi tutaiweza na hali yetu ya kiuchumi?
Hakuna gharama yeyote mimi haya ndio mambo yangu, chimba kisima chako mimi nakuletea kimashine cha kutoa hizo chumvi hapo hapo nyumbani kwako.
 
Kuna nchi nyingi za Waarabu jangwani hazina mapori, misitu wala mito ila zina maji tele ya kutosha

Waarabu wanajaribu sana kuligeuza jangwa kwa kupanda miti.

Israel wanageuza jangwa na kupanda miti. Walichukua udongo kutoka Orange Free state , Afrika kusini na kupeleka jangwani na walianza kupanda machungwa na hivi sasa wanasafirisha.

Oman . Saudi Arabia hivi sasa wanalima ngano kwa wingi

Nchi za Ulaya hasa Scandinavia ukikata mti mmoja hyupanda 100 kwani misitu ni mali ya watu , private na ni mali sana.

Wenye misitu ni matajiri sana
 
Kuna muda ni lazima ukweli usemwe maana usiposemwa lazima kumbukumbu zitakuwa za upotoshaji Mkubwa

Kwenye Tatizo linaloikumba Tanzania la ukame na ukosefu wa Maji kwa sasa lawama zangu zote nazipeleka kwa watu wafuatao

1. William Lukuvi
Akiwa Waziri wa Ardhi kuanzia Awamu ya Tano, nchi yetu imeshuhudia urasimishaji mkubwa sana wa Mapori ya akiba pamoja na hifadhi kuwa makazi ya watu!

Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana uharibifu wa Mazingira hasa ukataji Miti wa kutisha kwenye mapori mengi yaliyokuwa yanategemewa kuleta mvua uliofanywa na Jamii za wafugaji na wakulima hasa kwenye mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora, Morogoro, Pwani na kusini mwa Tanzania.

Mfano wa hili nimejionea kwenye Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora inayoongoza kwa kuwa na Misitu mingi.

Kwenye mikoa hii kumekuwa na uvamizi sana wa maeneo yenye mapori na misitu ya asili unaofanywa na Jamii za watu wa mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Watu hawa wamekuwa wakikata miti kwenye mapori kwa Kiwango cha kutisha na hata sasa takwimu zimeanza kuonesha hivi karibuni mito iliyokuwa ikititirisha maji mwaka mzima kwenye mikoa ya Kigoma na Katavi bila kusahau Rukwa imeanza kukauka kutokana na shughuli hizi za binadamu.

Waziri Lukuvi akiwa waziri wa Ardhi badala ya kushauri Serikali watu hawa waondolewe kwenye maeneo haya na kurudishwa kwenye maeneo yao ya asili yeye amezidi kushauri serikali watu hawa kurasinishwa kwenye maeneo hayo. Hivyo tusilaumu mtu. Tatizo ni Lukuvi

2. Mawaziri wa Mazingira kuanzia Awamu ya 3,4,5 na huyu wa Awamu ya 6

Hii ni Kwa sababu Nchi yetu imekuwa na Mawaziri wa Mazingira kwenye Awamu zote. Ila kamwe nchi hii haijawai kuwa na kampeni kubwa ya upandaji Miti.

Kila siku watu wamekuwa wakisema juu ya ukame na ukataji mkubwa wa Miti Ila kusema kweli Mawaziri wa Mazingira hawajawai kuanzisha kampeni ya Kitaifa kubwa inayohusu upandaji miti yenye lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na misitu mingi, mapori mengi ivyo kuwa salama dhidi ya majanga ya ukame.

Kwa Waziri wa Sasa wa Mazingira Suleiman Jaffo huyu ndo naona ameshindwa kabisa kazi yake maana hata suala la mifuko ya plastiki naona linaanza kurejea kwa kasi sana. Ukitembea kwa basi kutoka Dar kuelekea mikoani hali unayoikuta barabarani inasikitisha. Kuna mifuko mingi ya plastic na materials nyingine za plastiki zimetupwa kando ya Barabara hadi unafikia kujiuliza Kama kucontrol plastiki au usafi tu inatushinda kwa nini tuwe wa Waziri wa Mazingira au Wakuu wa Mikoa na Wilaya?

Nilikuwa Mkoani Dodoma siku si nyingi nikaona hadi Kuna vibanda vya chips vimeanza kuwafungia wateja wake chips kwenye mifuko ya plastiki. Waziri Jafo lawama zangu haziwezi kukuacha kwenye hili maana unamuangusha Mama Samia. Kama huwezi kazi sema.

Hatari ninayoiona mbeleni

1. Sasa tumeanza ona baadhi ya sehemu zinapata mgao wa maji na umeme kutokana na ukame unaosababishwa na maamuzi mabovu pamoja na usimamizi mbovu ubaofanywa na watu walioaminiwa na kupewa madaraka. Hali ikienda hivi ninaona nchi ya Tanzania ikishindwa kuzalisha umeme wa kutosha na baadae chakula cha kutosha.

Tukishindwa kuzalisha umeme wa kutosha kutokana na ukame Mradi wa Bwawa la Nyerere utaonekana rasmi kuwa mradi ulioliingizia Taifa hasara kutokana na kushindwa kuzalisha umeme uliotarajiwa pamoja na kujengwa kwa gharama kubwa.

2. Naona baadae Taifa litakuwa tegemezi na gharama za maisha kuongezeka maradufu jambo linaloweza kuleta hatari kwa kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kutokana na nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye nishati na chakula!

Tuchukue hatua sasa

Huyu Lukuvi hafai kabisa kuwa hata mjumbe wa Nyumba 10, hana busara hata kidogo katika uongozi. Ni mtu wa mihemko tu na hamasa nyingi za kichama na udini mwingi

Ataliangamiza taifa aondoshwe haraka
 
Sisi hatuitaji hiyo technology kutibu maji Chumv tuna mito karibu kila mkoa yenye maji ya kutosha mwaka mzima

Tuna maziwa, mvua tuna Pata karibu kila mkoa shida hapa ni mifumo mibovu tulio nayo juu ya maji na hili Lina kera Sana
Taja iyo mito iliyopo kila sehemu inayotiririsha maji mwaka mzima?
 
Waarabu wanajaribu sana kuligeuza jangwa kwa kupanda miti.

Israel wanageuza jangwa na kupanda miti. Walichukua udongo kutoka Orange Free state , Afrika kusini na kupeleka jangwani na walianza kupanda machungwa na hivi sasa wanasafirisha.

Oman . Saudi Arabia hivi sasa wanalima ngano kwa wingi

Nchi za Ulaya hasa Scandinavia ukikata mti mmoja hyupanda 100 kwani misitu ni mali ya watu , private na ni mali sana.

Wenye misitu ni matajiri sana
Wanaongea tu hawa hawajui uhalisia
 
Back
Top Bottom