Tatizo la maji nchini mwisho 2025, Rais Samia anatekeleza

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema anatambua matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji nchini linakuwa limekwisha.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi, Agosti 6, 2022 wakati akizindua mradi wa maji katika kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya wenye thamani ya Sh2.5 bilioni utakaozalisha maji lita Milioni mbili kwa siku.

Amesema katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo 2025 ilielekeza kutatua tatizo la maji na kwa Mkoa wa Mbeya kuna miradi 50 ambayo imefikia asilimia 95 na ifikapo 2025 tatizo la maji litakwisha kwa asilimia 100.

''Wito wangu, sipendi kusikia wananchi wanapata maji wakati Rais amefika lakini akiondoka huduma za maji hakuna, Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji,” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athon Sanga amesema mradi huo umefikia asilimia 70 ambao utazalisha lita milioni mbili zitakazo ondoa tatizo la maji katika Wilaya ua Chunya.

Amesema wizara ina mpango wa kuchimba visima vikubwa vya maji katika mji wa Makongorosi ili kuondokana na hadha kwa baadhi ya maeneo huku akimpongeza Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka kwa kutatua changamoto ya maji jimboni kwake kwa kuchimba visima.

Kwa upande wake, Mbunge Kasaka amemuomba Rais Samia kusaidia kuboreshwa miundombinu ya barabara kutoka chunya mpaka kijiji cha Itumbi ambako kuna shughuli za uchimbaji wa madini ili kufungua fursa za kiuchumi.

''Rais Wilaya ya Chunya inategemea zaidi shughuli za uchimbaji madini ambazo zinachochea uchumi tunaomba ikikupendeza miundombinu ya barabara iboreshwe li kuongeza kasi ya shughuli ya uchimbaji wa madini na kuongezeka kutoka kilo 250 mpaka 400 kwa mwezi,''amesema.
 
Moja ya kipaombele Kikuu cha Mh.Rais ni kumtua mama ndio na anamtua kweli kweli..

Pili elimu kwa watoto wa kike na anawajengea mashule kweli kweli.

Barabara Vijijini na eongeza mapesa kama yote..

Na ajira hasa Kwa vijana ,ameamua waende kwenye ajira za kilimo chenye tija na anafanya kweli kweli..

Kwa mtizamo wangu,Rais Samia ndio Rais atakayeleta mageuzi ya maana kwenye hii Nchi..

Imagine ajenda 1030 ya kilimo na ajenda 2025 ya Watalii mil.5.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema anatambua matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji nchini linakuwa limekwisha.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi, Agosti 6, 2022 wakati akizindua mradi wa maji katika kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya wenye thamani ya Sh2.5 bilioni utakaozalisha maji lita Milioni mbili kwa siku.

Amesema katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo 2025 ilielekeza kutatua tatizo la maji na kwa Mkoa wa Mbeya kuna miradi 50 ambayo imefikia asilimia 95 na ifikapo 2025 tatizo la maji litakwisha kwa asilimia 100.

''Wito wangu, sipendi kusikia wananchi wanapata maji wakati Rais amefika lakini akiondoka huduma za maji hakuna, Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji,” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athon Sanga amesema mradi huo umefikia asilimia 70 ambao utazalisha lita milioni mbili zitakazo ondoa tatizo la maji katika Wilaya ua Chunya.

Amesema wizara ina mpango wa kuchimba visima vikubwa vya maji katika mji wa Makongorosi ili kuondokana na hadha kwa baadhi ya maeneo huku akimpongeza Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka kwa kutatua changamoto ya maji jimboni kwake kwa kuchimba visima.

Kwa upande wake, Mbunge Kasaka amemuomba Rais Samia kusaidia kuboreshwa miundombinu ya barabara kutoka chunya mpaka kijiji cha Itumbi ambako kuna shughuli za uchimbaji wa madini ili kufungua fursa za kiuchumi.

''Rais Wilaya ya Chunya inategemea zaidi shughuli za uchimbaji madini ambazo zinachochea uchumi tunaomba ikikupendeza miundombinu ya barabara iboreshwe li kuongeza kasi ya shughuli ya uchimbaji wa madini na kuongezeka kutoka kilo 250 mpaka 400 kwa mwezi,''amesema.
Hakuna kitu Kama hicho may be itolowe amri kwamba kila halmashauri nchini pitia makusanyo yake ya ndani KILA kwenye shida ya maji vichimbwe visima na wawepo wakadarasi angalau 10 wanaoaminika kuifanya KAZI hii, 20m unaweza chimba kisima mpaka meter miambili, na watu wakapata maji, ila serikali hii na KWa watendaji wake utaambiwa kisima kimoja, lot of money
 
Kila uchwao nyie chawa wa Samia kazi yenu kuu ni kusifia tu hata vitu impossible anashindwa vitu vidogo Kama mfumuko wa bei suala la maji ndo ataweza?
 
Moja ya kosa ambalo sitaki kulifanya kwenye maisha yangu ni kumuamini mwanasiasa
 
Back
Top Bottom