Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Unaishi wapi mkuu?

Kama uko Dar nenda Ekenywa Hospital, ni Mwembe Chai Magomeni kama unaenda kwa Marehem Shekhe Yahya, gorofa la kwanza mkono wa kulia ukikatisha barabara ya lami pembeni ya kituo cha mafuta cha SuperStar.

Hapo wamejaa specialists wa sikio, koo na pua. Wakishindwa hao rudi kwa akina Mzizi mkavu.
 
Last edited by a moderator:
habari ,

Nna matatizo na sikio langu la kushoto tangu nipo mdg, niipima n kupewa "hearing aid" bt nkashndwa kuitumia kwa mda mrefu maana nilkua naskia saut kuubwaa ad kichwa kinauma,,, so nkaamua kuvaa darasan af nikitoka navua.

Tatizo langu ss lmezd kdg,yan sikio la kulia pia lnauma istoshe nackia saut za ""zyiiiiiiiiiiiiii"" , nijuavo mimi ,hii hali ya kupata hii saut maskion huitwa TITTUNIS .Mnisadie ni vip naeza kupona hii hali n pia ka kuna uwezekano wa kupata matibabu ili nipone n kuweza kusikia vzr kama wenzangu.
Kabla ya kukupa dawa za Tibambadala ilikuwa kwanza uende hospitali wakakuangalie vizuri kisha uje hapa utupe feedbak pole sana kwa hayo matatizo yako.

Sikio (Ear) limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.

Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:


Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga na watoto wadogo.


Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na hutokea zaidi wakati wa baridi.


Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media:

Kuumwa na kuchomwa kwa sikio
Kutokwa na uchafu ndani ya sikio
Kutosikia kwa ghafla
Homa

Sababu za Otitis media:
Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube)
kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.

Sababu za Otitis externa:
Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.

Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili.
 
Wadau kwa mwenye ufahahamu juu ya tatizo hil kwan sikio linawasha af linatoa usaha.
 
Hiyo ni fungus, nenda kwa OTC ukasafishwe na kupewa dawa( OTC ni mtaalam wa magonjwa ya sikio, koo na mfumo wa pua!!!!!
 
Sikio linapotoa usaha wakati mwingine ngoma ya sikio inakuwa imetoboka.Na kama tobo linakuwa kubwa,matibabu sahihi ni operation.Ushauri mzuri ni kwenda kwa daktari akuangalie ndani ili kujua usalama wa ngoma ya sikio.Tena ikiwezekana nenda hata kesho.
 
Mara nyingi hili tatizo hutokea mtoto Akiwa mdogo kuingiwa na maji sikioni, husababisha ngoma kupasuka na kuanza kutoa usaha. Tiba halisi ni operation, Nairobi wanafanya na South Africa, SA n cheap ukilinganisha na Nairobi, tatizo n kwamba ukifanyiwa hutakiwi kupanda ndege ama bus kwa mwezi mmoja ili ngoma ikauke na kupona vizuri. Nilifanyiwa 2012 na nimepona kabisa.

lakin waone doctors kwanza kwa ushauri wa kitabibu.


pole Sana
 
Wadau kwa mwenye ufahahamu juu ya tatizo hil kwan sikio linawasha af linatoa usaha.

Mkuu, pole sana. tafuta bhangi, iponde then kamulia matone yake matatu tu, lakini kila tone lipishane dk 5
 
Jaman mi nina mtoto wa miaka 2, akiwa na miezi mitatu alipata infection ya masikio hadi kufikia kunuka na kutoa usaa kwenye. Tukaangaike hospitali nyingi ikiwa ni pamoja na muhimbili na ikenywa pale mwembe chai, lakin baada ya miangaiko na misukosuko yote mtoto akapona ile infection ikapotea kabisa, bt tatizo ni kwamba ile hali imeanza kurudi tena sikio linatoa harufu kama zamani, naomba ushauri wandugu ni wapi naweza kupata matibabu.
 
Pole kwa kuuguza, nakushauri umuone daktari bingwa . Pale ekenywa kuna madaktari wa level tofauti ila kuna super specialist anaitwa Dr Emmanuel ni mzuri sana mimi alimtibiaga mtoto wangu akapona kabisa.
 
Pole kwa kuuguza, nakushauri umuone daktari bingwa . Pale ekenywa kuna madaktari wa level tofauti ila kuna super specialist anaitwa Dr Emmanuel ni mzuri sana mimi alimtibiaga mtoto wangu akapona kabisa.

Naomba kujua gharama kwasababu mtoto wangu anatatizo kama hilo.Ntashukuru sana.
 
Pole kwa kuuguza, nakushauri umuone daktari bingwa . Pale ekenywa kuna madaktari wa level tofauti ila kuna super specialist anaitwa Dr Emmanuel ni mzuri sana mimi alimtibiaga mtoto wangu akapona kabisa.

Naomba kujua gharama,mwanangu anatatizo kama hilo.


Pole kwa kuuguza, nakushauri umuone daktari bingwa . Pale ekenywa kuna madaktari wa level tofauti ila kuna super specialist anaitwa Dr Emmanuel ni mzuri sana mimi alimtibiaga mtoto wangu akapona kabisa.
 
Habari wanaJF

Tareh 27 june, lilianza tatizo la sikio moja la kulia kutosikia vizuri na kuwa kama linatoa mlio hivi, hali ambayo ilipelekea kizunguzungu kunipata, baadae kusikia kichefuchefu na kutapika.

Nlipokwenda kwa doctor wa mtaani kwetu (anafanya kazi hospitali ya jirani) nlichomwa sindano na kunipa dawa, ambazo nlitumia na kujisikia vizuri tu.

Ila tar. 30 June, hali ile ilinirudia na nilipokwenda hospital nikapimwa nikalazwa kabisa kwamba nina malaria kali, nilitundikiwa drips 3 za quinine, na kesho yake niliruhusiwa (hii ilikuwa mara ya kwanza kulazwa na kuumwa malaria, sijawahi toka nizaliwe na am 22 yrs).

Baada ya kutumia dawa nlianza kujisikia vizuri,malaria nlipona lakini tatizo la kizunguzungu na hili la sikio halikomi, nilitapika kama mara mbili baada ya kutoka hospital, tar. 15 July, nikaenda kupima nicheki kama tatizo ni damu nyingi au imepungua nikaambiwa damu ipo sawa tu.

Kuanzia pale, hilo tatizo bado linajirudia, mara moja au mbili kwa wiki, Ila toka ulipoanza mwezi huu, lilikuwa halijanitokea ila juz nikaanza kusikia kichwa kinauma nilipoenda kupima nimeambiwa nina malaria naumwa, nimepewa dawa natumia, ila jana jioni sikio likaanza kuuma, kizunguzungu na nikatapika sana.

Je, hii hali tatizo laweza kuwa nin?, Malaria inaweza ikawa inaingiliana na masuala ya sikio kuuma na kizunguzungu?

Mbona hata baad ya kutibiwa malaria nikapona sikio, kizunguzungu na kutapika viliendelea kunisumbua?

Karibuni kwa mchango wenu ndugu.
 
pole mkuu..hio shida yako inabid umuone daktari bingwa wa magonjwa ya pua,sikio na koo (ENT Surgeon). unaweza kuwa na Vestibular Disease ila kwa kuanzia tumia Meclizine 50mg mara 2 kwa cku (tafuta dawa inaitwa vomidoxine ina hio meclizine). ila fanya mchakato uwaone hao mdaktari hapo juu
 
Back
Top Bottom