Habari wanaJF
Tareh 27 june, lilianza tatizo la sikio moja la kulia kutosikia vizuri na kuwa kama linatoa mlio hivi, hali ambayo ilipelekea kizunguzungu kunipata, baadae kusikia kichefuchefu na kutapika.
Nlipokwenda kwa doctor wa mtaani kwetu (anafanya kazi hospitali ya jirani) nlichomwa sindano na kunipa dawa, ambazo nlitumia na kujisikia vizuri tu.
Ila tar. 30 June, hali ile ilinirudia na nilipokwenda hospital nikapimwa nikalazwa kabisa kwamba nina malaria kali, nilitundikiwa drips 3 za quinine, na kesho yake niliruhusiwa (hii ilikuwa mara ya kwanza kulazwa na kuumwa malaria, sijawahi toka nizaliwe na am 22 yrs).
Baada ya kutumia dawa nlianza kujisikia vizuri,malaria nlipona lakini tatizo la kizunguzungu na hili la sikio halikomi, nilitapika kama mara mbili baada ya kutoka hospital, tar. 15 July, nikaenda kupima nicheki kama tatizo ni damu nyingi au imepungua nikaambiwa damu ipo sawa tu.
Kuanzia pale, hilo tatizo bado linajirudia, mara moja au mbili kwa wiki, Ila toka ulipoanza mwezi huu, lilikuwa halijanitokea ila juz nikaanza kusikia kichwa kinauma nilipoenda kupima nimeambiwa nina malaria naumwa, nimepewa dawa natumia, ila jana jioni sikio likaanza kuuma, kizunguzungu na nikatapika sana.
Je, hii hali tatizo laweza kuwa nin?, Malaria inaweza ikawa inaingiliana na masuala ya sikio kuuma na kizunguzungu?
Mbona hata baad ya kutibiwa malaria nikapona sikio, kizunguzungu na kutapika viliendelea kunisumbua?
Karibuni kwa mchango wenu ndugu.