Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Habari wakuu...
Naamini Mungu bado anatupenda na kutupa uzima ndo maana tunakutana hapa

Samahan naomba kuuliza hii hali ya kusikia kelele nyingi masikioni( kama mashine ya kusaga mahindi) n hali ambayo natakiwa kuikubali na kuishi nayo?

Hali hii ilianza mwaka juzi(2016) na nmetumia dawa nyingi lakin sion mafanikio
Kuna wakat nashindwa hata kufanya kazi kwa sababu ya usikivu kuwa mdogo kwa sababu ya kelele hizi
Hivi naandika uzi huu ikiwa ni siku chache tangu niache kibarua changu kwa sababu ya shida Hii

Najaribu kufikir kama swala hili n halipon( kama wengi wasemavyo) bas nitaishi maisha ya namna gan
Najikuta nakata hata tamaa ya kuishi

Naomben mtazamo wenu ndugu zangu kama kuna mtu anaijua hii shida au alishawahi kukutana nayo na aliipona vipi

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
Muhimu kufika hospital kwanza inaweza kua n mattzo ktk masikio tu.
 
Mkuu miriam 111 jaribu dawa za kienyeji pia zinasaidia . Landa unasumbuliwa na mzio.

Na pia yawezekana ni kuchafuka kwa damu yake, yaani kuna element imeingia katika damu yake ambapo dalili zake ni hiyo ear buzzing, kwa hiyo pia aangalie masuala ya damu yake kwa ujumla.
 
anza maombi na nivizuri ukaanza kwa kujifungua mwenyewe kwanza hiyo hali itapona kwa imani kwa kuwa MUNGU wetu hakuna analoshindwa.
Matatizo ya kiafya hasa yanayohusianisha maswala ya afya ya akili na ufahamu, hutibiwa kama magonjwa mengine!

Haipaswi jufungamanishwa na demon possession!...huu ni mtazamo wa zama za kale kabisa ambapo magonjwa haya yanayofungamanishwa na matatzo ya kisaikolojia yalikuwa yanatibiwa kwa mtu kupasuliwa kichwa ili kumtoa shetani ambaye "anampigia kelele/kumsumbua" mgonjwa (Exrcisism)

miriam 111 dadangu, waone madaktari bingwa wa afya ya akili na saikolojia utapona!
 
Jamani asanten sana kwa vile mnaonesha kunijali na kunitia moyo katika hili nnalopitia! Natambua mchango wenu na nauheshimu pia
Mungu wangu azidi pia kuwafanikisha katika njia zenu
 
Jamani asanten sana kwa vile mnaonesha kunijali na kunitia moyo katika hili nnalopitia! Natambua mchango wenu na nauheshimu pia
Mungu wangu azidi pia kuwafanikisha katika njia zenu

Nawe, hasa Mungu akusaidie na akupe ponyo lisilobakisha kasoro, hakika mponyaji ni Mungu pekee na Daktari ni katika njia yake ya uponyaji, Amin yaa rabb alamiin.
 
aretasludovick, Mkuu wewe ni Hatari sana unajaribu vitu vipo nje ya uwezo wako?lakini ninakupa hongera sana ulipofikia ukiendelea unaweza kufunguka jicho la 3 aka Thrid Eye. Lakini muone Mkuu Rakims azidi kukusaidia zaidi ili uweze kufunguka hilo jicho la 3 aka Third Eye.

Can tinnitus go away?
They hope that the ringing will disappear. While tinnitus caused by a medication or other temporary situation may cease if that element is removed, the reality is that tinnitus does not just “go away” for most people
 
Wakuu Nina tatizo la sikio langu linauma kwa ndani... kuna kama kipele hivi yaani... nimevumilia nimeshindwa.. je tiba yake ni nini??.... ntashukuru nikipata majibu hapa...
 
Wakuu Nina tatizo la sikio langu linauma kwa ndani... kuna kama kipele hivi yaani... nimevumilia nimeshindwa.. je tiba yake ni nini??.... ntashukuru nikipata majibu hapa...
Nenda hospitali kaonane na bingwa wa Pua Koo na masikio..
Hivyo viunvo Ni very delicate havipaswi kuchezewa chezewa mkuu.
USIINGIZE CHOCHOTE NDANI YA SIKIO IWE KIJITI, MAFUTA, MAJI AU DAWA YOYOTE KABLA HUJAONANA NA BINGWA WA MATATIZO YA MASIKIO
 
Wakuu Nina tatizo la sikio langu linauma kwa ndani... kuna kama kipele hivi yaani... nimevumilia nimeshindwa.. je tiba yake ni nini??.... ntashukuru nikipata majibu hapa...

Aisee Bro; Ulikuwa unavumilia hadi iweje? Nakushauri zingatia yaliyosemwa hapo juu Na. 4
 
Suluhu ni kwenda kumuona daktari tu kwani ndio atakayejua ni dawa gani inafaa kwa hali ya sikio lako ukitaka dawa huku utakuwa unabahatisha tu.
 
Pole sana. Nilikuwa na tatizo ili nilienda hospital iliyoko maeneo ya Mwembe chai inaitwa EKENYWA wanadeal na masikio,pua na kinywa akika hawa jamaa wapo vzr sana niliponea hapo hapo baada ya kunifanyia tiba. Nakushauri umuone daktari.
 
Nenda hospitali kaonane na bingwa wa Pua Koo na masikio..
Hivyo viunvo Ni very delicate havipaswi kuchezewa chezewa mkuu.
USIINGIZE CHOCHOTE NDANI YA SIKIO IWE KIJITI, MAFUTA, MAJI AU DAWA YOYOTE KABLA HUJAONANA NA BINGWA WA MATATIZO YA MASIKIO
sawa sawa mkuu Asante Sana
 
Back
Top Bottom