Nimekua nikisumbuliwa na hili tatizo kwa zaidi ya mwaka wa 10 nikilichukulia poa tu. masikio yangu sigusishi maji kabisa, ikitokea kwa bahati mbaya hasa kwenye wakati wa kuoga maji ya kugusagusa kwa ndani basi kinachofata hapo ni maumivu kwa siku nzima japo kua hua simakubwa. Je hili nikawaida au ni tatizo? Kwa kifupi naishi mbali na maji karibu na sikio.
Na pia sewezi eka headset and headphone kwenye sikio langu kwani dakika moja tu itanitosheleza kuleta maumivu ya masikio kwa masaa na muda mwengine yakiambatana na maumivu ya kichwa. Ila kila nikitizama wenzangu wanajifanyia vizuri tu. Hata simu nikizungumza kwa muda mrefu kiodogo tu au simu ikiawa na sauti kubwa basi matokezeo ndio hayo hayo.
Je, hii ni hali ya kawaida au ni ugonjwa? na kama ugonjwa naomba msaada wakuu.