Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Nakubaliana na wazo ka kucheck uzima wa ngoma kwanza. Kama hajaathirika basi tafuta bangi mbichi uweke matone mawili hivi basi mchezo utakuwa umekwisha.
 
Samahani kwa kudandia hoja. Ila nami nina tatizo hlo hlo la sikio huu mwaka wa 20 sasa
1.ni la kushoto.
2.linatoa usaha hasa sehemu za baridi na kama kuna mawingu mazito
3.likiingia upepo tu,silali
nb.nimetumia dawa nyingi mfano mafuta ya kuku,simba,mbuni na punda.Pia nimetumia dawa za hospitalini na za kienyeji lakini wapi.Mfano nimetumia hizi wazouza maduka ya dawa mfano Boric Acid.Msaada tafadhali
 
Wakuu!

Mwenzenu nasumbuliwa na tatizo(ugonjwa) wa masikio kutoa usaha, tangu nikiwa mtoto mdogo kabla hata sijapata ufahamu sikio langu moja hutoa usaha.

Tatizo hili nimeishi nalo kwa kwa muda mrefu mpaka hivi sasa nina 20's bado tu linanisumbua...... nimetumia dawa kibao za hospitali na mitishamba lakini wapi mpaka hivi sasa nimechoka kiasi kwamba wakati mwingine nawaza aliyeniloga ashakufa...........hatua niliyofikia naona kawaida tu na nishakata tamaa ya kupona .....kwa ujumla huwa linanikosesha uhuru sana kwani muda wote popote nilipo lazima niwe kimachalemachale na pamba zangu na vijiti ili kudhibiti huo uchafu......

MWENYE KUIFAHAMU TIBA YAKE YA UHAKIKA TAFADHALI!
CC. MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Kama hujafanya kipimo cha culture and sensitivity test (C/S) ya huo usaha , usikate tamaa. Nenda mhimbili na umuone ENT surgeon au pathologist kwa ajili ya evaluation and treatment. Utapona. Dawa za kienyeji si muafaka kwa tatizo lako. Pole sana.
 
Mkuu si ungem-mp tu MziziMkavu?
Anyway,kama hutajali hebu jaribu kuwaconsult maspecialists wa mambo hayo.Siamini kabisa kwamba umetumia matibabu/dawa zote za hospitali zimeshindikana.Watu wengi wamekuwa na mazoea ya kununua dawa kwenye vibanda vya kuuzia dawa na wasipopona wanasema wametumia dawa zote za hopitali imeshindikana.

Mind you,hizo pamba za masikioni(hata kama zinauzwa),sio salama kwa afya ya masikio.Zimekuwa ni chanzo kikubwa cha maambukizi ya vijidudu masikioni,usiziamini sana ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI: Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.

TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Kanuni ya kwanza: Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio
lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.

Kanuni ya pili: Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.. Kanuni ya tatu: Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili. Kanuni ya nne: Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.


Na pia nenda hospital kitengo cha ENT hapo Muhimbili kawatafute Ma-Daktari mabingwa hawa mmoja wapo Dr Edwin, Dr Kimario au Prof. Mushi Wataweza kukusaidia hayo Matatizo yako Pole sana.@mpalu
 
Mastoiditis\unahitaji mastoidectomy anyway recurrence iko kwene high chance ,anza na tiba mbadala kama alivyoshauri MZIZI halafu waone wataalamu wa ENT,CT-scan inaweza kuombwa
 
Sikio langu lina uvimbe kwa ndan, sio mkubwa sana ila ni wawastani. Naomben mnisaidie, nnunue dawa gan ili niweze kupona. vilevle uvimbe huo husababishwa na nn? {kiutaalamu}
 
The same last week, nilipewa hosp. gentamicin Eye/Ear drop na antibiotic tablets, nimeshapona.
 
Back
Top Bottom