Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Mtoto wangu ana tatizo la kutokwa na uchafu mithili ya usaha sikion na unakuwa na harufu mbaya.
Na kuna mda huwa analia akilalamika maumivu.

Wana jf, nijuzeni tatizo ni nini na wapi naweza pata tiba nzuri ya tatizo la mwanangu.

Nawasilisha
 
Mwone Dr Ole Lengine, wa Ekenywa hospital Magomeni. Ni ENT specialist (Dr Bingwa)
 
Mkuu pole sana.Chukua tone la mkojo udondoshee sikioni kwa ndani.Kisha tone lingine upake sikio lote kwa nje.Tupe ushhda
 
Magomeni Mikumi, unaingilia pale kwa Sheikh Yahaya unanyosha kama mita 300 hivi utaona kibao cha hospital hiyo
 
Magomeni Mikumi, unaingilia pale kwa Sheikh Yahaya unanyosha kama mita 300 hivi utaona kibao cha hospital hiyo
Mkuu embu funguka make huwa nakusoma ukipiga promo.
Hiyo hospital ni maalum kw masikio tu, au wanatibu na magonjwa mengine!
 
Mtoto wangu ana tatizo la kutokwa na uchafu mithili ya usaha sikion na unakuwa na harufu mbaya.Na kuna mda huwa analia akilalamika maumivu.Wana jf, nijuzeni tatizo ni nini na wapi naweza pata tiba nzuri ya tatizo la mwanangu.Nawasilisha
Jambo la kwanza ni kuwa usizibe sikio na pamba.Jambo la pia ni kufanya ear mopping au kulipiga deki sikio nayo ni kuhakikisha unalisafaisha na pamba safi kila baada ya muda ili liwe kavu.Unaweza kutumia dawa inayoitwa boric acid ear drops lakini kama unakaa Dar muone ENT specialist atakusaidia.Fanya hivyo kwa wiki moja na nijulishe matokeo.Pole sana.
 
Ear,Noose and Throat (ENT) specialist.Daktari bingwa wa Sikio,Pua na Koo
 
Nashukuru sana wadau kwa concern yenu. Nilipewa dawa ya kudondoshea sikioni. Naona maendeleo si mabaya. Natumia kwa siku tano.
 
Msaada wadau kwa anayejua matibabu ya sikio,mtoto wangu ana tatizo la kutoka usaha kwenye sikio lake moja yapata mwezi sasa nimehangaika mpaka ENT CCBRT nilichoambulia leo ni muendelezo wa utitiri wa madawa,kama kuna mwenye kujua dawa jamani anijuze ili mtoto wangu apate tiba.
 
Mkuu Mchaka Mchaka hayo mafuta ya kuku nitayapata wapi na yanatumikaje (dose)!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchaka Mchaka hayo mafuta ya kuku nitayapata wapi na yanatumikaje (dose)!
Ukipika kuku (hasa aliyenona) maji yakikauka yatabaki mafuta, usiweke mafuta mengine sijui Korie nk, mpike kuku pekee mwishoni atatoa mafuta. Mimina hayo mafuta kwenye chombo kisafi. Kila asubuhi na jioni yapashe kidogo (kwa kuwa yakikaa muda mrefu yanaganda),mwekee mtoto matone kadhaa 2-3.
 
Back
Top Bottom