Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Naomba kujua haya matatizo ya kua na ganzi kwenye mikono nini sababu zake na nini dawa yake maana ilianza mkono wa kulia alafu ukawa mkono wakushoto na wakulia ukawa umepona.
 
google scalenius muscle syndrome, unafanya kazi gani kwani.?Nimewahi kuwa na tatizo kama hilo nilipokuwa jeshini.
 
Naomba kujua haya matatizo ya kua na ganzi kwenye mikono nini sababu zake na nini dawa yake maana ilianza mkono wa kulia alafu ukawa mkono wakushoto na wakulia ukawa umepona.
Hujatuambia wewe ni Mwanamke au Mwanaume? Una miaka mingapi? Hayo matatizo yako yanakutokea wakati gani? unapo amka au wakati gani? Mwili Kufa Ganzi haswa Sehemu za mikono na Miguu Ni moja katika

sababu zinazoweza kuhatarisha kiungo cha mwili ni mfumo wa kufanya ganzi katika kiungo kwa muda mrefu, ganzi hutokana na kuvilia au kusalilia damu katika sehemu moja kwa ufupi damu

kutozunguka katika sehemu ile kwa muda mrefu. Kwa mfano ukikaa sana, au pia ukisamama sana na hii sio sababu ya kukaa na kusimama tu, mwili wa mwanaadamu haustahamili kitu

kupita kiasi.
Miili ya wanaadamu imeumbwa na kiasi kila kitu kwa kiasi, kula kunywa kulala n.k kwahivyo, ikiwa utakaa au utalala kwa muda wa kupindukia bila harakati yoyote basi damu

hushindwa kuzunguka katika mwili na hushindwa kupokea hewa safi na kutoa hewa chafu, ndipo mfumo wa GANZI hutokea na ukianza kufanya harakati tu basi ngazi wenyewe huondoka.Sababu

nyingine ya kufa ganzi kwa mikono au miguu ni upungufu wa Vitamin mwilini mwakoau pia ni Dalili ya wewe kupatwa na
ugonjwa wa Kisukari au ugonjwa wa kiharusi yaani (Stroke). Jaribu

pia kutumia Dawa hii hapa
vitamin B12 itakusaidia kuondosha hayo maradhi ya Kufa ganzi kwa mikono yako.

Ninakushauri nenda haraka Hospitali kamuone Daktari .
 
Kama unajuwa kusoma kiingereza Soma hapa chini

WHAT CAUSES NUMBNESS IN FINGERS AND FEET?
87602489_XS.jpg

Numbness is a symptom associated with a plethora of diseases and disorders. Transient numbness not accompanied by pain or changes in skin color may be a normal response to cold temperatures or other benign conditions. Persistent or recurrent numbness, however, always requires medical attention. Unless other symptoms are present, extensive testing

and evaluation may be necessary before the underlying cause of the symptom is uncovered.

VITAMIN AND MINERAL DEFICIENCIE SLow levels of several minerals, including calcium and phosphorus, may cause numbness in the fingers and feet.

MedlinePlus notes that vitamin B12 deficiency, or pernicious anemia, and some other vitamin deficiencies may also cause numbness in the extremities. Blood tests are effective at determining what deficiencies are present so that dietary changes, supplementation or other treatment options can correct the underlying deficiency and ease symptoms. Low

calcium often occurs in conjunction with vitamin D deficiency, and both problems require correction before a complete resolution of symptoms is possible, according to Merck.STROKE AND TIAStroke and transient ischemic attack, or TIA, often cause numbness and tingling on one side of the body. A TIA, caused by temporary changes in the blood supply to

the brain, produces stroke-like symptoms for up to 12 hours. A TIA may be a warning sign of an impending stroke, but it does not cause the same damage to the brain that a stroke causes.GENERAL MEDICAL DISORDERSVarious medical

disorders may cause numbness in the fingers and feet, including hypothyroidism, shingles, Raynaud's phenomenon and migraines. Shingles is a disorder caused by the same virus, the herpes zoster virus, that causes chickenpox. After a period of dormancy, the virus wakes, affects the nerve roots and begins producing symptoms when the immune system

is weakened due to another reason. Raynaud's phenomenon is a disorder that causes constriction of the blood vessels in the extremities, usually the toes and fingers, resulting in episodic attacks of numbness. The National Institute of Arthritis

and Musculoskeletal and Skin Diseases states that attacks of Raynaud's phenomenon may be triggered by cold or stress. Numbness is also a common symptom of diabetes.

NERVE PROBLEMSMultiple sclerosis is a progressive disorder characterized by damage to the myelin in the central nervous system. This damage interferes with the transmission of

nerve signals and may cause numbness and tingling in the extremities. Other possible causes of numbness in the fingers and feet include seizure disorders; pressure on peripheral nerves caused by tumors, scar tissue, enlarged blood vessels or infection; or pressure on the nerves in the spine.

MEDICATIONS, TOXINS AND CIRCULATORY PROBLEMSMedications, radiation therapy, tobacco use, alcohol abuse and frostbite may lead to loss of sensation in the fingers and feet. Circulatory disorders or impaired circulation due to sitting or standing for prolonged periods may lead to temporary or intermittent numbness. Nerve damage due to lead poisoning is another potential cause, according to MayoClinic.com, but this typically only occurs after months or years of exposure to the toxic metal.
 
madaktari wa jf tafadhali naomba mnieleweshe juu ya hili tatizo kwani nimekua nalo kwa muda mrefu
Na ipi hasa tiba ya tatizo hili?
 
Ni takribani mwaka sasa nyayo za miguu yangu nahisi zikiwaka moto hasa mida ya jioni au usiku ninapokuwa nimepumzika. Nilienda kwa kituo cha afya nikapimwa sukari sikukutwa nayo. Daktari akanipa Vidonge vya neurobions na vitamins nikatumia kwa siku kadhaa hakuna mabadiliko. Doctors out there naombeni msaada wenu kabla sijasonga mbele please.
 
Pole sana kwa mtu ambae mwili wake una waka moto chukua rawanda na kuzbara hindi twanga chemsha kunywa kwani hizo ni balghami itaondoka haraka kunywa glasi 2 kwa siku kwa muda wa siku 7 tu hakikisha umekula chakula ndio ule hiyo Dawa usinywe Dawa kabla hujala chakula ni khatari usikose kuja kunipa Feedback.
 
Nashukuru sana kwa ushauri MziziMkavu nitafanyia kazi ushauri wako. Bado sijajua ili tatizo linasababishwa na nini?
 
rawanda na kuzbara hindi ni nini..cc MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana kwa ushauri MziziMkavu nitafanyia kazi ushauri wako. Bado sijajua ili tatizo linasababishwa na nini?
Mara nyingi, nyayo kuwaka moto huwa inatowa ishara kuwa damu haikosawa, au viungu, yani kukiwa na maradhi kwa mwili, mishipa hubeba damu mpaka kwa nyayo, kutowa toxins mwilini, hivi hufanya nyayo saa ingine kuwaka moto sana. Hata mimi blood sugar yangu iko high, nahisi Mpaka kwa nyayo. sisemi una kisukari. Namaanisha Labda blood sugar iko high.

rawanda na kuzbara hindi ni nini..cc MziziMkavu

Dhania.JPG

Kuzbara kwa kiingereza inaitwa Coriander

rawanda picha yake sina ukizihitaji hizi dawa nenda Kariakoo Mtaa wa Nyamwezi na mkunguni wanapo uza Madawa ya kisunna uliza utapata hapo. Kwani wewe .@
Crashwise Unaumwa na nyayo kuwaka moto?
 
Attachments

  • Kuzabara.jpg
    Kuzabara.jpg
    87.1 KB · Views: 168
mama yangu anakisukari pia miguu huwaka sana moto na kuuma kama inakatwa katwa na wembe
 
Ni takribani mwaka sasa nyayo za miguu yangu nahisi zikiwaka moto hasa mida ya jioni au usiku ninapokuwa nimepumzika. Nilienda kwa kituo cha afya nikapimwa sukari sikukutwa nayo. Daktari akanipa Vidonge vya neurobions na vitamins nikatumia kwa siku kadhaa hakuna mabadiliko. Doctors out there naombeni msaada wenu kabla sijasonga mbele please.

Jaribu kupaka mafuta ya taa fresh(ambayo hayajatumika) asubuhi na jioni ukitaka kulala
 
madaktari wa jf tafadhali naomba mnieleweshe juu ya hili tatizo kwani nimekua nalo kwa muda mrefu
Na ipi hasa tiba ya tatizo hili?
Matatizo ya ganzi na matatizo ya sikio ni tofauti kabisa.

TATIZO LA MIGUU/MIKONO KUFA GANZI

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

FANYA HIVI:

Fanya mazoezi,kula vyakula vyenye virutubisho na kula mboga mboga na matunda.

Nenda kapime Sukari mwilini mwako kuhakikisha huna Maradhi ya ugonjwa wa kisukari.

Kanunuwe Dawa hii Vidonge vya
Vitamin B12 uwe unakula kila siku kidonge 1

baada ya kwisha kula. Pendelea kula vyakula hivi kila siku.

375x321_vitamin_b12_ref_guide.jpg

eggs.jpg

799px-Feta_Greece_2.jpg

(Cheece) Jubini.

Tumia Dawa kisha uje hapa unipe feedback.

Mwambie Mama yako apakae hina nyayoni kwa muda wa siku 7 kisha uje hapa utupe feedback.

Mke wangu alipatwa na tatizo hili kwa muda wa mwezi mmoja.Tatizo hili lilipelekea kukonda kwa haraka sana kwa sababu usiku alikuwa halali,Nilipitia uzi mmoja ambao MziziMkavu alitoa maelezo kama haya lakini hakuna unafuu uliopatikana, pamoja na kwenda kwa madaktari na kutoa dawa lakini madaktari wanazidiana kwani wengine waliandika hizo neurobian pamoja na dawa moja ya tube ya kupaka kwenye unyayo ila haikutibu tatizo ingawa lilipunguza tu. Baadae tulienda hospitali ya Nyakahoja jijini Mwanza na kumuona daktari mmoja ambae alikuwa ufumbuzi wa tatizo hili. Baada ya vipimo aliagiza kuwa mke wangu ajitahidi kunywa maji wastani wa lita 3 kwa siku kwa muda wa siku 7, vile vile aliandika dawa za aina mbali mbali ambazo nakumbuka ni CETRIZINE, NEUROBIAN, Elavil (AMITRIPTYLINE) pamoja na dawa fulani ya vidonge jina lake limenitoka. Ila katika yote hiyo Elavil ni komesha ya hilo tatizo.
Alitumia dozi hiyo kwa muda wa siku 10 tu baada ya hapo likaisha kabisa. Tuliporudi kwa dokta alimuongezea dozi nusu dozi kwa kuwa alikuwa ametumia nusu dozi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom