Uko salama, sasa cha kufanya, kwanza acha kabisa vinywaji vyenye kaffeina i.e chai, kahawa, soda zote na juisi zote za viwandani, punguza au acha kabisa vyakula au vinywaji vyenye asidi nyingi na mwisho fanya zoezi hili kila siku; lala chali mgongo chini halafu unainua mguu mmoja juu kisha unaushusha na kuuinua mwingine juu tena hivyo hivyo ukipishanisha huu juu huu chini, fanya taratibu siku ya kwanza dakika 5 siku ya pili dakika 10 hivyo hivyo unaenda ukiongeza, usifanye kwa fujo siku ya kwanza tu, fanya kwa wiki 2 mfululizo. Zoezi hilo litafanya damu iliyokuwa imegandamana chini ya miguu kurudi juu mwilini na hivyo asidi kutoka ndani ya mwili na taratibu miguu kuwaka moto itaacha.
Pia kumbuka kunywa maji ya kutosha mpaka lita 3.7 kwa siku na utafune mara kwa mara chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa/haijapita kiwandani.