Steph Curry
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 5,936
- 4,707
Habarini za jioni wakuu, poleni kwa mihangaiko ya kila siku...
Jamani nina tatizo la miguu kuwaka moto kila nikiingia kitandani kulala.. Hili jambo limekuwa likinisumbua miezi kadhaa sasa. Mwanzoni nilidhani ni kwakuwa natembea peku kwenye tiles.. Nikaacha hiyo tabia nikawa navaa ndala kila wakati lakini bado hili jambo linanisumbua..
Naamini humu kuna madaktari na watu walio'experience hili jambo, naombeni msaada wenu jamani nifanyaje??
Vuta subira kidogo watakuja sasa hivi. Tuwasikilize wa pande zote wale wa darasani na akina Kingunge
Punguza pombe, kama huwezi jitahidi kunywa maji mengi angalau glass 12 kwa siku lakini uwe unakunya sana sio unajibanabana wakati mavi yanaumaa!
mbona mi nina 62 na inawaka motoNi uzito tu unaosababisha hayo nilikuwa na tatizo hilo wakati huo nilikuwa na kg. 83 kwa sasa nimepungua uzito nina kilo 76 tatizo limekwisha kabisa. Hivyo nakushauri fanya mazoezi ya kupunguza uzito tu tatizo
litakwisha.
Miiguu kuwa na ganzi,ni kwanini na nitumie dawa gan?
pole sana mkuu. cc mzizi
Habari.
Ndugu wana Jf, kwa takribani zaidi ya mwaka sasa, ninasumbuliwa na tatizo la nyayo za miguu kuwaka moto.
Wakati inaanza nilijua tatizo ni aina ya viatu ninavyo tumia, nikabadirisha na tatizo likabaki pale pale.
Nikaamua kwenda hospitali mara kadhaa bado tatizo halija ondoka,(dawa nilizo tumia, ni multvitamin, neurobine, na neuro support. na siku hizi, nyayo zina uma mda wowote tofauti na mwanzoni ambapo nyayo zilikuwa zinauma wakati wa usiku pekee.
Pia, nyayo zikiuma nnakuwa najisikia hali ya kuchoka sana, na kukosa nguvu.
Hospitali nilizo enda ni za serikali, moja ya wilaya na nyingine ni ya mkoa.
Sasa nnawaomba ndugu zangu, msaada wa mawazo wa jisni ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu, eidha kwa kunielekeza hospitali ambayo nnaweza kwenda kupata matibabu kwa gharama yeyote ile nipo tayari.
Na kama kuna mtu aliwahi kupata hili tatizo, na likatatuliwa nnaomba unishirikishe na mimi nipate kupona maana nnateseka.
Asanteni.
TATIZO LA MIGUU/MIKONO KUFA GANZI NA KUWA MOTO
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili
yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu,
Ushauri wangu kabla ya Tiba.
(1) Nenda Hospitali kapime huenda una ukosefu wa Vitamini Mwilini.
(2) Kapime Mapigo yako ya Moyo na figo na ini lako je yote hayo Yapo Sawa?
(3) Kapime Ugonjwa wa Kisukari.
(4) Je una kunywa Pombe? kama unakunywa Pombe acha. je unavuta Sigara? Je una kilo ngapi?
Ukimaliza yote na upo powa hujapata dawa nitafute mimi dawa ya kukutibu Maradhi yako