Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
ndugu jf doctor nina tatizo, mguu wangu wa kushoto ganzi inanisumbua, kuunyanyua na kutembea naweza ila nasikia ganzi, nikilala ndo nasikia maumiv yan hiyo ganzi yenyewe na nikiwa natembea kuifeel ile ganzi kunapungua ila nikisimama au kukaa naisikia lakin kwenye mguu wa kulia niko poa ni huu mguu wa kushoto tu kuanzia juu ya magot had chin, naomba ushauri wako
TATIZO LA MIGUU/MIKONO KUFA GANZI
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili
yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu,
Ushauri wangu nenda hospitali kapime Figo lako je linafanya kazi vizuri? kapime Ugonjwa wa kisukari, kapime
Je una upungufu wa Vitamini mwilini? Kapime Mapigo ya moyo au una ugonjwa wa Presha? Ukitaka dawa