Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

ndugu jf doctor nina tatizo, mguu wangu wa kushoto ganzi inanisumbua, kuunyanyua na kutembea naweza ila nasikia ganzi, nikilala ndo nasikia maumiv yan hiyo ganzi yenyewe na nikiwa natembea kuifeel ile ganzi kunapungua ila nikisimama au kukaa naisikia lakin kwenye mguu wa kulia niko poa ni huu mguu wa kushoto tu kuanzia juu ya magot had chin, naomba ushauri wako

TATIZO LA MIGUU/MIKONO KUFA GANZI

670px-Cure-Numbness-in-Your-Feet-&-Toes-Step-6.jpg

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

Ushauri wangu nenda hospitali kapime Figo lako je linafanya kazi vizuri? kapime Ugonjwa wa kisukari, kapime

Je una upungufu wa Vitamini mwilini? Kapime Mapigo ya moyo au una ugonjwa wa Presha? Ukitaka dawa
 
Mmh. Pole sana. Alichosema mshauri wa kwanza kinawezeka. Mimi si dr lakini unachopitia niliwahi kupitia nikatibiwa na sasa nimepona. Nilikutwa na shida katika uti wa mgongo iliyosababisha usumbufu kwenye mishipa ya fahamu. So ili kutibu ilibidi warekebishe tatizo kwenye pingili za mgongo. Nilianza tiba kitengo cha bima ua afya muhbili kilichopo ocean road wakanipa reffaral muhimbili kitengo cha mifupa then MOI. Sijui umri wako na shughuli zako ningekushauri zaidi kwani mimi niliteseka almost 3 month hafi kupata tiba sahihi nawrza sema ninaexperience na aina hyo ya maumivu. Huwa nasikia uchungu mwingine akiyapitia hayo.

Mimi ninakushauri uende Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI) Ukatibiwe. Kwani pia inawezekana tatizo lako limeanzia mgongo. Kama na wewe una bima ya afya fuata mlolongo huo ni njia rahisi sana kupata refaral ya Muhimbili ukapate tiba sahihi kwa madr sahihi.
 
Fika Muhimbili hospital muone neuro physician anaitwa Dr Njenje atakupima vipimo vya nerves conduction studies.
 
Nenda uangaliwe kama uko na dvt(deep venous thrombosis)...upewe blood thinners
 
Hellow WanaJF,

Kuna ndugu yangu anasumbuliwa sana na kichwa. Kwa muda mrefu sana amejaribu kwenda Hospitali, anapimwa macho na kupewa miwani bila mafanikio yoyote.

Na pia miguu inamsumbua, ganzi katika miguu na vichomi pia.

Kwa mtaalamu anayejua nini tatizo, naomba anijuze.
 
nasumbuliwa na tatizo la nyayo kuwaka mota karibu mwaka mmoja na nusu sasa hasa ninapokua nimekaa ila nikiwa natembea sisikii na kuna wakati huwa hali hiyo hupotea na muda mwingine hujirudia na pia nina taizo la vidonda vya tumbo kwa miaka minne sasa nasikia matangazo mengi ya tiba mbadala ila naogopa kuliwa pesa kama nilivyopoteza kwa tatizo la vidonda vya tumbo mwenye kujua wataalam walipo anisaidie

Habari mkuu. Vipi ulipona tatizo lako? tupe feedback kaka
 
Habar Wana Jf, My Sister Alifanyiwa Opereshen Ya Mgongo Alikua Na Tatizo La Disk Imepita Kama Miaka 9 Sasa, Wiki Hii Alivokua Anadeki Choo Aliteleza Akaanguka, Ameumwa Sana Mgongo Na Anapata Ganz Mguu Mmoja, Alivoenda Hosptl Amepigwa X-ray Wakamwambia Asubir Tangu Ijumaa Had Juma 4 Amuone Speshalist Kutoka Kcmc, Kwa Kweli Halal Ucku Na Mchana Jaman, Naomba Ushaur Wa Doctor Pls,,, Dawa Yoyote Ya Maumiv Haimsaidii
 
Ndugu zangu nasumbuliwa na maumivu ya tumbo nakuwa nahisi kama kuna kitu tumboni ambacho hunisababishia mpaka upumuaji kuwa wa shida na kuhisi maumivu ya tumbo.

Pili miguu kuwa na ganzi ya muda mrefu kuanzi unyayo mpaka magotini, ngozi inavuta mpaka inaletea hali ya maumivu fulani na kuhisi kuchochoma na kushindwa kutembea kwa umbali mrefu, hali hii pia ipo kuanzia kwenye viganjani mpaka kwenye kiwiko.

Naombeni ushauri hizi ni dalili za ugonjwa gani?

Na ni wapi naweza pata huduma bora ya dokta?
 
Ndugu zangu nasumbuliwa na maumivu ya tumbo nakuwa nahisi kama kuna kitu tumboni ambacho hunisababishia mpaka upumuaji kuwa wa shida na kuhisi maumivu ya tumbo.
Pili miguu kuwa na ganzi ya muda mrefu kuanzi unyayo mpaka magotini, ngozi inavuta mpaka inaletea hali ya maumivu fulani na kuhisi kuchochoma na kushindwa kutembea kwa umbali mrefu, hali hii pia ipo kuanzia kwenye viganjani mpaka kwenye kiwiko.
Naombeni ushauri hizi ni dalili za ugonjwa gani? Na ni wapi naweza pata huduma bora ya dokta?

Umeshapima shinikizo la damu ndugu??
 
MKUU MATATIZO YAKO HAYO YANASABABISHWA NA UTUMBO KUWA MCHAFU[0659-649891)

UMUHIMU WA KUSAFISHA UTUMBO MPANA
Kuna sababu 18 ambazo zinkupelekea ULAZIMIKE kusafisha utumbo wako MPANA. HILI ni eneo ambalo uchafu wote ambao unahitajika kutoka kwa njia ya haja KUBWA UNAKWAMA.
1. UCHAFU HUO HUPELEKEA WADUDU WENGI KUISHI ENEO HILI KAMA BACTERIA,VIRUS, MINYOO YA KILA AINA NA UKUBWA MBALI MBALI
2.VYUMA KUTOKA VIWANDANI NA MASUFURIA YA ALUMINIUM YATUMIKAYO KUPIKIA
3. MAFUTA YALIYOGANDA KWENYE KUTA ZA TUMBO
4. MAWE
5.PRESERVATIVES( KEMIKALI ZINAZOZUIA VITU VINGINE VISIHARIBIKE)
MKUSANYIKO WA UCHAFU WA AINA ZOTE HIZI HUSABABISHA MATATIZO NA MAGONJWA YAFUATAYO;
1. KUTOPATA CHOO MARA MBILI NA ZAIDI KWA SIKU
2.KUWA NA GESI TUMBONI
3. TUMBO HUCHAFUKA MARA KWA MARA
4.MATATIZO YA MAGONJWA YA MOYO
5.KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUME
6.MATATIZO YA HEDHI
7.UTI SUGU
8.KIUNGULIA
9.GANZI YA MIGUU NA VIDOLE
10.MIFUPA KUVIMBA
11.KUBADILIKA BADILIKA KWA KIWANGO CHA SUKARI KATIKA DAMU
12.MAUVIMBE MWILINI NA SARATANI YA TUMBO
13.MAGONJWA YA NGOZI
14. KUKOSA USINGIZI NA KUMBU KUMBU
15.MWILI KUKOSA NGUVU
16.HARUFU MBAYA MDOMONI NA KIKWAPA
17.MACHO KUTOONA VIZURI
18. UVIMBE WA TEZI DUME(PROSTATE GLAND)
4LIFE FIBRE SYSTEM PLUS | Afya4life
UNAWEZA KUSAFISHA TUMBO HILO KWA KUTUMIA 4LIFE FIBRE SYSTEM PLUS( 10 DAYS) AU kwa KUTUMIA TEA4LIFE KWA MUDA WA SIKU 30.
 
Ni vyakula gani vya asili vinaweza kuondoa tatizo hilo?
 
Kuna dawa zozote unatumia au uliwahi kutumia kwa muda mrefu huko nyuma? Ushauri r?hisi nenda hospitali na onana na daktari....usichelewe...
 
ndg maumivu si ugonjwa bali ni dalili la tatizo katika moja au viungo vyako mwilini,so kwa hali unayojisikia inakupashwa kufanya vipimo vingi tu itategemeana na wewe utakavyo jieleza kwa dr na jinsi atakavyo kuelewa ,mara nyingi ni vyema ukaonana na dr pale unapokuwa na hayo maaumivu kwani nafahamu definitely hayo maumivu hayapo muda wote hii itasaidia hata dr kukupalpate na kujua kiungo gani especially tumboni kina hayo maumivu
NENDA HOPSPITAL
 
Jamani naombeni mnisaidie mguu wangu wa kushoto unawaka moto sana ni kma wiki tatu sasa hili tatixo lipo.nimetumia dawa ya kienyeji lakini tatizo bado linaendelea tu.naombeni msaada watalaam
 
Back
Top Bottom