Naomba msaada kwa doctors wa jf tatizo langu kutokwa na vipele vya ndevu mpk vimekomaa nmejaribu kutumia bump patrol , epiderm cream na dawa nyinginezo ningeomba dawa tofaut na hiz wenda ningepona msaada zaid
Na mimi pia hili tatizo linanisumbua sana. Nimejaribu mbinu nyingi ila imeshindikana....
Nilikuwa na tatizo kama lako ila lilikwisha bila kutumia dawa yoyote ile zaidi ya kutopaka dawa yoyote baada ya kushave na kumweleza kinyozi tatizo langu nayeye hakati ndevu mpaka chini kabisa kwenye kiini, au ile ananiambiaga atatumia wembe namba 1 ili MAUPELE yasinitoke tena.
Nakushauri pindi unaponyoa ndevu zako shave to the direction of your hairs hii ndo suluhisho mwenyewe nilikuwa na tatizo kama lako nimetumia dawa nyingi mfano pump patrol na after shave lotion ikashindikana jaribu uttupe mrejesho
Nikiwa Morogoro saluni fulani siwezi kuitaja jina mara nyingi huwa napendelea kwenda kunyoa nikiwa huko,kuna kinyozi wa hiyo saluni aliniambia:
Brother hii magic sio nzuri kiafya maana kuna wateja wangu watatu walikuwa wanatumia kunyoa nywele(kipara)kwa kutumia magic walifariki na karibu wote watatu vifo vyao vilifanana.Kwa mujibu wa mtoa taarifa ni kwamba waliumwa vichwa sana kabla ya umauti kuwafika.
My take:
Kwa akili ya kawaida tu bila kuwa mtaalamu wa afya,inakuwaje nywele na ugumu wake hata uifukie chini miaka haiozi lkn ije kutoka kwa kukwangua tu baada ya nusu saa?
Wazungu wanatuua,cha kushangaza kwenye kopo la magic powder pameandikwa:FOR BLACK SKIN ONLY!
tumia dawa inaitwa magic powder, ni unga flani ambao ukichangaya na maji inakuwa kama cream unapaka kisha baada ya dakika chache ndevu zinatoka zenyewe kwa kufuta na kitambaa. saloon nyingi mjini wana hiyo huduma, vipele utavisikia kwenye bomba
Mimi nilijaribu Mara moja nikaipenda sana! Nikaenda kununu kikopo kizima maana mi huwa nasafiri Kwa Malory lakini wiki moja kabla dawa magic powder kwisha nikaanza kuona nikiitumia kidevu kinawaka moto kuja kucheki kidevu kinaelekea kuungu na kuweka vidonda nikaiacha wembe unanitoa mapele zaidi ya fenesi sasa nayumia mashine nimenunua lakini changa moto iko hapa nitasafiri na mashine kila mahali? Je nikikuta hakuna umeme nilipoenea nitaishije maana nikipitisha muda wa kunyoa ni balaa lazima ninyoe kila baada ya siku mbili au tatu zikizidi hapo nakoma sasa kuna mtu kasema anauza lotion ya aloe vera inamaliza mapele na muwasho baada ya kunyoa anadai bei yake ni elf 35 kama kuna mtu aliye wahi tumia naomba Matokeo tafadhali maana ameniambia ukitumia siku 60 kama haikusaidii unarudishiwa hela yako yote
Megic inaleta mvi.
Duuuuh!!! Kila baada ya siku mbili unanyoa ndevu kama afande kwanini?