Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Na mimi pia hili tatizo linanisumbua sana. Nimejaribu mbinu nyingi ila imeshindikana....
 
Wana Jamiiforums,

Hebu nisaidieni hivi kuna madhara gani kutumia magic kutolea ndevu.

Maana kuna jamaa yangu moja hapa ananiambia inasababisha kansa hivi ni kwel?
 
Mimi nlitumia mara moja sikurudia tena nliona kidevu kinachemka chenyewe.nywele huwa haziozi bt hiyo dawa ukipakwa ndani ya dakika10 ndevu inatoka kirahisi lazma ina side effect kubwa badae ni chemical kali sana
 
Mhh mi natumia megic powder mwaka wa nane sasa sikuona madhara yoyote mi naona kutokana ma mwili maana hata mi nikitumia kiwembe napata vipele sana
 
Mm nilitumia kwa kudhani ingenisaidia kuzuia vipele vya ndefu ila haikufanikiwa nilijaribu njia zingine za kuzuia vipele nikafanikiwa kwahiyo nina mwezi wa sita sasa situmii magic.nikienda salon nanyoa tu ndevu kawaida bila magic
 
Nilitumia mara moja na sitokaa nirudie tena. Uso wote uliharibika na chunusi nyingi zilinitoka....
 
Mpwa tumia machine tu mbona inatoa ndevu vzr tu hayo mengine achana nayo
 
vipele vinat0kana na ng0z ya m2. .wengne hawajawah kut0kwa na upele khabsa .na wana2mia mashne...magic uzeeni huenda ikakuletea cancer ya ng0zi.
 
Nikiwa Morogoro saluni fulani siwezi kuitaja jina mara nyingi huwa napendelea kwenda kunyoa nikiwa huko,kuna kinyozi wa hiyo saluni aliniambia:

Brother hii magic sio nzuri kiafya maana kuna wateja wangu watatu walikuwa wanatumia kunyoa nywele(kipara)kwa kutumia magic walifariki na karibu wote watatu vifo vyao vilifanana.Kwa mujibu wa mtoa taarifa ni kwamba waliumwa vichwa sana kabla ya umauti kuwafika.

My take:
Kwa akili ya kawaida tu bila kuwa mtaalamu wa afya,inakuwaje nywele na ugumu wake hata uifukie chini miaka haiozi lkn ije kutoka kwa kukwangua tu baada ya nusu saa?

Wazungu wanatuua,cha kushangaza kwenye kopo la magic powder pameandikwa:FOR BLACK SKIN ONLY!
 
Ni njia gan ya kutoa vipere vya ndevu wakuu??

Usinyoe ndevu kama hutaki vipele.

Kama lazma unyoe mfn mwanajeshi, polisi, mwanafunzi sekondari, n.k. basi nyoa kila siku bila kuacha. Lakini lazma upate vijipele vidoogo ambavyo huwa havikeri wala kuharibu uso.

Wakati unanyoa, fuata ulalo wa ndevu zako. Usiende kinyume.

Maandalizi, lainisha ndevu kwa maji ya vuguvugu na sabuni ya kawaida.

Ukinyoa baada ya kuoga ndevu zinakua zimelainika vizuri zaidi.
 
wenzetu hawatumii hii makitu nlisafiri sku mmoja nkaitafta bila mafanikio nimeachana nayo mwaka wa tatu sasa nashauri mtu uwe na mashine yako mwenyewe ujinyoe ndevu tu hautapata vipele
 
Nilitumia magic powder kwa miaka miwili 2006-2008 baadae ikaanza kunitesa kwa vipele nikaachana nayo ila sahivi nafikiri imeanza kuniletea madhara naanza kupata MVI kidevuni wakati hata 35 sijafika!!!
Nashauri watu wasipendelee kuitumia.
 
Kuna mshikaji fulani aliitumia tukiwa sekondary. Aliumuka uso mzima. Tukaogopa.

Sijawah kuitumia na sitakaa niitumie
 
Niliobahatika kuwaona kadhaa wana vipele sugu
 
Back
Top Bottom