KERO Tatizo la Usafiri kwa Wananchi tunaoishi MOSHONO - ARUSHA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi tunaoishi Moshono Arusha tunapata sana shida ya usafiri wakati wa asubuhi tunapoenda kwenye shunguli zetu na jioni tunaporudi majumbani.

Hali hii imechangiwa na baadhi ya madereva wa daladala zinazoenda Moshono kuzuia Bajaji zilizokuwa zinafika hadi Moshono zisiende tena Moshono na ikitokea wakaenda basi wanakamatwa na hao madereva daladala.

Hii sio sawa sababu daladala asubuhi zinapita zimejaa sana na kuacha baadhi ya wananchi barabarani tukikosa usafiri na kuchelewa kwenye shughuli zetu. Na je kwanini iwe ni Moshono peke yake wakati maeneo mengine Arusha bajaji zinaendelea na kazi (hata hii barabara ya kwenda Moshono kuna bajaji zinaishia Kijenge na zinabeba abiria kama kawaida).

Je sisi wananchi tunaokaa kuanzia Suye, Boma Siara, Moshono kona, Laizer tutaendelea kuteseka na usafiri hadi lini?? Tunaomba serikali isaidie usafiri wa bajaji urejee kama kawaida kupunguza hii shida LATRA, Mbunge wa Arusha mjini, Halmashauri ya jiji Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Amos Makala, tunaomba mtusaidie kutatua hili tunateseka sana.
 
Daladala Zipo Za Kutosha Barbara ya Moshono.
Changamoto Ni pale wanapokatia Barbara ya uzunguni kuelekea Fire kisha Samunge na kuathiri wasafiri wanaotaka kupita Naaz, Metro hadi Friends Corner.
Bajaj hazina shida zenyewe zinapita Naaz hadi Posta bila shida.
 
Wananchi tunaoishi Moshono Arusha tunapata sana shida ya usafiri wakati wa asubuhi tunapoenda kwenye shunguli zetu na jioni tunaporudi majumbani.

Hali hii imechangiwa na baadhi ya madereva wa daladala zinazoenda Moshono kuzuia Bajaji zilizokuwa zinafika hadi Moshono zisiende tena Moshono na ikitokea wakaenda basi wanakamatwa na hao madereva daladala.

Hii sio sawa sababu daladala asubuhi zinapita zimejaa sana na kuacha baadhi ya wananchi barabarani tukikosa usafiri na kuchelewa kwenye shughuli zetu. Na je kwanini iwe ni Moshono peke yake wakati maeneo mengine Arusha bajaji zinaendelea na kazi (hata hii barabara ya kwenda Moshono kuna bajaji zinaishia Kijenge na zinabeba abiria kama kawaida).

Je sisi wananchi tunaokaa kuanzia Suye, Boma Siara, Moshono kona, Laizer tutaendelea kuteseka na usafiri hadi lini?? Tunaomba serikali isaidie usafiri wa bajaji urejee kama kawaida kupunguza hii shida LATRA, Mbunge wa Arusha mjini, Halmashauri ya jiji Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Amos Makala, tunaomba mtusaidie kutatua hili tunateseka sana.
Mbunge wenu Makonda anajua mnapitia hiyo changamoto?
 
Mtoa mada tatizo ni nini? Hakuna route ya daladala au daladala hazifiki?

Bajaji sio usafiri wa umma.
 
Hili ndio tatizo kubwa na ukimuuliza dereva kwanini unapita huku na sisi tunashuka sehemu fulani utajibiwa majibu mabaya, tunaoenda kwenye shughuli asubuhi tunapata sana tabu. Tunakubali daladala zipo nyingi lakini bajaji hawana hizi tabia na wanatusaidiaga sana tunaowahi kwenye shughuli asubuhi hatupati hii shida
 
Mtoa mada tatizo ni nini? Hakuna route ya daladala au daladala hazifiki?

Bajaji sio usafiri wa umma.
Kama sio usafiri wa umma kwanini ni Moshono pekee ndio zizuiwe na maeneo mengine zinaendelea na kazi kama kawaida?
 
Back
Top Bottom