Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.

Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.

Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.

Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.

Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.

Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.

Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.

Serikali ingefanya jambo katika swala hili.

Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.

Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.

Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.

Hii ni orodha ya makampuni ambayo vijana wa mafuta na gesi wana nafasi ya kuajiriwa hapa Tanzania.
  • Shell Tanzania
  • Total Tanzania Ltd
  • East African Crude Oil Pipeline (EACOP) project In Tanzania
  • Swala Oil and Gas Tanzania Plc
  • Statoil Tanzania Limited
  • Ndovu Resources Ltd/Aminex Plc
  • CAROIL(T) limited
  • Equinor Tanzania
  • Songas Limited
  • Dodsal Resources & Mining Itingi (Tanzania) Pvt. Ltd
  • Maurel exploration Production Tanzania Limited
  • Artumas Energy Ltd. (Wentworth Resources Limited)
  • Lake Oil Ltd.
  • Pan African Energy Tanzania Ltd
  • Heritage Oil Tanzania Ltd
  • Tanzania Petroleum Development Corporation
  • Orca Exploration Group Inc.
  • Petrofuel
  • Barkat Gas
  • Oilcom (T) Limited Terminal
  • Swala Oil and Gas (Tanzania) PLC (SOGTP)
  • State Oil
  • Halliburton
  • Aminex PLC
  • Oryx Energies
  • Lake Group
  • PUMA
  • MOGAS
  • VIVO Energies
  • TPDC
  • EWURA
  • TBS
  • PURA
  • OIL COM
  • N.K
Ahsante sana
Kwa nini wahitimu wanajifunga Tanzania tu wakati fani hizi zinahitaji wahitimu wa kuzifanyia kazi dunia nzima?

Wahitimu wetu wamejiandaaje kushindana katika soko la ajira la kimataifa?
 
Back
Top Bottom