Tatizo siyo viongozi wala vyombo vya dola bali mamlaka makubwa aliyonayo Rais, mwishowe wanafanya kazi kulinda ugali wao!

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa sana, yapo mambo makubwa ambayo yanahitaji hadi Rais ashirikishwe kufanya maamuzi lakini mambo mengi hupuuzwa.

Kwa sababu Katiba imempa mamlaka makubwa mkuu wa nchi hasa kwenye teuzi na mambo mengine ndiyo maana anapoona unaenda kinyume naye utaishia kutumbuliwa na wengine kuendelea.

Nchi yetu viongozi wengi wanateuliwa na Rais, humwabudu Rais kama mungu wao hata akikosea NI vigumu sana kumkosoa na hata kumshauri maana huamini kuwa endapo watamshauri wanaamini kuwa wanaweza kukosea na kutumbuliwa!

Haya tunayaona kwenye ngazi za wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla wengi wetu tunatetea ugali wetu ili watoto wasiende kwenye shule za walimu wawili watoto 300 na ndiyo maana ukiwasikiliza waliowengi kauli yao ni "Fanya kazi uondoke watakuja wengine"!

Maneno kama haya ndiyo yanafumaza maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa na katiba mbovu.
 
Muliro amesema ukweli, lkn ni ukweli mchngu, kwamba "rais ametoa uhuru wa kusema lkn wanaovuka mipaka hutekwa na polisi". Soon anaweza kutumbuliwa.
 
Lost generation ina kazi kubwa ya kufanya kuinusuru nchi
 
Vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa sana, yapo mambo makubwa ambayo yanahitaji hadi Rais ashirikishwe kufanya maamuzi lakini mambo mengi hupuuzwa...
Wakati mwingine tunamlaimu Rais bure. Fikra za kitumwa na kujipendekeza ndiyo tatizo linaloweza kufanya hata Rais mwenyewe ashangae.

Kujipendekeza husababisha matendo ambayo humletea Rais sifa mbaya kwa wananchi wake.
 
Vyombo vyetu vinafanya kazi kubwa sana, yapo mambo makubwa ambayo yanahitaji hadi Rais ashirikishwe kufanya maamuzi lakini mambo mengi hupuuzwa.

Kwa sababu Katiba imempa mamlaka makubwa mkuu wa nchi hasa kwenye teuzi na mambo mengine ndiyo maana anapoona unaenda kinyume naye utaishia kutumbuliwa na wengine kuendelea.

Nchi yetu viongozi wengi wanateuliwa na Rais, humwabudu Rais kama mungu wao hata akikosea NI vigumu sana kumkosoa na hata kumshauri maana huamini kuwa endapo watamshauri wanaamini kuwa wanaweza kukosea na kutumbuliwa!

Haya tunayaona kwenye ngazi za wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla wengi wetu tunatetea ugali wetu ili watoto wasiende kwenye shule za walimu wawili watoto 300 na ndiyo maana ukiwasikiliza waliowengi kauli yao ni "Fanya kazi uondoke watakuja wengine"!

Maneno kama haya ndiyo yanafumaza maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa na katiba mbovu.
Tatizo kubwa ninaloliona hapa nchini ni Katiba ya nchi tuliyonayo ambayo ni mbovu

Inabidi Kila mtu atetee "ugali" wake,.

Wewe umeshawahi kuona nchi Gani katika dunia hii, ambayo Rais wa nchi anateua Kila nafasi nyeti ya nchi?

Yeye ndiye anateua Jaji Mkuu na Majaji wote wa Mahakama Kuu, maRC"s, maDC"s, DED"s wote wa nchi hii!
 
Kwa kweli katiba yetu inamfanya raisi kuitwa mungu ! Chawa ukiwaambia mambo kama haya wanakwambia katiba haiwezi kuleta maendeleo huwa nacheka Sana ! Wengine tukiamka nao haifiki jioni hajakuomba tsh 20,000/= ya matumizi! Nashangaa Sana mama anavyopiganiwa watu wanatoka dodoma tabora shinyanga n.k wanaenda katavi kumfurahisha Tu mama [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Elimu elimu elimu
 
Tatizo kubwa ninaloliona hapa nchini ni Katiba ya nchi tuliyonayo ambayo ni mbovu

Inabidi Kila mtu atetee "ugali" wake,.

Wewe umeshawahi kuona nchi Gani katika dunia hii, ambayo Rais wa nchi anateua Kila nafasi nyeti ya nchi?

Yeye ndiye anateua Jaji Mkuu na Majaji wote wa Mahakama Kuu, maRC"s, maDC"s, DED"s wote wa nchi hii!
Katiba ya kijinga sn
 
Back
Top Bottom