Uchaguzi 2020 Tazama hii video ya kivuko alichozuiwa kupanda ndugu Tundu Lissu kwa madai kuwa ni kibovu kikiwa Mwibara kisha soma ufafanuzi wa yaliyotokea

Uchaguzi 2020 Tazama hii video ya kivuko alichozuiwa kupanda ndugu Tundu Lissu kwa madai kuwa ni kibovu kikiwa Mwibara kisha soma ufafanuzi wa yaliyotokea

Lissu ameambiwa yakua kivuko ni kibovu na hakuna safari ya Ukerewe leo yote.

MaCCM hovyo sana.
 
Ubovu wa kivuko cha Kisorya - Ukerewe
Lakini uongo wao wa kivuko kibovu umeanikwa hadharani. Huu ubaguzi wa kutisha unaofanywa na huyo anayejiita MWENDAWAZIMU unaleta chuki za kutisha nchini na kuharibu kabisa mshikamano wa miaka mingi. Ni ushahidi tosha kwamba ukisikia mtu anajiita KICHAA basi muamini na usimpe uongozi wa mahali popote pale kwani ATAVURUNDA TU!
 
Kivuko kimelalamikiwa ubovu tangu kipindi hicho. Shukuruni tu Lissu hajahatarisha maisha yake. Je kingepinduka. Zengwe nyingine ni baraka ujue
Numbisa hii thread ni ya April 2020 haina uhusiano wowote na hali ya kivuko leo hii. Kivuko leo hii hakikuwa kibovu.
 
Anazidi kutengeneza chuki kwa watu.

Tusiendelee na ratiba zetu kisa mtu mmoja na interest zake?

Haiingii akilini.

Police au askari wakiamua kuvunja vioo vya magari na kuamua ku unlock hizo gari then wa park pembeni ili shughuli ziendelee kawaida utasikia poliCCM au askaliCCM.Kumbe wanayataka wenyewe.

Hii ni aibu kwa msafara unaoongozwa mwanasheria kublock public way⚠.

Nakiri kusema jeshi la polisi wanatakiwa kuwa na busara sana katika wakati huu. but wakiaamua kutumia sheria Lissu anaenda kukiponza chama cha chadema pakubwa sana na hata kufutwa kabisa.
We lizombie umeelewa kilichotokea kweli?Naona unatoa maushuzi tu
 
Yawezekana wote Ni watoto, au mmoja wao Ni mtoto.
1. Wote Kama kivuko kilikua kizima halafu wakamdanganya kwamba HAKITA TENGEMAA LEO " Siku hiyo" ili asipate hiyo huduma.
Halafu yeye na watuwake wakajua Ni kizima Kisha wakaziba njia kwa makusudi.

2. Mamlaka Ni watoto Kama walisema leo hakifanyi kazi kwa sababu yeyote Ile ili tu asipate huduma.
Na yeye kwa kuona hivyo akaacha hapo magari. Sio kwa lengo la kufunga njia , ila kwasababu alijua haita itajika maana hamna huduma siku hiyo.

3. Na wajinga watakua wenye msafara na madereva wao Kama Ni kweli kilikua kibovu kwa mda huo. Ila huduma ilikua irejee mda wowote kikitengemaa. Nao walijua Hilo wakafunga njia kwa makusudi.
Kama ni hivyo kweli waombe msamaa wananchi walioathirika.

4. La hasha walijisahau na kuacha kwa kutojua Kama baadae njia ingehitajika Basi hiyo itakua bahati mbaya hata hivyo kiungwana bado waombe msamaha.

Ila kwa upande wa mamlaka , nna wasi wasi maana Kama walijua kwamba huduma ingerudi na Kama walikua hawana shida na msafara kufahamu Hilo, kwa nini wasingewaelekeza msafara waweke magari pembeni ili huduma ikirudi wasiathiri utaratibu wa kutoka kwenye kivuko.

Inanitiliashaka labda waliwalaghai.
Au labda na wao walijisahau.
Hivyo Mamlaka waombe radhi wanachi na waombe radhi msafara kwa kujisahau au kwa kutowapa maelekezo stahiki.
 
Numbisa hii thread ni ya April 2020 haina uhusiano wowote na hali ya kivuko leo hii. Kivuko leo hii hakikuwa kibovu.
Leo hii Kivuko kilikuwa kinafanya kazi na kama kiliruhusiwa kubeba Watanzania wengine leo hii basi kingeweza kabisa kumbeba Lissu na timu yake yote lakini kutokana na yule mbaguzi anayejiita MWENDAWAZIMU wafanyakazi wakaambiwa waseme uongo ili tu Lissu ashindwe kuvuka. Ubaguzi kama huo haukubaliki hata chembe. Lissu ni Mtanzania na pia ni mlipa kodi anastahili kutendewa haki popote pale ndani ya Nchi yetu.
Kivuko kimelalamikiwa ubovu tangu kipindi hicho. Shukuruni tu Lissu hajahatarisha maisha yake. Je kingepinduka. Zengwe nyingine ni baraka ujue
 
Nchi hii kila mtu akiamua anafunga njia maana naona wote wanafanya hivyo sasa. Kuanzia wale wa chama tawala na sasa wapinzani wanaanza.
Hao hata wazifunge tu maana ndo waliofanya maendeleo ya vitu! Shida ni hao wa maendeleo ya watu...
 
Hahahaaaa . good .kivuko kibovu Sasa kitakuwa kmebeba magari mabovu pia .so hayo magari bila Shaka hayahtaj kutembea barabaran yabaki kwenye kivuko tu
 
Kwenye video hapa chini kinaonekana kivuko ambacho kipo upande wa Mwibara. Kilitoka Ukerewe kwenda Mwibara ambapo kimemuacha ndugu Lissu akiwa Ukerewe kwenye mkutano. Yani Lissu amefika Ukerewe na kivuko kikatoka Ukerewe (Na tuliambiwa kuwa ni kibovu)

Tazama mbele ya kivuko yanaonekana magari. Magari haya ni pamoja na gari la Tundu Lissu (Prado nyeupe) na magari mengine ya msafara wa Lissu ambayo walitaka kuyavusha kwa kutumia kivuko hicho kutoka Mwibara kwenda Ukerewe. Sasa kwa kuwa waliambiwa kuwa kivuko ni kibovu, wakamua kuyaacha magari yao hapo (kama yanavyoonekana) kisha wakaenda zao Ukerewe kwa kutumia Mtumbwi.

Sasa ajabu kivuko kimetoka Ukerewe kimefika Mwibara hatimaye wameshindwa kushusha mizigo na mabasi waliyopaki ndani ya kivuko kwa kuwa magari ya msafara wa Lissu yaliachwa hapo na madereva wote wameenda Ukerewe pamoja na Lissu (Yame block njia).Sasa wanalazimika kusubiri hadi atoke Ukerewe ndipo waje watoe hayo magari ili kivuko kiweze kushusha mizigo na hayo mabasi.

Angalizo: Tundu Lissu aliambiwa kuwa kivuko ni kibovu na kwa leo kisingefanya kazi kabisa!

Swali, hapo nani kacheza kitoto?
View attachment 1599922
Walishaambiwa kuwa Lisu ni mbeba maono.
Kwa mini wanashindwa kusoma alama za nyakati
 
Kwanini Lisdu afunge njia?? Haoni kuwa anawakwamisha watu! Inawezekana kweli kivuko kilikuwa kibovu lakini kimetengamaa baada ya kutengenezwa
Kivuko si kilikuwa kibovu bro wakayaacha tu waliambiwa hakiponi leo
 
Hivi unajua Lissu anagombea Urais na anataka awe Rais wa Jamhuri. Hiki alichofanya ni ujinga na amethibitisha Hana Busara hata kidogo. Sasa hapo amemkomoa nani Kama siyo hao Wananchi ambao anataka wampigie kura awaongoze
Aliambiwa kivuko leo hakitokuwepo
 
Na hao watu wakiamua wawe Kama yeye unajua Nini kitatokea kwenye hayo Magari.Halafu eti huyu ndiye anaomba awe Rais, wakati vitu vidogo Kama hivi anashindwa kuonyesha uvumilivu wake na Busara zake.
Busara ipi kivuko kibovu hakitokuwepo week
 
Kwa mawazo yangu,naona kama timu ya Lissu imekosea. Mwisho wa siku atakayepata tatizo si Magufuli wala CCM ni wananchi watumiaji wa hicho kivuko. Nakiri kafanyiwa roho mbaya tu ila sidhani kama anapaswa kuwa sehemu ya mkwamo kwa wananchi wengine. Mwisho wa cku kura yangu ATL kura yangu anayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliambiwa leo kivuko hamna hakifanyi kazi.
 
Ni kulipia cost of loss wasipolipa magari yatashikiliwa hadi walipe au yatapigwa mnada na madalali wa mahakama.

Ila gharama watatakiwa kulipa si kwa wamiliki kivuko tu Bali na wenye magari binafsi waliokuwa blocked

Ofisi ya dereva yeyote ni kwenye gari hao madereva wa Lisu waliondokaje na kuachia ofisi zao au magari yao kwa kivuko? Wenye kivuko andaeni invoice haraka wakija tu hapo loss yote walipe na wenye magari binafsi blocked daini fidia
Walimwambia hakuna kivuko siku mbili.cost gani alipe?
 
Ni jambo la kipuuzi sana hili, wapinzani wanajiona wao ndo wenye nchi hii peke yao. Kwani kivuko kuwa kibovu ina maana hakitatengenezwa ili kipone na kiendelee na shughuli za kijamii. Mambo mengine sijui wapinzani wanafikiria kwa kutumia nini?
Guarantee ya siku 2 aliambiwa
 
Hivi unajua Lissu anagombea Urais na anataka awe Rais wa Jamhuri. Hiki alichofanya ni ujinga na amethibitisha Hana Busara hata kidogo. Sasa hapo amemkomoa nani Kama siyo hao Wananchi ambao anataka wampigie kura awaongoze
Waliokomesha wananchi ni hao ambao walisema kivuko ni kibovu
 
Back
Top Bottom