TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

Mimi siamini kama ubatizo wa maji ndio wokovu kwani ingekuwa hivyo wote walio batizwa wangeokoka ref. Yuda iskariote ni mmoja wao waliobatizwa.
Ubatizi wa maji ni dhamira safi kwa watu kwamba umemwamini Kristo ila sii uthibitisho maana Kristo mwenyewe ndie humpa/batiza mwaminiyo kama uthibitisho wa kuikubali imani yake.
Wala hili la kuongoza mtu sala ya toba kwa kumkaririsha kurudia kile unachomwambia sii la kimaandiko. Hakuna mahali mitume wala wanafunzi wa Yesu mwanzoni walipowahi kufanya hivyo zaidi ya kwamba walilihubiri neno na wale waliolisikia wakaliamini walibatizwa.

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
HUna mpya wewe tumeshakudharau na kukupuuza humu. Tunajua u mganga na umejificha kwenye logic na rhyotorics zako. Unatupotosha.
Zimekusumbua kiasi umejaribu kuzipinga bila kuonesha makosa yake.

Zako zimekufa zaidi.
 
Mmesema Vyema; Hoja ya kubatizwa msingi wake ni ishara ya kuzika utu wa kale (Wa dhambi) na kuvaa Utu upya!

Na hapo ndipo hoja ya Yohana inanzia, kwamba yeye ubatizo wake huashiria toba (machoni pa watu) si rohoni, lakini kwa Yesu Kristo ni zaidi!

Tendo hili huanza ndani (rohoni) kisha nje kama ushuhuda, ndio maana JC unasema si tendo la wokovu!

Nataka kumanisha pia, Ubatizo ni Muhim sababu ni ishara ya kukubali mauti ya Kristo/kufa na kufufuka kutoka dhambini lakini si tendo la wokovu/kuokolewa.





 
HUna mpya wewe tumeshakudharau na kukupuuza humu. Tunajua u mganga na umejificha kwenye logic na rhyotorics zako. Unatupotosha.
Umenidharau na kunipuuza wakati huwezi hata kujizuia usinijibu?

Sina mpya wakati zangu za zamani umeshindwa kuzijibu, mpya nikupe za nini wakati za zamani huziwezi?
 
Natumai mkuu hukushangaa maneno ya Mwenyekiti.

Maandishi yaliyopo kwenye Biblia yanatanabaisha kwamba mafarisayo (PhD holders wa Old Testament) hawakumkubali Yesu. Sababu ni zile zile za kumpinga TB Joshua kwamba hakuwa na Baba mlezi wa kiroho aliyemtambulisha kiimani.

Tukibaki kwenye suala la Imani, wakongwe wa Imani (mafarisayo) wanapenda kuona yeyote anayeimba Bible mlezi wake wa Imani anajulikana. Kinyume chake lazima wampe jina baya ikiwezekana watamsulubisha.

Ikitokea Leo hii mkuu umepata nuru ya Mungu, "mafarisayo" watakupinga sanaaa
 
LAKIni mkuu hoja za mafarisayo kama zina mashiko kwa mbaali.

Hata Yesu bin Mariam alisema tuyafuate maneno ya mafarisayo ila tusienende ktk matendo yao
 
Ukipata muda naomba umchunguze na baba askofu Gwajima Kama amempokea yesu na kubatizwa ili nijue sadaka yangu jumapil naipeleka kwake au nitombeee tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mkristo yeyote asiyekubali ubatizo lazima uwe na mashaka naye.
Ubatizo ni kiapo
 
Hizi dini uongo mtupu mwanzo mwisho.

Hakuna hata mmoja anayeweza kuthibitisha huyo Mungu yupo.
Wejamaa wewe iko siku jibu litapatikana humu jf, jiandae na ugonjwa wa sonona.
 
Wejamaa wewe iko siku jibu litapatikana humu jf, jiandae na ugonjwa wa sonona.
Siku gani, hebu taja tarehe turudi hapa kuhakiki.

Unaelewa hata kuwepo kwa ugonjwa unaousema kunathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?
 
Maneno ya kuambiwa 😂😂
 
Ni kweli. Wamefanya vizuri kumkataa. Hakuwa mkristo bali tapeli aliyetumia ukristo kama bidhaa ya kutengezea utajri tokana na ujinga wa waafrika wengi wanaondelea kuamini kwenye miujiza badala ya kutumia akili kutatua akili zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…