Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni vizur pia mkawa mnajiunga na BBC ile SAA 3 usku kulko kuleta mavipind ya ziara za katbu wa ccm au katbu mwenez ,yaan kuna cku nataman niipusue hii TV kwa mavipind yenu ,afu mbaya zaid no dstv hivyo ITV ,channel ten ,star sion kabsa ,yaan napita kwenye jarbu kubwa sana la kuvumilia kuangalia TBC muda wote huo..Mungu aniepushe na kutoa lugha za laanaNdugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.
AmenNi vizur pia mkawa mnajiunga na BBC ile SAA 3 usku kulko kuleta mavipind ya ziara za katbu wa ccm au katbu mwenez ,yaan kuna cku nataman niipusue hii TV kwa mavipind yenu ,afu mbaya zaid no dstv hivyo ITV ,channel ten ,star sion kabsa ,yaan napita kwenye jarbu kubwa sana la kuvumilia kuangalia TBC muda wote huo..Mungu aniepushe na kutoa lugha za laana
anza kwa kufuta ule ujinga awavumi lakin wamo..
ndo ntajua mnaskilza af niwashauli kukwepa u-kada
Nadhani umepotoka ndugu yangu,kati ya stesheni zenye vipindi vya kufundisha katika Taifa hili,Tbc wanaongoza kwa kuwa na vipindi vya ubunifu wa hali ya juu,hongereni sana Tbc.Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
Mkuu mbona wakati wa Tido TBC ilibadilika sana Ikaanza kupendwa...Alivyoondoka imerudi kulekule ilipotoka.Asanteni sana kwa mnaoendelea kutoa ushauri elekezi wa nini kifanyike..
Ambao bado mpo kwenye upande wa lawama bila kushauri cha kufanya niwaombe mjielekeze kwenye kutoa mawazo ya kujenga ili tupate matokeo tunayoyatamani.
Ni matumaini yangu uongozi wa TBC utapita hapa kuyachukua na kuyafanyia kazi.
Shukrani.