Travic unaangukia kwenye mtego ule ule wa kukataa maoni ya wananchi ambayo yapo kinyume na matarajio yako
Kumbuka hapa ni JF wadau wanaongea openly. Na anayekwambia ukweli anakupenda.
Ushauri mkubwa umetolewa katika nyanja kuu kama tatu hivi.
Moja, kuweni fair/impartial. Mnafahamu maana yake. Kama ni TV ya umma na ionekane hivyo. Hilo wamelisema na ndio kubwa sana.
Pili, boresheni ubora wa vipindi pamoja na ubora wa picha. Wadau wametoa mifano tatizo lilipo (aina ya vipindi) na vipi viongezwe. Wengine wamesuggest aina ya quality ya picha. Hadi wengine wamejitolea kuja kuwasaidia upande wa graphics.
Tatu, wadau wameshauri kuwa na channel zaidi ili kuaccommodate mahitaji ya vijana watoto wazee wapenda michezo nk lakini pia muonekano wa kimataifa wa TV yetu! Tunaweza kiwa na channel ta habari tu (TBC news) kisha nyingine ya mambo ya kawaida (documentaries-wildlife, elimu, ziara za tunatekeleza, this week in perspective, shuleni/watoto, science and engineering) halafu TBC Sport/music/emtertainmenr ( mpira wa nje na ndani tafuteni haki za kuonyesha japo mara moja moja, mieleka, muziki kwa sana wa vizazi vyote, bongo/nigerian movies, mambo kama hivyo kwa mpangilio maalumu).
Kutekeleza hayo ni dhahiri mnahitaji revamp ya hali ya juu, kuanzia staff training/upgrading, vifaaa, ubunifu nk.
Hamu yangu ni kuona kuwa mtanzania anaweza kuyapata haya yote in one package yaani TV station ya taifa ambayo kwa uchungu analipa kodi kuiwezesha. Lakini pia mtaweza kujiendesha na hata kutoa dividend kwa serikali kama mtatekeleza ushauri wa wadau humu.
Nawatakia utekelezaji mwema.