TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Pia ajirini watangazaji warembo wanaovutia jifunzeni hata kwa citizen TV watangazaji wao walivo. Tatizo TBC mna mazoea mno. Ikiwezekana TBC iajiri CEO kutoka nje ya nchi mwenye uzoefu wa mambo ya habari.

Na hao kina grace kingalame kwanini wasipumzike kutangaza yani mvuto zero kabisa
Nakazia hilo la kuajiri mkurugenzi toka nje ya nchi, japo najua waTz hawatakuelewa wasivyopenda watu wa nje. Wanasahau hatuko kisiwani.
 
Acheni siasa tena zile za upande mmoja. TV station imepoteza mvuto kwasababu ya kukosa ubunifu na kuegemea katika kampeni za chini kwa chini na ziara za kuzindua visima.
Taarifa yenu ya habari haina mvuto,taarifa nzima ni utekelezaji wa ilani ya chama fulani.
Vipindi vinginevyo,navyo havina mvuto hata hamasa ya kutazama. Kila wakati ni "Miaka mitano ya Mkulu",mara "Kutoka Maktaba ya Chama ChaChaMa".

Yani TV station iko kama jukwaa la siasa. Shame on you'.
 
Utangazaji ni kipaji na sio mavyeti tu..hawashangai clouds media wanaendelea kuwa relevant kwa kiasi fulani kutokana na kuweka watu wenye vipaji na sio tu degree ya mass communication na journalism..

Sehemu ukichajazaa wazee wengi hata ubunifu unakuwa hamna..refer taasisi nyingi za serikali kama Ttcl na nyingine..
Jiwe gizani kwa JONIII
 
Umeongea point lkn CEO awe mtanzania sema sasa iv teknolojia inabadilika sana ivo hao TBC ina wazee ambao hawawez kwendana na kasi ya teknolojia ivo wa ajiri vijana bana ambao wanaenda na wakati na kasi ya teknolojia
CEO wakitanzania aliyewezea alikuwa Tindo Mhando, tukisema tuweke mtanzania asiye mzoefu vingine tuangalie performance haiwezekani TBC inapewa support na serikali lakini inafanya hovyo huo ka si ufisadi nini.

TBC wazee hawabadiliki ka enzi za Nyerere rangi mbaya, watangazaji wa kike mvuto zero wabonge sana hata poda tu hawapaki kwa kweli ni aibu kubwa. Background ya studio yenyewe hovyo, mheshimiwa Raisi aingalie TBC kwa jicho la tatu.

Hivi.hawawezi hata kujifunza kwa media zilizoendelea hata kuajiri expert mzoefu ili awape mawazo mubadala, vtu vingi vya serikali hujifia tu vile hamna ubunifu bora liende.

Hata Mkurugenzi alipewa hyo nafasi na Raisi naona anamuangusha mheshimiwa licha ya kuwa msomi. TBC inahtaji mabadiliko makubwa tusililie uzawa wakati utendaji wao ni zero ajirini expert wazoefu hata wa nje ya nchi
 
Acheni siasa tena zile za upande mmoja. TV station imepoteza mvuto kwasababu ya kukosa ubunifu na kuegemea katika kampeni za chini kwa chini na ziara za kuzindua visima.
Taarifa yenu ya habari haina mvuto,taarifa nzima ni utekelezaji wa ilani ya chama fulani.
Vipindi vinginevyo,navyo havina mvuto hata hamasa ya kutazama. Kila wakati ni "Miaka mitano ya Mkulu",mara "Kutoka Maktaba ya Chama ChaChaMa".

Yani TV station iko kama jukwaa la siasa. Shame on you'.
Umesahau na ile kuonyesha bombadia kila saa na kuhamia Dodoma, TBC mumezidi kwa kweli
 
Nakazia hilo la kuajiri mkurugenzi toka nje ya nchi, japo najua waTz hawatakuelewa wasivyopenda watu wa nje. Wanasahau hatuko kisiwani.
Kuleta watu wa nje ni wazoefu pia kuleta mawazo mapya ya ubunifu, watafte watu wa kubuni vipindi ikiwezekana watoe ka shindano la watu kubuni vipindi vyenye maudhui kuanzia kila sector inayoendana na wakati. Kuajiri watu hata wa nje au ushirikiano ni kujifunza vtu vipya na kuboresha.
 
Ushauri wa maana tena wa bure kabisa.
 
Umesahau na ile kuonyesha bombadia kila saa na kuhamia Dodoma, TBC mumezidi kwa kweli
Uko sahihi mkuu,ni jambo la kushangaza hili!
TV station mwaka mzima inaonesha Bombardier!.
Nawashauri watafute Watangazaji/Wafanyakazi wenye weledi na ubunifu, vinginevyo TBC itabaki kuwa hivyo hivyo ilivyo kwa sasa.
 
Tunataka muonekano angavu sio wavumbivumbi, pia navipind view vya kisasa zaidi
 
TBC hata mkipewa CNN muiendeshe ndani ya wiki 2 tu itakuwa haina watamazaji.

Muulizeni Tido Mhando alikuwa akifanyaje? Ondoeni upupu wenu humu.
emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu umemaliza
 
Uko sahihi mkuu,ni jambo la kushangaza hili!
TV station mwaka mzima inaonesha Bombardier!.
Nawashauri watafute Watangazaji/Wafanyakazi wenye weledi na ubunifu, vinginevyo TBC itabaki kuwa hivyo hivyo ilivyo kwa sasa.
Kama hawataki kubadilika wasichezee kodi zetu bure kwa vipindi hewa, pia nimemshangaa Sam mahela kaenda kule naye kafubaa weledi wote umekwisha au ni zile rangi za ajabu za hyo TV.
 
Tatizo la tbc ni uchama zaidi, viongozi wake hawajiongezi vipindi vya kipuuzi vingi sana. Polepole na mkuu kila saa.
Badilisheni, michezo, wnyama utafiti sayansi na komedi kidogo
 
Binafsi sina ugomvi na vipindi vingi vya TBC naona viko poa na vimenifanya nielewe mambo mengi ambayo serikali inafanya na hili ndo hasa tv ya taifa iinapaswa kufanya. Mfano wa vipindi nhivyo ni Tunatekeleza, na ziara za viongozi sehemu mbalimbali kiukweli nawapongeza maana nimeijua hii nchi jinsi ilivyo kiasi flani kupitia ziara zinazorushwa mubashara na TBC.

Tatizo la TBC ni colour yao sio nzuri kabisa na sauti pia. Kuhusu watangazaji naona wako poa ila namkubali sana Mwanadada Flourence Mahundi hichi kichwa kipo serious sana na anajua kuitendea haki sauti yake ya kipekee kabisa japo siku hizi simuoni sana.
 
Kuwa mstaarabu, wape uhuru wachangiaji, naona unaleta ukada! Najua huna mamlaka wala nguvu ya kuyafanyia kazi maoni na mapendekezo ya wananchi na wala hakuna kiongozi/mfanyakazi yeyote wa TBC mwenye uwezo wa kufanya hivyo so tulia, waache wachangiaji watapike nyongo zao maana palipo na kero ndipo maoni hutolewa. Kifupi: TBC ni ufujaji wa kodi za Watanzania, haikupaswa kuwepo maana hata viongozi wa juu kabisa wamethibitisha kutoiangalia!
Mkuu. Maswali yako yote sijaona lenye tija kulijibu. Niwie radhi.
 
Back
Top Bottom