TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.

Mkuu huu ushauri wako kwa TBC1 ni kama vile ama unapaka rangi Upepo au unaogelea katika Lami au unandika namba Sifuri katika Ndoo ya Maji.
 
Nimepitia maoni. Nasikitika kwamba bado wengi mmejikita kwenye kulalamika zaidi badala ya kupendekeza angalau program ideas ili kulimaliza tatizo.

Nyuzi za malalamiko zipo nyingi sana na tayari yanafahamika. So nasisitiza tujielekeze zaidi kwenye mapendekezo kuhusu kinachotakiwa kufanywa huku tukitoa ideas ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.

TBC ni mali yetu sote. Ni lazima tutoe mawazo yanayojenga ili ifanikiwe.

Naelewa tuko disappointed kwa sababu ya itikadi zetu na jinsi tunavyohisi hakuna fairness, lakini tuweke grudges pembeni na tuelekeze njia sahihi ya kupita.

Tusilalamike tu ili kuponya nafsi zetu. Tutoe constructive ideas ili kuiponya TBC yetu.
Hayo ndio maoni mkuu we soma hapo utakutana nayo mengi... USHAURI MSIFANYE KAMA TV YA CCM.. HIYI NI YA TAIFA.. WATANGAZAJI WAZEE WATOENI.. VIPINDI VYA KIPUUZI KAMA CHEREKO MARA SIJUI TAFAKURI ONDOENI MARA MOJA.. FUNGUENI CHANNEL ZINGINE KWA AJILI YA MAMBO YA MICHEZO
ANGALAU MUWE NA INTERNATIONAL FORUM KIDOGO..
PICHA NI MBOVU SANA BADILISHENI HIYO ISHU..
ONDOENI KABISA VIPINDI VYA KUMTUKUZA MAGUFULI.. YY NI MTU NA SI MUNGU SOMEWHERE, ANYTIME ATAKUFA TU NA TBC ITABAKIA..
ANGALIENI WATANGAZAJI VIJANA.. HAO WANYAKYUSA WA MBOZI WANGEBAKIA KWENYE RADIO TU..
 
Tuachane na kwenye siasa kidogo. Hayo yameshasikika vya kutosha sasa naamini yatafanyiwa kazi.

Hakuna mawazo mbadala nje ya hayo ya kisiasa ambayo TBC wanatakiwa kuyafanyia kazi?

Jina nalo ni tatizo? Unashauri iitwe jina gani?

Karibu.
Natamani kuchangia bt moyo unasita musije mukaniteka.
 
Asante kwa maoni mkuu
 
Ushauri ninao utoa naamini utabadili mtizamo hasi ambao baadhi ya Watazamaji wanao juu ya TBC na Watazamaji hawa na wengine wengi wataanza na kuendelea kuingalia TBC kama TBC itauzingatia ushauri wangu kwa 100%:

1. TBC iboreshe ubora wa picha zake- nashauri matangazo yote yarushwe kwenye HD/UHD/4K kwa kuwa Watazamaji wengi wa Tv kwa sasa wanamiliki tv au wanaangalia vipindi vya Tv kwenye TV zenye uwezo wa kuonyesha picha kwenye mifumo hiyo.Baadhi ya watazamaji hawapendelei kuangalia TBC kwa kuwa ubora wake wa picha hauridhishi hasa kwa wale watazamaji wanaojari ubora wa picha kwenye Tv na wenye Tv za kisasa(Flat screen TV or Curved screen TVs with larger screens).

2. Mwonekano wenye mvuto iwe ni mojawapo ya kigezo muhimu cha kumuajiri Mtangazaji.

3. Vipindi viandaliwe kwa kuzingatia mahitaji ya habari kwenye jamii na siyo ya TBC.

4. TBC iwe na “results oriented technical and Management team”.Results= Watazamaji wengi wa kudumu wasioweza kuhama kirahisi na kuteka wengine wapya.

Naomba kuwasilisha,

Article.
Ushauri mzuri mkuu. Ingawa hujataja mambo specifics lakini ni bora zaidi kuliko ungelalamika.
 
Kuna upya gan mbona nme tune bado picha za kupauka tu
 
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.

Fufueni akili zenu kwanza kabla ya kufufua TBC. Wafu wa akili.
 
Watu wameombwa maoni, lakini wao wanatoa kero, Alafu mtake CCM itoke madarakani
Nilidhani labda sikueleweka vizuri. Watu kuendelea kutoa kero badala ya ushauri wa cha kufanya inasababisha tunabaki pale pale kwenye tatizo.

Naamini watatoa tu maoni na mapendekezo. Ni suala la kueleweshana taratibu tu.
 
Ushauri mzuri mkuu. Ingawa hujataja mambo specifics lakini ni bora zaidi kuliko ungelalamika.
Kabla ya kutoa ushauri wangu nijibu kwanza hya.
1.umechukua dhamana ya kuuleta huu uzi ukiwa kama nani hasa, kwenye maelezo sijaona.

2.TBC ni television ya CCM au ni television ya taifa.

3.Malalamiko yoooote kuhusu tbc kwenye reply yko unasema unayafahamu, je wewe kama mdau mmoja wapo umetumia nafasi yko vipi kuishauri tbc administration and board of directors.

Note:huwezi ukaomba ushauri wa maboresho ya vipindi kabla hujatatua chanzo cha malalamiko na kuyapatia ufumbuzi. Ni kazi bure.
 
Mkuu. Maswali yako yote sijaona lenye tija kulijibu. Niwie radhi.
 
Lazima TBC wabadilike na wakitaka kwenda mbele waombe ushauri kwa Mzee Tido hakuna jingine jipya.
 
Tuachane na kwenye siasa kidogo. Hayo yameshasikika vya kutosha sasa naamini yatafanyiwa kazi.

Hakuna mawazo mbadala nje ya hayo ya kisiasa ambayo TBC wanatakiwa kuyafanyia kazi?

Jina nalo ni tatizo? Unashauri iitwe jina gani?

Karibu.
Hapo kwenye siasa mkuu ndiyo pamebeba mengi sana. Mkijikwamua hapo mengine ni rahisi yatakuja hatua kwa hatua. Ukishafungwa na siasa huwezi kuwa na uwezo wa kufikiri mengine. Huoni kila unapopewa USHAURI hapa, ukigusa tu kaeneo hako unapata shida!!?? Ni kwa sababu mizizi imejikita huko. Ng'oeni hiyo mizizi muwe huru mtaweza kusikiliza ushauri na ubunifu utakuja tu mkuu.
 
Tatizo lenu la ukada ndilo linaloiua hata star tv kwa sasa, hakuna sumu mbaya kwenye biashara ya umma kama kuweka mlengo wako. Kabla ya awamu hii ya 5 star tv ilikuwa vizuri sana hasa upande wa mijadala, walikuwa wanachambua mambo kwa undani hasa, lakini kwa sasa wamekwisha yote ni sababu wanataka kufurahisha wakubwa, matokeo hata mishahara wanashindwa kulipa.

TBC ni televisheni ya taifa, mnatakiwa kutangaza kila kitu kinachofaa kuwa habari, maana hata msipotangaza nyie wengine watatangaza na ndio wataendelea kufuatliwa. Tumefika mahali mtu ukiangalia tv pendwa ukiona hakuna kinachokufurahisha kwa wakati huo unaamia channel za nje, tunasahau kama kuna channel ya TBC
 
Unajua kuna kipindi watawala wanafikiri wanaweza kuwachagulia wananchi nini cha kutazamwa au kusikilizwa.Lakini katika zama hizi za utandawazi ni vigumu sana kuwalisha watu chakula wanachotaka wao.

Mwl Nyerere aliweza kwakuwa zama zake dunia ilikuwa katika giza lakini leo ukiona kiongozi kutwa nzima anataka kutukuzwa na kusifiwa tena kwa kutumia TV ya taifa unabaki mdomo wazi.
 
Ushauri ninao utoa naamini utabadili mtizamo hasi ambao baadhi ya Watazamaji wanao juu ya TBC na Watazamaji hawa na wengine wengi wataanza na kuendelea kuingalia TBC kama TBC itauzingatia ushauri wangu kwa 100%:

1. TBC iboreshe ubora wa picha zake- nashauri matangazo yote yarushwe kwenye HD/UHD/4K kwa kuwa Watazamaji wengi wa Tv kwa sasa wanamiliki tv au wanaangalia vipindi vya Tv kwenye TV zenye uwezo wa kuonyesha picha kwenye mifumo hiyo.Baadhi ya watazamaji hawapendelei kuangalia TBC kwa kuwa ubora wake wa picha hauridhishi hasa kwa wale watazamaji wanaojari ubora wa picha kwenye Tv na wenye Tv za kisasa(Flat screen TV or Curved screen TVs with larger screens).

2. Mwonekano wenye mvuto iwe ni mojawapo ya kigezo muhimu cha kumuajiri Mtangazaji.

3. Vipindi viandaliwe kwa kuzingatia mahitaji ya habari kwenye jamii na siyo ya TBC.

4. TBC iwe na “results oriented technical and Management team”.Results= Watazamaji wengi wa kudumu wasioweza kuhama kirahisi na kuteka wengine wapya.

Naomba kuwasilisha,

Article.
Nina Tv curved tv Uhd 8k na nvidia shield andtoid Tv na ukiangalia quality ya picha duniani sasa hivi wakati tv zetu ha hd hawamo.
Ukiserch hd quality programs hupati cha kwetu, je uhd? Je 4k? Na sasa watu wainaitafuta 16uhd quality.
Masikini tbc
 
Ushauri ninao utoa naamini utabadili mtizamo hasi ambao baadhi ya Watazamaji wanao juu ya TBC na Watazamaji hawa na wengine wengi wataanza na kuendelea kuingalia TBC kama TBC itauzingatia ushauri wangu kwa 100%:

1. TBC iboreshe ubora wa picha zake- nashauri matangazo yote yarushwe kwenye HD/UHD/4K kwa kuwa Watazamaji wengi wa Tv kwa sasa wanamiliki tv au wanaangalia vipindi vya Tv kwenye TV zenye uwezo wa kuonyesha picha kwenye mifumo hiyo.Baadhi ya watazamaji hawapendelei kuangalia TBC kwa kuwa ubora wake wa picha hauridhishi hasa kwa wale watazamaji wanaojari ubora wa picha kwenye Tv na wenye Tv za kisasa(Flat screen TV or Curved screen TVs with larger screens).

2. Mwonekano wenye mvuto iwe ni mojawapo ya kigezo muhimu cha kumuajiri Mtangazaji.

3. Vipindi viandaliwe kwa kuzingatia mahitaji ya habari kwenye jamii na siyo ya TBC.

4. TBC iwe na “results oriented technical and Management team”.Results= Watazamaji wengi wa kudumu wasioweza kuhama kirahisi na kuteka wengine wapya.

Naomba kuwasilisha,

Article.
Natamani kuchangia bt moyo unasita musije mukaniteka.
Usiogope mkuu utarudishwa salama [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom