TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)


Asante mkuu. Angalau wewe umetoa ushauri elekezi kuanzia namba 3 na kuendelea. Hiki ndicho nilichokilenga. Tutaje ideas kama hivyo. Asante.
 

Asante kwa maoni. Namba 2, 4 na 5 ni mawazo elekezi. Hayo mengine ni malalamiko na kejeli ambazo nashauri tujaribu kuziepuka kwa sababu zinaficha ushauri.
 

Natamani wachangiaji wote tungeenda hivi. Huku ndiko kuelekeza cha kufanya. Unatoa ushauri ambao unajadilika na unaweza kufanyika.

Kuna watu humu wana mawazo mazuri ila wanashindwa kuyatoa na kuishia kulalamika sijui kwanini.

Tujitahidi kutaja suluhu wakuu. Kama una ideas ambazo unaona ni workable, zitaje tu. Huenda ukaikuta imefanyiwa kazi.
 

Sahihi kabisa. Asante kwa kujazia maarifa. Napenda kama wadau tuchukue hatua kwa kutoa mapendekezo na tusikubali kukwama kwenye malalamiko tu.
 
3. Mechi za Team ya taifa anzeni kuonyesha hyo ruzuku mnayopewa kaz yake nn unganeni hata na ZBC 2
4. Wekeni vipind vinavyoendana na dunia ya sasa sio kla siku vipind vya wazee tu unategemea nan ataangalia

3. Safi
4. Unaweza kutaja mifano? Pendekeza mfano wa kipindi mkuu.
 
Ongezeni ubora wa picha
Watangazaji wamezubaa pia badilisheni kuweni kama media nyingine nunueni vipaji toka station nyingine kama alivyofanya efm au clouds
Wekeni siasa pembeni na mfocus kwa wananchi kero na maoni yao
 
CEO: Naomba ushauri.

Mshauri: Punguza ukada.

CEO: Huo siyo ushauri, ni kulalamika.

Ushauri ni ushauri. Hata mtu akisema neno TBC lihamishwe litoke upande huu kwenda ule ndiyo ushauri wenyewe huo.

Mpaka sasa inaonyesha hiko kitu ndicho kinawakera na kuwapotezea viewers wengi. Mi ninachojua hata kama umeamua kusifia CCM kuna namna unaweza kuifanya hata watu wakapenda.

Tatizo ni wazee walioshikilia siti. Tugeeni kijiti vijana
 
Siku TBC watakapoweza kutofautisha kati ya Chama(CCM) na Serikali, naamini safari ya mabadiliko ya kweli itakuwa imeanza.
 
Constructive [emoji106]
 
Kuna yule mzee wa tafakuri, yeye kwenye kila tafakuri lazima amtaje mzalendo no.1 kwani amsipomtaja atafukuzwa kazi? Acheni kujipendekeza kupita kiasi.
 
Labda tupate uzoefu wa watu kama BBC, najua hatuwezi kuwa kama wao by 100%, but we can emulate a few things from them.

Kuna BBC One- Hii ni flagship channel
BBC Two- Kwa ajili ya habari za michezo na current affairs.
BBC Four Kwa ajili ya serious issues na documentary
BBC News- Habari zinazotokea na live coverage.
Zipo za bunge, international affairs, lugha zingine, watoto, art, nk. Wamegusa almost kila kitu.

Sisi muhimu ni Habari, Michezo, Home affairs, International affairs, Arts, Utalii, Watoto nk

Ubora wa mitambo ni kitu muhimu.

Go for talented, presentable and charming news anchors, tafuteni talents kama ambavyo mnaangalia vyeti.
 

Umeeleza vizuri sana mkuu pamoja na kushauri. Wewe ni miongoni mwa mlioelewa lengo la Uzi huu.

Asante kwa kutoa ushauri constructive..
 
Hivi orijino komedi bado ipo? Naombeni majibu leo nataka niangalie TBC baada ya kuiblock kwa miaka tisa.
 
Anzeni na kubadilisha mwonekano wenu kwanza..
 
Ushauri tu.
1. Ongezeni channel nyingine ziendane na hali halisi ya sasa. Nazi ziwe free ving'amuzi vyote.
2. TAARIFA ya habari ni muhimu sana. Mnapogusia,Siasa mubalance mambo, hapo ndipo mwaharibu kabisaaa, ndipo wengi mnapowakera watazamaji. Mnaegemea sana Chama tawala yaani HD mnaboa. Hadi aliyekuwa kwenye tukio hushangaa. Leteni wale wazungumzaji kwenye jambo muhimu wafafanue.
 
Subiri kidogo msemaji wa tBc, nikaangalie kwanza hiyo runinga ya taifa, ntakuja kutoa shauri, sikuwa na taarifa kama bado mpo hewani
 
1. Onyesheni bunge mubashara, kama mnaweza kuonyesha na kufuatlia ziara za rais wetu mubashara basi naamini hata bunge mubashara inawezekana.
2. Boresheni ubora wa picha zenu.
3. Kuweni "fair" kama mnaweza onyesha harakati/habari za CCM onyesheni basi na upinzani.
4. Binafsi sifurahishwi na kipindi cha chereko na kile kinachoonyesha kumbukumbu za vifo vya watu jina lake limenitoka.


Vipindi vyenu vingi vinajenga ukiacha hayo mapungufu yenu, kuna watu wametoa ushauri mpunguze vipindi vya kizee na kuongeza vya vijana ili hali hawajataja vipindi vya kizee ni vipi hivyo na vya vijana ni vipi. Wasiwasi wangu ni kuwa hivyo vipindi vya vijana wanavyovitaka ni muziki yaani bongoflava sijui naija/hiphop/kwaito n.k kama "channels" nyingi za kisasa zinavyofanya. Mimi nashauri hivi kuliko kuonyesha muziki usiokuwa na maadili ni heri tuendelee na hivyo vipindi wanavyoviita wao vya kizee.
Ni hayo tu.


Ficus
 
Bibi mzee hata ukimpaka wanja hapendezi, nimeangalia zaidi ya mara tatu sijaona mabadiliko yoyote. TBC tayari haina jipya, mkitaka kufufuka badilisheni mitizamo yenu, TBC ni televisheni ya taifa, lakini ipo chini ya chama kwa sasa. Matukio mengi ya wananchi wanayohitaji kuyaona hamuonyeshi, nyie ni vipindi vya ziara tu za viongozi wa CCM. Wapeni wananchi habari wanazozitaka hata kama nyie mnazichukia.

Hata hao wanasiasa mnaowatumia hawawaangalii, na ndio maana kila wakati simu zinapigwa clouds, mjue wengi hawana habari na nyie.

Rudi kwenye tamasha la URITHI WETU, clouds ndio ilicover kwa zaidi ya 80%, na ni tamasha la TAIFA, hamjajua tu ni kwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…