Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC
TBC1 stop hypocrisy! tatizo mnalijua mnakaa kujadili upuuzi! Huyo PhD hopeless kabisa, hajui kwa nini mko hivyo. Ametoka uraiani anajua fika maana uraiani kuna kila kitu , tunaambizana particularly kama hauko wa kundi la kijani, tunajadili mapungufu!
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC

Kila siku huwa tunawaambia tatizo la nchi hii kusonga mbele ni hicho chama chakavu. Kimekigeuza hicho kituo cha umma kuwa kipeperushi cha fitina, chuki dhidi ya wengine nk. Akija mtu mwenye uwezo anafanyiwa zengwe kisa hafuati huo upuuzi wa chama chakavu. Kituo kimekuwa cha kizee ile mbaya, hata watangazaji vijana wamejuwa kama wazee. Sasa hao jamaa wa chama chakavu wamegundua hicho kituo kinaangalia na wale mtaji wao wa kura huko vijijini na hakina mvuto wameamua kufagilia vituo vya kileo. Kwa maneno marahisi wamekitumia hicho kituo kama kondomu saa hii wanachekea kwenye shuka.
 
Sidhani kama TBC wana kipindi hata kimoja kinachovututia.
 
Tbc hawanaga jipya kila cku ni sisiem, Mbaya zaid mnanenepeana kwa kula kodi zetu
 
Watanzania wanapenda mambo ya ovyo ovyo na yenye kusisimua hisia zao.TBC ni chombo cha umma lazima kiwe na maadili ya kutoa taarifa lakini zaidi lazima itoe elimu kwa umma,sio miziki na mambo ya ovyo ndio muone inawafaa.
 
TBC Wakita Wafanyakiwe:
a)Wapunguze Ukada,wawe kama BBC,mambo yakitaifa yawe na kipaumbele!na wafanye coverage ya vyama vyote kwa usawa!
b)Wapunguze "Uzee" na Wakumbatie "Ujana"!Vipindi vyao haviwavutii vijana kutokana na maudhui ya vipindi!
c)Wapunguze kuweka miziki ya kizamani,unakuta toka asubuhi mpaka jioni wanapiga nyimbo za Bongofleva za miaka ya 2005 kushuka chini,mbaya zaidi nyimbo zenyewe mbayaa!
e)Waboreshe Rangi ya vipindi vyao,tena hapa wanakera sana!

Mkuu umenena vyema kabisa pamoja na kuwakosoa pia tuwape ushauri kama ulivyo pendekeza!
a). Waamue ama waweke coverage ya vyama vyote ama wasiweke kabisa! Wanaweza kuweka mambo ya Coverage kenye Channel maalum, ili impe mtazamaji option ya kwenda huko au kuacha!
-Kuwa Biased ni tatizo sana kwa TBC na vyombo vyote vya habari vya serikali, na hii inapelekea kutouza bidhaa zao kabisa.

b). Kuhusu uzee hapo pia tatzo lipo, wanaweza watengea wazee wao vipindi kadhaa kwa siku ama kwa wiki, halafu wakaribishe na damu changa wanaojua wasikilizaji/ watazamaji wanataka nini. Vinginevyo watajiangalia na kujisikiliza weneyewe! Watu wa sasa wanataka "uhalisia" sio "kuhariri" jambo ambalo lipo WAZI kabisa ili kumfurahisha fulani tu!

c). Kuhusu rangi nk, nafikiri wana haja ya kutafuta watalamu kutoka nje!
 
Sijajua kwanin wafanye kikao cha dharula wakati tatizo linajulikana toka muda mrefu ...?!
 
Tatizo wakubwa washaitumia sasa wanaona haifai wanaikimbia kwasabu watazamaji tumeikimbia
 
wamwombe Radhi ndugu Dastan Tido Mhando, na wamrudishe kwenye Nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu.

Kinyume na Hapo ni kujidanganya, maana Tv Hii imepoteza kabisa Ladha.
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC
Duniani kote vituo vya Taifa sio rahisi kushindana na vituo vya kibiashara, na sidhani kama hilo ndio lengo.
 
Kwani TBC nini sihifahamu haiitaji ufike darasa la 7 na kutumia mda mwingi kujadili tatizo imekua mali ya ccm msifungamane na pande yoyote hata kwenye vipindi vyenu arikeni wakina Tindu Lissu, Malim seif onyesheni mikutano ya hadhara ya wapinzani hata the comedy waliua baada ya kuja huko hawakua na uhuru wa kukosoa serikali
 
Back
Top Bottom