Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Taasisi nyingi a serikali zimekosa ubunifu au watumishi wao hawapo commited. Serikali ibadilishe ibadilishe mfumo wa ulipaji mishahara. Isiwe mtumishi analipwa tu hata kama haja-perform au kuwe na initial payment ya mshahara then tafsiri ya hili ni bonus kwa best performers.
 
Hiyo tv saa 24 ni habar za chama..wacha waangalie wao na familia zao mm hata sijuagi kama inaoperate
 
Siku hizi ukitwa na rafiki zako unaangalia taarifa ya habari ya TBC unaonekana huna akili kabisa
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC
Wamuulize Tido Mhando alifanyaje TBC ikawa na mvuto, wajilinganishe na wanachokifanya sasa then watagundua tatizo
 
Bibi yangu mwenyewe ukimuwekea tbc anakutukana
 
"Wafungulie bunge live" mambo itakuwa byeee
 
Siku Zote Kupanga Ni Kuchagua, Hivyo Acha TBC Wavune Walicho Kipanda.
 
TBC TV, TBC RADIO, sijui ni miaka mingapi sijaangalia na kusilikiza, nadhani tokea Tido Mhando aondoke ndio mara ya mwisho kuangalia, nasema kweli kabisa...

Sina imani nao kabisa, yaani kinachonijia kichwani ni waongo sana na habari zao, sbb zipo.. I never trust them, and matangazo na programme zao sio impressive kabisa kutazama.. hazivutii kabisa.. alafu chenga kibaooooooo, cracks balaaa, picha mbovuuuuuuuuuuu... Audio ndio usiseme iko ONE SIDE YA SPEAKER TU, HADI UCHUKUE REMOTE, UBADILI kila saa, ndio utapata speaker zote.. Audio button ya Remote, the una press to left, badala ya stereo ndio utapata speaker zote kuongea.. ukihamisha station, ukirudi tena unatakiwa ufanye audio settings tena, balaaa tupu.. kila kitu TBC ubora mdogo sana jamani

Watanzania wanapenda mambo ya ovyo ovyo na yenye kusisimua hisia zao.TBC ni chombo cha umma lazima kiwe na maadili ya kutoa taarifa lakini zaidi lazima itoe elimu kwa umma,sio miziki na mambo ya ovyo ndio muone inawafaa.
Maadili ya kurusha habari za ccm tu
 
Mimi nilidhan kipo kwa ajili ya kuonesha hafla za serikali tu.... Mikutano, kampeni.. [emoji5]
 
Uonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC
Bora hata wangeonyesha bunge live tungewakumbuka, waendelee kuonyesha harusi, na animal
 
Siasa ukiingiza kwenye jambo lolote inaleta shida... Na waone sasa habar inavyokua.. Na january wataweka kikao chengine
 
Back
Top Bottom