Unataka TBC ibakie na misingi yake hata kama ni ya hovyo? Iendelee na misingi yake hata hakuna mwenye hamu ya kukitazama kituo hicho?
BBC, CNN ni vituo vya TV vya kitaifa lakini vinapendwa na asilimia kubwa ya watu wote Duniani? TBC kama inataka kuwa chombo cha umma, ijifunze kutoka kwa waliofanikiwa kuliko kushikilia misingi isiyo na manufaa kwa umma.
Nini sababu ya viongozi wengi kutumia vituo vya umma kuliko TBC? Jibu ni wazi, kama unataka watu wengi wakusikie unaenda kwenye kituo kinachosikilizwa na watu wengi.
Hata ukiwa na biashara, utakuwa mjinga kama utapeleka tangazo lako la biashara kwenye gazeti la UHURU wakati unajua kuna wasomaji wachache sana wa gazeti hilo, tena wale ambao wanalazimishwa kulinunua.