TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Huyo jamaa hakustairi kuingia bungeni anafanya siasa pasipostairi kamavip waifunge kabisa iyo bajet waliokuwa wanawapa iperekwe ITV au AZAM TV
 
Sasa ajira zisizo rasmi za humu jf zipo mashakani. Kama bunge halitakuwa live vijana wengi watapotea humu jukwaani.
 
Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.
 
Frankly speaking hii TBC ni taasisi ambayo inahitaji restructuring. Inachekesha kuona TBC 2 ina airtime kuonyesha miziki almost 24 hrs kila siku. I mean, haiingii akilini mfanyakazi wa TV yuko kazini kwa pesa za taxpayers anakaa kuonyesha muziki all the time around all the week. Na wakati huo huo hata TBC 1 nayo ina airtime ya muziki. Kama hawana ubunifu wa vipindi basi ni afadhali wafunge channel moja ili kupunguza gharama za uendeshaji.
 
mmmh...TV tunayokatwa kodi kuendesha...imelemewa na gharama!tuibinafisishe tujue moja!
 
ukiona vyaelea ujue vimeundwa ndugu yangu
 
Bunge ni muhimu kufanya vikao vyake, siyo kwa kuliangalia, Wabunge wasitafute tu umaarufu kwenye kutazamwa wajikite kwenye hoja.
Duh kwahiyo kwenye kampeni watu wanataka umaarufu ndo maana wanaonyeshwa?? Tanzania tuendako ni kubaya maona udikteta huo...
 
Asilimia kubwa ya Watanzania wako vijijini na hawana TV wanaendelea na shughuli za kujitafutia maendeleo. Nyie asilimia ndogo mnaona mna haki ya kuitaka serikali ilipe ghrama kubwa ya kurusha Bunge live kwa ajili yenu tu!? Mnataka Magufuli ajaze dawa mahospitalini, ajenge barabara nareli, asomeshe bure nk nk. Akisema msiangalie Bunge kuokoa pesa ili zielekezwe kwenye hayo muhimu mnang'aka! Una hamu ya kuangalia Bunge live chukua likizo nenda bungeni kama kweli ni muhimu sana kuangalia live. Mmeambiwa litaonyeshwa saa 4 usiku! Mnashindwa nn kusuburi kuangalia ucku? Saa hizo ni nzuri za kupumzika na kuangalia TV. Watanzania bwana Magufuli kazi unayo ya kupigana na wasiopenda kazi.
 
Haiwezekani kila maamuzi Rais aombwe ushauri, inakua haina maana ya waziri kuwepo.
Acha watu wafanye wanavyoona inafaa mwisho wa siku kila mmoja ahukumiwe kwa utendaji wake, hatutaki kusikia mambo ya 'oda' kutoka juu.
 
mmmh...TV tunayokatwa kodi kuendesha...imelemewa na gharama!tuibinafisishe tujue moja!



Naangalia TBC hapa nimeona Tangazo kuwa TBC watakuwa wanaonyesha Vipindi Maalumu vya Shughuli za Raisi JPM.


Je! hivi vipindi havitumii fedha?????????!!!"
 
Kipindi cha Kampeni kilikuwa ni muhimu sana, siyo tu kwa mikutano ya CCM bali ya vyama vyote. Sasa hivi hakuna sababu ya kutumia gharama kama hakuna ulazima.
Kama bunge siyo muhimu hivyo basii lifutwe tu kusiwe na bunge nchi hii
 
Huu ni uhuni mkubwa sana. Wanaficha madudu yao wakiogopa wataonekana. Kams sababu ni gharama waruhusu tv nyingine idadi yeyote warushe live. Tv inaendeshwa kwa kodi za wananchi anasema gharama kubwa. Hizo binafsi kama azam na star tv wasemeje. Tbc si inafanya biashara kurusha harusi, hii sio haki kabisa. Ameshindwa kutoa sababu za msingi. Magufuli je atakubaliana na hili? Wananchi hatuna haki ya kuwaona tuliowachagua wakituwakilisha bungeni kama wanatutendea haki. Hata hiyo saa nne wasirushe
 
Nape anadhani cheo chake Ndani ya CCM ni bora kuliko Cheo cha Kuwa Waziri wa Jamhuri ya Muungano
Badala ya kufanya kazi kwa maslahi mapana ya nchi, anafanya kazi kwa maslahi ya CCM
Naunga mkono hoja, kwa hatua hii, nadhani Magufuli kuna haja akaingilia kati kuona kama je HII HATUA YA SERIKALI YA KUZUIA UWAZI, NA KUMINYA INFORMATION ILI WANANCHI WASIJUE YANAYOJIRI KATIKA BARAZA LAO, JE NI KWA MASLAHI MAPANA YA UMMA AU MASLAHI YA KISIASA YA WATU WACHACHE?

Pia Natoa Rai kwa Raisi kujiridhisha je Anataka kuongoza Watu mbumbumbu wasio na taarifa, au anapenda kuongoza watu wenye ufahamu wa nini serikali yao inafanya?

Katika suala la Demokrasia na Uwazi nchi hii imepiga hatua kubwa katika tawala zilizopita, Hatutegemei Serikali ya Magufuli itupeleke hatua nyuma!, WE WANT DEMOCRATIC AND TRANSPARENCY PROGRESS, NOT RECESS!
 
Alianza na MAWIO tukanyamaza
Amekuja na TBC tukinyamaza,
Atakuja JamiiForums
Hapo ndipo tutalia na kusaga meno
SAY NO CENSORSHIP
 
Halafu jpm kama mnafiki vile kumuhusisha Mungu na matendo yake tofauti kabisa mimi ndo maana huyu Mungu wa TB joshua wala simuamini.watu wamechota bil 300 tena wachache leo bil 4 kwa mwaka watanzania waone bunge ni kero. Pesa ngapi walilipana bunge la katiba na haikupatika hebu ifike Mahali waache kutucheze leo ccm ndo ya kuonea uchungu pesa ya watanzania .lake oil tu akilipa ni miaka 2 tunapata bunge.achana na twiga walioiba na sasa yupo albino olé wenu apotee tena
 
Zitto Kabwe


Hoja ya gharama ni hoja
dhaifu sana katika kuzuia
mikutano ya Bunge kurushwa
'live'. Demokrasia ni gharama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…