TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Kama serikali ina lengo na dhamira ya kweli ya kusafisha mwezi wa nchi hii kwanini wasituoneshe wabunge wetu wanavyochambua mambo bungeni na kama kuna dhamira ya kweli kwanini waogope kurusha bunge live unadhani ni woga wa kuanikwa na wabunge walioenda bungeni kuwatumikia wananchi na siyo kwa faida zao.
 
Ulishawahi kuona wabunge wanachambua mambo ya maana hata siku moja zaidi ya kuuza sura tu.
 
Nimesoma hii report ya Nape kuhusu utaratibu serikali ilioutumia wakuhamishia vipi vya bunge usiku nikacheka sana...

Hoja ya Nape ni kwamba eti watu wapate muda mzuri wa kushuhudia yaliyojiri mchana...

Namuuliza swali moja jepesi sana Nnauye hivi saa tano usiku ni sawa na saa tano asubuhi?

Pili je lisaa limoja linatosha kumpa mlipa kodi habari ilitumia masaa matano wakati ikiwa halisi?

Hivi kwani bunge ni kwaajili ya Nape magufuli au kwaajili ya waliowapa hayo madaraka?
 
KWA KAWAIDA VYOMBO VYOTE VVYA HABARI NDO UTUPASHA HABARI ZILIZOJIRI NA ZINAZOJIRI NA KWA ASILIMIA KUBWA WATANZANIA WENGI VIJIJINI NA MJINI WANAPATA HABARI ZILIZOJIRI KUPITIA TARIFA YA HABARI NA WANAFAAMU KINACHOENDELEA,
KUNA TATIZO GANI BUNGE KUONYESWA RECORDED KATIKA MUDA AMBAO WATU WANAPATA HABARI NJE YA MUDA WA KUANGAIKA ILI KUJIONGEZEA KIPATO MTU BINAFSI ILI KUONDOKANA NA UMAZIKINI WA MTU BINAFSI
 
Tatizo hajui kwamba yeye ni Serikali na hana nguvu kwenye Bunge.Awaachie wabunge waamue nini wafanye.Mbona ile TBC 2 ni full kukataa mauno na gharama zote inatoa Serikali. labda akamdanganye aliyempa uwaziri
 
weeee mbwa wa nape kale makombo yake tayari amekuwekea jalalani kwake mpuuzi wewe; unadhani kukataza watz kuangali wawakilishi ndo utafich a uovu na udhaifu wa serokali dikiteta kama hii?
 
hiv kumbe matusi yanaruhusiwa humu!! bila kuelimishana!!!! hii sasa sio JF!
 
kajifunze kuandika vizuri kwanza, umazikini ndio nini?
 

Ndugu usitake kunambia huelewi nini maana ya taarifa ya habari! Mpaka kuitwa "taarifa ya habari" maana yake ni yaliyokwisha tokea. Hii ni tofauti na "habari ya yanayotokea sasa".

Pia kumbuka kama wewe unahangaika mchana, sio kila mtu anahangaika mchana kama wewe. Wakati wewe umelala kuna wengine wameamka, ukiamka wengine wamelala. Kama haitoshi sio wote wameajiriwa kama wewe, wengine wamejiajiri au hawajapata kazi kabisa na wanahangaika.
 
ni ngumu sana kumuelimisha mwana lumumba kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
 
Hoja ya kufanya kazi kujiongezea kipato ni ya kijinga sana, hili bunge limeanza lini kuoneshwa live, kabla ya hapo watanzania walikuwa na utajiri gani? Kwa nini TV zisizuiwe kurusha matangazo muda wa kazi? Acheni watu waone yanayojiri huko mnaficha nini?
 

Kama ni hivyo si vituo vya habari vingekua vinazimwa usiku ili kwatu walale kwa kua mchana kutwa wamehangaika? Hii yote lengo lake ni kutetea bunge kutoonyeshwa moja kwa moja au ana hoja nyingine?
 
Mi nashindwa kuelewa..wapinzani ni kama watoto wa kambo hawaishi "kompleini"..nnachokiona hapo ni mabadiliko ya ratib,kwani kilivokuwa kinarushwa live mchana mlikua na nyie mnachangia kwa Njia ya simu?
 
iv wafuac wa ukawa ni kip kwanza mnajivunia! Mbon mnakoment matuc badil ya kujenga hoja? Jengen hoja achen hasira siasa haziendeshw kiivo nitukanen na me maana nyie
 
Sasa napata picha kama vile NAPE hatakaa muda mrefu kwenye nafasi aliyonayo hapo kwenye serikali ya Ngosha!
 
Mi nashindwa kuelewa..wapinzani ni kama watoto wa kambo hawaishi "kompleini"..nnachokiona hapo ni mabadiliko ya ratib,kwani kilivokuwa kinarushwa live mchana mlikua na nyie mnachangia kwa Njia ya simu?
Huwezi kurusha bunge zima la siku kwa saa moja tu. mabadiriko ya ratiba yaendane na muda halisi uliotumika. Musiedit hata second moja.
 
Rais ni mwanasayansi, wabunge wanapiga siasa, wanajua media zitawarusha, wanajua watapata wa kuwaunga mkono. Kila siku ukiwasikiliza wanasiasa unaweza kudhani kuwa kuna jambo la hatari sana linatarajiwa kutokea ndani ya siku chache zijazo. Mapinduzi makubwa ya elimu yanahitajika ili kuweza kuwaokoa hawa watoto wanaonza chekechea katika miaka hii ya karibuni, ili na wao wasiweze kuzama katika mtego huu wa kudanganywa na media zetu. Kila kitu kinaandikwa kishabiki, kila mtu anakuwa na mawazo ya kishabiki. Nawashauri wabunge waanze kujipanga ili tija yao iweze kuwarudisha tena ndani ya bunge lijalo. Lakini rais ni mwanasayansi mwenye dhamira njema na uwezo wa kufanya makubwa anao.
 
Huyuu bwana ni katibu mwenezi wa chama, kila afanyacho anafikiria zaidi kipi kitakipa chama chake credit na anasahau kabisa kuwa hata katiba ya nchi inasema kila mtanzania ana haki ya kupata habari. Karne ya leo kuleta hoja kama hii bingeni ni aibu kwa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…