Gharama za Kurusha Mikutano ya Bunge zinatokana na Kodi zetu wananchi, ni fedha zetu wananchi, Tuna haki ya kujua ni kwa namna gani wawakilishi wetu wanatuwakilisha bungeni na pia tunataka kujua kuwa Serikali yetu ina majibu gani juu ya matatizo yetu.
Hii hatua ambayo serikali inaichukua kuzuia sisi wananchi kufuatilia LIVE mambo yetu kupitia bunge letu, ni hatua ya KIDIKTETA, kinyume cha Utawala bora na kinaturudisha nyuma hatua kadhaa katika suala zima la Uwazi.
Ni ajabu serikali ya Magufuli imeanza kupiga hatua moja nyuma kwa kutaka kujipa power zaidi juu ya wananchi kwa kujaribu Kucontrol Information juu ya namna gani nchi hii inaendeshwa.
Ni matumaini yangu kuwa Wananchi hatutokubali kitendo hiki cha "Kioga" kilichofanywa na Wizara ya Habari.
SERIKALI INAOGOPA GHARAMA KWANI FEDHA SI NI KODI ZETU, NA TBC SI NI SHIRIKA LETU?.
Hii ni hatua ya Kisiasa tu na wala haina mantiki yoyote!