TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Haina shida, ikiwezekana wazime kabisa matangazo yao, mbona tutaangalia kupitia STAR TV, live wao wanaonyesha

ha ha haaa

Kumbuka TBC tu ndio anaweza kurusha live, hao wengine walikua wanachukulia TBC
 
Walianza kuzuia Mikutano ya Wapinzani kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu....


Tumekaa kimya..

Sasa wameamua kuzuia na Matangazo ya Bunge.


Jakaya alisaini Open Government Partenership... Huu ndio Uwazi ktk Serikali???
walizuia mikutano wakati huohuo majaliwa akafanya mkutano lindi,..
hii nchii doo
 
kwani mikutano ya ccm ilikuwa inalipiwa na serikali? jaribu kuelewa nini kinalengwa kwenye mada.
 
Kipindi cha Kampeni kilikuwa ni muhimu sana, siyo tu kwa mikutano ya CCM bali ya vyama vyote. Sasa hivi hakuna sababu ya kutumia gharama kama hakuna ulazima.


Hivi watu wa Lumumba mnashabikia hata UROJO kisa nini ? Ukereketwa ???????????? Mna boa sana
 
Mheshimiwa spika,
kutokana na hali hii, TBC
imeona ni busara
kubadilisha mfumo wa
utangazaji wa shughuli za
bunge ili kukabiliana na
kupanda kwa gharama za
uendeshaji, hivyo basi, TBC
imeona ni busara kuanzia
mkutano huu wa bunge
iwe inarusha baadhi ya
matangazo ya bunge moja
kwa moja yaani live ikiwa
ni njia ya kubana
matumizi.



==========================


Hapa watakuwa wanachagua mikutano wanaona ina faida kwao na mingine hatutaiona
 
Huu ni uhuni mkubwa sana. Wanaficha madudu yao wakiogopa wataonekana. Kams sababu ni gharama waruhusu tv nyingine idadi yeyote warushe live. Tv inaendeshwa kwa kodi za wananchi anasema gharama kubwa. Hizo binafsi kama azam na star tv wasemeje. Tbc si inafanya biashara kurusha harusi, hii sio haki kabisa. Ameshindwa kutoa sababu za msingi. Magufuli je atakubaliana na hili? Wananchi hatuna haki ya kuwaona tuliowachagua wakituwakilisha bungeni kama wanatutendea haki. Hata hiyo saa nne wasirushe
Hapa wabunge wasimamena waimbe nyimbo zote mpaka koeleweke!
 
UNo longer at easy ...alisema Chinua Achebe.Leo nimeona mantiki ya maneno yake katika nchi yangu.Tbc haitaonyesha tena bunge live sababu ni kubana matumiz pili et watu watakuwa kwenye shughulizao mchana HAPA KAZI TU....Binafsi sababu ya matumizi haina uzito Tbc ilipoanzishwa tulijua lazima ,tutaingia kwenye matumizi ,hilo li wazi ,kama tunataka kupunguza matumiz Tbc,ifutwe kabisa haina maana ya kuwepo kwasababu inatugharimu .Sababu ya pili eti watu mida ya asubuhi na mchana wapo kwenye kazi mbona mikutano ya ccm ,ilikuwa inaonyeshwa live saa tatu asubuhi ?? au watu kipindi cha kampeni walikuwa hawana kazi ?? baada ya kampeni watanzania wanakazi je wadau ambao ni wananchi wameshirikishwa kuhusu Tbc yao kuwa mzigo kwao katika kuwapasha habari au ni udikteta wa waziri wa habari ?.Serekali ikumbuke demokrasia inagharama zake mojawapo nikuwapa watu habari.Wadau wa habari na wananchi wasipoangalia tutakuwa kama nchi zinazo abudu mifumo ya kidikteta. UHURU WA HANARI NA KUPATA HABARI ANAUZKA NAPE,ila historia itamhukumu.Baada ya miaka mitati mbele tunaweza.kubaki na vyombo vya habari vya chama na serekali kasi ya kupata habari inapunguzwa.Katika dunia ya sayansi ma teknolojia sis tunaabudu bado katika kuwapimia watu habari .Mwisho kabisa kama uhuru wa habari unadidimizwa hivyo tutegemee mafisadi wa chache wa kineemeka kwa kisingozio cha hapa kazi tu.
Mbona ITV hawaonyeshi na hatulalamiki
 
ukiona vyaelea ujue vimeundwa,..
hayo maamuz yamekaliwa chini,..na pengine nape kapokea hoja2 kutoka kwa boss wake,..
yeye katekeleza2,...
ccm nia yao siku zote ni kumbana mtz ili watawale milele,.kwanini wanafanya hivi
alaf wanazuga ni democratic country,...i hate them,...
vipi ITV/AZAM?????????
HAPA NAPATA PCHA ukawa inabidi tuwe na kituo chetu private cha chama
 
Nape ametoa tangazo hilo muda huu!

Baadhi ya matukio ya shughuli za bunge yatarekodiwa na kurushwa kuanzia saa nne usiku!


arab's camel story! Nakumbuka mkutano uliopita baadhi ya wabunge walipendekeza Tbc/Tv zisioneshe kabisa vipindi vya bunge.Kisa wabunge wa upinzani hawana nidhamu! Wenye busara zao wakawaambia mtakua mmewanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kutoka kwenye chombo chao.Toka kipindi hicho walikuwa wanatafakari waje na mbinu gani ya kupunguza makali ya wapinzani kuonwa na wananchi.Hiyo ni hatua ya kwanza,hatua ya pili itakuwa ni kufuta kabisa
!
 
Kumbe TBC inaangaliwa zaidi kuliko tv nyingine sasa mbona walikuwa wanaiponda ama kweli ni ukweli na uhakika.
Inaangaliwa kipindi cha bunge....ndo mahali unapata habari kuhusu mbunge wako serekali inapojibu hoja ....za matatizo ya wananchi
 
Nape asitake kuendesha hiyo wizara kama anaendesha akaunti yake ya fb kwamba ukimuuzi tu anakbrock
 
Back
Top Bottom