TBT: Unakumbuka nini kuhusu mabomu ya Mbagala (2009) na Gongo la Mboto (2011)?

Hii ilionesha ni namna Gani hili jeshi la wavunja matofali lilivyo na uwezo mdogo kijeshi.Yaani silaha tu kuzihifadhi vizuri limeshindwa Hadi imepelekea milipuko kutokana na uchakavu na mazingira mabovu?.Kama kutunza tu limeshindwa je wanauwezo kweli wa kuenda na wakati kama majeshi mengine kama jeshi la Rwanda?.
 
Unaongea kama vile wanahifadhi embe kwenye friji au kama vile mabomu yanaongea!!
 
Waziri wa Ulinzi hakuhojiwa na Polisi.
Nakumbuka pia Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa anasema," Nchi yetu safi kabisa. Siyo kama jirani zetu. Hapa hatuzalishi wakimbizi. Hapa tunapokea wakimbizi."
Kesho yake yale mabomu yakalipuka na wakimbizi wengi walikwenda Stadium.
Halafu nasikia watoto wengi walipotea.
Af,nakumbuka nilikuwa nimefunga kula chakula for two weeks non-stop .
Niko Mikocheni naisikiliza Ile milipuko inadunda kwenye moyo wangu.
Nikashukuru siko karibu kule.
Halafu ilikuwepo tafrifa kwenye garden ya Ikulu
Nilikuwa na - chat na yule Kamanda wa Jeshi anaitwa Mbowe, alikuwa Jeshini amekamatwa finances za Jeshi.
Nikamuuliza unamfahamu Freeman.
Akasema ni,sijui alisemaje,yule Freeman ni mdogo wangu au kama mtoto wangu.
Basi kesho yake asubuhi,for some reason, Kikwete akamchagua yule kuiongoza tume ya kupelekeza lile tukio.
 
Mabomu ya Gongolamboto.

Nipo nyumbani natazama tv, sasa majira kama ya saa moja nikaanza kusikia miungurumo kama, basi kwakuwa tikuwa sana na shida ya maji haya kutoka zaidi ya siku 4.

Nilitoka nje nikiwa na mabeseni kwa ajiri ya kukinga maji, hivyo nikayayegesha kama kawaida, ila kilichonishangaza kila nikipiga jicho angani sioni dalili za mvua ingawaje miungurumo imepamba moto.

Ndipo nilipo rudi ndani kukutana na maandishi chini ya tv, yakielezea milipuko inayo endelea kulindima huko Gongolamboto.

babu wa maraha.
 
Nchi yetu ni kweli kabisa hatuzalishi wakimbizi. Kuna tofauti kubwa kati ya wakimbizi na watu walioondoka kwenye makazi yao au kuelekea kuishi sehemu nyingine. Mtu ambaye hajavuka mpaka wa Kimataifa sio mkimbizi. Sasa hawa wa Mbagala na Gongolamboto walivuka mpaka gani wa Kimataifa??1
 
Nilijua Kagame ndio katuvamia Sasa Mkwere na Makamanda wake wanauona Moto kumbe.

Nilikuwa shule Asee niliwasomba watu kwa stori za Nini kinaendelea kuja kugeuka Hilo mobb lilivyonizunguka kuskiza Counter Intel wa Domitory namba 3 nikimwaga fiction.
Hakika watanikumbuka Zaid ya hayo mabomu yenyewe.
#CHAI.
 
Mlipo wa mwanzo ulikuwa mwaka 2003 au 2004 kama sikosei hapo Gongo la Mboto…Inaonekana tukio hili wengi hawalikumbuki sana.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ yani ww matukio yote mawili ulikuwemo, unatakiwa kuwa steringi wa hii movie aiseeπŸ˜‚πŸ˜‚​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…