TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Brother Scandinavia ilikuwa cha mtoto. Kuna basi lilikuwa linaitwa HOOD likitoka Dar SAA 12 asubuhi SAA 8:30 mchana mpo TUNDUMA lile basi lilikuwa linakimbia wajameni sijawahi ona nchi hii

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Safi sana mkuu sijawahi kuitokea hii bus,Leo hii ,umbali ule ule with more modern buses, eti bus ya kwanza tunduma kuanzia 20:00hrs ,na bus hii imeondoka Dar saa 6am it's craze, buses zinatakiwa zianze kuingia from 16:00 hrs
 
Hii kampuni nayo itakumbukwa japo Haina muda tangu anguko lake
Kuna kipindi nilikuwa naifanyia timing pale Bunda ikiwa inatokea Musoma, mapema sana nilikuwa naingia Mwanza tofauti kama ningepanda gari la moja kwa moja kutoka Mugumu huko
 
Daaah umenikumbusha miaka ya Scandinavia,Kuna dereva alivurugwa,tulisafiri Dsm -Mbeya huku ukipigwa wimbo mmoja tu wa K-Basil Ft Bizman & Stara Thomas-Riziki

NB-Mpaka leo huo wimbo haujawahi kunitoka kichwani

Pia, nimewahi kusafiri na HEKIMA DSM-Mbeya ila ilikuwa inaishia Tunduma,saa Tisa na robo nikashuka Mwanjelwa na kuwahi game ya Prisons vs Yanga,enzi za kina Henry Morice,Primus Kasonso,Shadrack Nsajigwa,Yona Ndabira
 
Shukrani mkuu. Kampuny ya Air Msae gari lake liliwahi tumbukia mtoni kama kumbukumbu zangu ni saba basi ni mto Pangani.
Air Msae ilipigwa kibega na Dar express Chalinze miaka ya 90 walianza kushindana tangu Korogwe ajali mbaya sana.
 
Hehehe mimi team mnazi wa scania. Sijawahi penda michina... nimejaribu kuwa msichana nimeshindwaaa[emoji23][emoji23] labda ni kwasababu nimelelewa mazingira ya haya magari... japo siku hizi nna uoga kidogo. Ila sitokaa nisahau ajali za air msae na buffalo. Memmories hurt jamani[emoji26]
Tunawashukuru sana madereva na watoa huduma wote kwa huduma zao zilizotukuka. Tunaweza sema udereva wa miaka hiyo ulikua very talented..
 
Mara ya kwanza kwenda dar,nilipanda Sumry Songea to Dar,
 
Brother Scandinavia ilikuwa cha mtoto. Kuna basi lilikuwa linaitwa HOOD likitoka Dar SAA 12 asubuhi SAA 8:30 mchana mpo TUNDUMA lile basi lilikuwa linakimbia wajameni sijawahi ona nchi hii

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Mwongo mkubwa wewe. Mnakoleza stori hadi inaboa sasa. Hakuna basi lililowahi kutoka Dar saa 12 likafika Tunduma saa 8 na nusu mchana. Hata la saa 10 halipo. Sio kila mtu anayesoma comments hapa ni mpumbavu.
 
Hatujaona Torino za Hood zilikuwa na madirisha madogo juu kama mabanda ya njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…