TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Brother Scandinavia ilikuwa cha mtoto. Kuna basi lilikuwa linaitwa HOOD likitoka Dar SAA 12 asubuhi SAA 8:30 mchana mpo TUNDUMA lile basi lilikuwa linakimbia wajameni sijawahi ona nchi hii

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Safi sana mkuu sijawahi kuitokea hii bus,Leo hii ,umbali ule ule with more modern buses, eti bus ya kwanza tunduma kuanzia 20:00hrs ,na bus hii imeondoka Dar saa 6am it's craze, buses zinatakiwa zianze kuingia from 16:00 hrs
 
Hii kampuni nayo itakumbukwa japo Haina muda tangu anguko lake
Kuna kipindi nilikuwa naifanyia timing pale Bunda ikiwa inatokea Musoma, mapema sana nilikuwa naingia Mwanza tofauti kama ningepanda gari la moja kwa moja kutoka Mugumu huko
 
Daaah umenikumbusha miaka ya Scandinavia,Kuna dereva alivurugwa,tulisafiri Dsm -Mbeya huku ukipigwa wimbo mmoja tu wa K-Basil Ft Bizman & Stara Thomas-Riziki

NB-Mpaka leo huo wimbo haujawahi kunitoka kichwani

Pia, nimewahi kusafiri na HEKIMA DSM-Mbeya ila ilikuwa inaishia Tunduma,saa Tisa na robo nikashuka Mwanjelwa na kuwahi game ya Prisons vs Yanga,enzi za kina Henry Morice,Primus Kasonso,Shadrack Nsajigwa,Yona Ndabira
 
Shukrani mkuu. Kampuny ya Air Msae gari lake liliwahi tumbukia mtoni kama kumbukumbu zangu ni saba basi ni mto Pangani.
Air Msae ilipigwa kibega na Dar express Chalinze miaka ya 90 walianza kushindana tangu Korogwe ajali mbaya sana.
 
Screenshot_20220819-075639_Lite.jpg
 
Hehehe mimi team mnazi wa scania. Sijawahi penda michina... nimejaribu kuwa msichana nimeshindwaaa[emoji23][emoji23] labda ni kwasababu nimelelewa mazingira ya haya magari... japo siku hizi nna uoga kidogo. Ila sitokaa nisahau ajali za air msae na buffalo. Memmories hurt jamani[emoji26]
Tunawashukuru sana madereva na watoa huduma wote kwa huduma zao zilizotukuka. Tunaweza sema udereva wa miaka hiyo ulikua very talented..
 
Mara ya kwanza kwenda dar,nilipanda Sumry Songea to Dar,
 
Brother Scandinavia ilikuwa cha mtoto. Kuna basi lilikuwa linaitwa HOOD likitoka Dar SAA 12 asubuhi SAA 8:30 mchana mpo TUNDUMA lile basi lilikuwa linakimbia wajameni sijawahi ona nchi hii

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Mwongo mkubwa wewe. Mnakoleza stori hadi inaboa sasa. Hakuna basi lililowahi kutoka Dar saa 12 likafika Tunduma saa 8 na nusu mchana. Hata la saa 10 halipo. Sio kila mtu anayesoma comments hapa ni mpumbavu.
 
1. TAWAQAL EXPRESS

View attachment 2054358

Pichani ni basi la kampuni ya Tawaqal. Kampuni hii ilikuwa balaa. Njia ya Dar - Mbeya, Dar- Kyela, Dar - Tunduma na Dar - Songea.

Kampuni hii ilikuwa na madereva mahiri kwelikweli. Miongoni mwao alikuwepo GIRIKI.

Jamaa alitoka Dar saa 12 asubuhi akaingia Mbeya saa 7 mchana.

2. SHABAHA EXPRESS

View attachment 2054378

Kampuni hii ilibamba sana miaka ya nyuma ikisafirisha abiria kati ya Dar na Arusha. Jamaa walikuwa wakishindana na wakongwe wa zamani kama Ngorika, Dar EXPRESS nk

3. SCANDINAVIA EXPRESS

Kampuni ya mabasi ya Scandinavia Express ni kampuni pekee ya kitanzania iliyowahi kutokea kwa kuwa na huduma za uhakika na za viwango vya hali ya juu kabisa kulinganisha na huduma zinazotolewa na kampuni za sasa. Kampuni hii ilijijengea jina kubwa na sifa nzuri ndani na nje ya nchi kwa huduma bora walizokuwa wakizitoa kwa abiria wake na pia kuliletea sifa taifa la Tanzania kwa kujulikana kuwa na mabasi ambayo ni quality na high class.

View attachment 2054407
Kampuni ya Scandinavia ilianzishwa zaiidi ya miaka thelathini na tano (35) iliyopita ikiwa na mabasi machache tu aina ya LEYLAND na ilipofika mwaka 1982 kwa mara ya kwanza Scandinavia walinunua basi lao la kwanza la kisasa kutoka kampuni ya SCANIA TANZANIA COACHES aina ya SCANIA ambalo kutokana na ubora wake na uzuri wake kwa kipindi hicho waliamua kulitumia kwa safari yao mpya waliyoianzisha ya Dar es salaam hadi Iringa.


BASI LA KWANZA LA KISASA KUNUNULIWA NA SCANDINAVIA 1982

Kadiri mahitaji ya usafiri yalivyokuwa yakiongezeka ndipo michirizi ya rangi ya BLUU,KIJIVU na NYEKUNDU ikaanza kuonekana katika mabasi mengi zaidi yaliyokuwa yakisafirisha abiria karibia kila kona ya Tanzania.

Ilipofika mwaka 2001 kampuni ya Scandinavia walianzisha safari yao ya kwanza kabisa kutoka nje ya nchi kwa safari ya Dare es salaam hadi Nairobi nchini Kenya,ambapo mafanikio ya ruti hiyo yalipelekea kuzaliwa kwa ruti nyingine kati ya Nairobi hadi Mombasa na Mombasa hadi Dar es salaam. Katika mwaka wa 2002 kampuni ya Scandinavia walipanua wigo wa huduma zao kwa kuanza ruti mpya ndani ya Afrika mashariki kwa safari za Dare es salaam hadi Kampala nchini Uganda.

Ilipofika mwaka 2003 kampuni ya Scandinavia ilipanua wigo zaidi kwa kuanza kwenda katika mji mkuu wa nchi ya Zambia Lusaka.

Wakati huo wote kampuni ya Scandinavia ilikuwa chini ya mkurugenzi na mwanzilishi wake MR.MUHAMED ABDULLAH.



Kampuni ya Scandinavia ilianza kutumia mabasi ya kisasa mwaka 1982 na kuanzia hapo walikuwa wakiongeza mabasi kadili ya mahitaji ya kampuni na abiria pia na kufikia jumla ya mbasi 100 ambayo yalikuwa yakitoa huduma za usafiri ndani na nje ya nchi na mengi ya mabasi hayo yalikuwa ni ya kisasa yaliyonunuliwa kutoka kiwanda cha SCANIA na MARCOPOLO kilichopo nchini BRAZIL

4. KISWELE

View attachment 2054432


Kiswele ndilo basi la kwanza Tanzania kuwa na injini nyuma.

Basi hili likitamba sana siku za nyuma na miongoni mwa njia ilizotamba ni Dar- Mbeya, Dar - Tunduma, Dar- Songea.

Mpaka leo hili basi linakumbukwa

5. SUMRI

View attachment 2054445

View attachment 2054448

Kampuni hii sasa haipo tena. Kampuni hii ilivuma sana ikihudumu njia ya Dar -Mbeya, Dar- Sumbawanga na Mbeya- Sumbawanga.

6. NGORIKA

View attachment 2054451


Kampuni hii kongwe imehudumu miaka mingi ikifanya safari zake kati ya Dar na Arusha.
Hatujaona Torino za Hood zilikuwa na madirisha madogo juu kama mabanda ya njia
 
Back
Top Bottom