TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

kwani si kweli watoto wanafuja mali za kampuni kwa starehe... kampuni aliyoijenga kwa tabu alafu watoto wanakuja kula bata tu.. hamna wanachokijua
 
Nakumbuka miaka ya 1996 au 95 hivi, nilipanda basi la Tawaqal kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda( mkoa wa katavi kwa sasa) namkumbuka konda wake alikua anaitwa Nassoro, mwarabu hivi . Kweli zamani sana
 
Ina maana ISLAM na SADIQ LINE hukuwakutaga!?
Nashangaa wadau wamejisahaulisha zamani ilikuwa huwezi kutaja route ya Dar Moro bila kuwagusa Islam,Sadiq Line,Hood na Abood..Hizo gari zilikuwa na upinzani wa hali ya juu kinoma kama vita vile halafu huwezi kuamini ukiambiwa wamiliki wa basi hizo wote wana relationship nzuri sana na wanasaidiana wakati wa matatizo..Enzi hizo Sadiq Line wakati anaanza akataka kutembelea kiki ya ushindani na Hood akakuta vijana wa Hood enzi hizo tupo moto tumeprint hadi fulana wachangamfu kinoma sio wale Dar au wale wa Moro wote tupo machachali kinoma basi tukampiga kijembe tukaandika mabasi yetu "jino moja mswaki wa nini!?" Hapo ilikuwa ni kijembe kwa sadiq line aliyetaka kushindana na sisi wakati alikuwa na basi moja tu wakati anaanza basi na wao walivyokuwa watata wakajibu eti "meno mengi lakini yote mabovu" enzi hizo usipokuwa na team nzuri ya wapiga debe huambulii abiria sisi tulikuwa na wapiga debe enzi zile Abood alikuwa anapata ajali sana basi wapiga debe wetu wakimuona abiria anapanda Abood wanaenda kumlilia 😂😂aloo ukiwa na roho ndogo unaweza kuhairisha kupanda abood watu wanakulilia design ile "anaenda kufa jamaniii mama weee" Halafu basi kama halijajaa pale stend kulikuwa na hela maalumu ya wapiga debe boss alikuwa ananipa mimi inspector niende nkawarushie sandakalawe wapiga debe basi nikifika Kibaha namwaga mahela,Chalinze,Mlandizi halafu huyo nashuka narudi Dar mpaka gari linafika Moro abiria wote nawekewa mimi hakuna basi lolote linaloweza kutuovertake kuchukua abiria wapiga debe walikuwa wananikubali kinoma nikikutana nao wengine wanashangaa jinsi nilivyobadilika kama sio mimi vile
 
Meno mengi yote mabovu
 
Very interesting hapo kwa Kamanda SIRRO.
 

Hood limited
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…